Monday, October 26, 2020

Lwandamina apewa masharti magumu

Must Read

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian...

NA HUSSEIN OMAR,

KATIKA kuhakikisha Yanga inakuwa moto wa kuotea mbali kwenye mechi za kitaifa na kimataifa, uongozi wa klabu hiyo umeamua kumpa mkataba wa miaka miwili, Mzambia George Lwandamina na ndiye atakayechukua nafasi ya Kocha Hans van der Pluijm.

Yanga imefikia uamuzi huo baada ya kuona timu yao ikiwa imeshuka kiwango na hivyo kuhofia huenda wakashindwa kutetea taji lao la ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu.

Hivi karibuni, baada ya Yanga kutoka sare ya 1-1 dhidi ya watani zao Simba, uongozi wa Wanajangwani hao ulikutana na kutathmini juu ya mwenendo mzima wa kikosi chao, lakini pia wakiyarejea matokeo ya kufungwa 1-0 na Stand United mjini Shinyanga.

Mara baada ya kusaini mkataba huo jana, Lwandamina anatarajia kuondoka nchini leo kurejea kwao Zambia kuaga kabla ya kurejea tena nchini Desemba mwaka huu kuanza kukinoa kikosi cha timu hiyo.

Chanzo cha ndani cha habari kutoka Yanga kilisema baada ya kusaini mkataba huo Lwandamina amewaahidi mambo mazuri viongozi wa timu hiyo na kuahidi kuifikisha mbali katika michuano ya kimataifa mwakani.

“Kocha amepewa mkataba mgumu sana. Kuna kipengele katika mkataba wake, kinachoonyesha moja ya kazi kubwa aliyonayo mbeleni ni kuhakikisha Yanga inacheza hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika na kucheza fainali,” kilisema chanzo hicho.

Pia mkataba huo unaonyesha kuwa Lwandamina amepewa rungu la kusajili mchezaji yeyote anayemtaka na gharama yoyote ili mradi ahakikishe Yanga inafika mbali katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika mwakani.

“Suala kubwa ambalo Mwenyekiti anataka hapa ni kwamba, Yanga ifike mbali katika michuano ya kimataifa lakini pia heshima yake irudi ndio maana kapewa mkataba mgumu,” aliongeza.

Pluijm anakuwa kocha wa tatu kuondolewa kwa mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu Bara katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita, lakini chanzo kikiwa ni matokeo ya mechi dhidi ya Simba.

Lwandamina ni nani?

Beki huyu wa zamani wa Mufurila Wanderers na timu ya taifa ya Zambia alizaliwa Agosti 5, 1963 na kustaafu kucheza soka mwaka 1995 kutokana na majeraha ya goti yaliyomsumbua kwa kipindi cha miaka mitatu.

Mwaka 2014, aliteuliwa rasmi kuwa kocha mkuu wa Zesco United na kufanikiwa kutwaa mataji mawili ya ndani katika msimu wake wa kwanza.

Pia, Lwandamina alifanikiwa kubeba tuzo ya kocha bora wa Zambia mara mbili mfululizo, mwaka 2014 na 2015.

Akiwa na Zesco, Lwandamina anajivunia rekodi ya kuiongoza klabu hiyo kucheza hatua ya nusu fainali Ligi ya Mabingwa Afrika mwaka huu akivuka kwenye kundi la kifo.

Zesco walipangwa Kundi A sambamba na Wydad Casablanca ya Morocco, Al Ahly ya Misri na Asec Mimosas ya Ivory Coast, walimaliza wakiwa na pointi tisa na kushika nafasi ya pili nyuma ya timu ya Morocco.

Dhidi ya Al Ahly ambao wamekuwa wakiisumbua sana Yanga kila wanapokutana, Lwandamina aliiongoza Zesco kupata pointi nne, wakishinda 3-2 mchezo wa kwanza nyumbani na kulazimisha sare ya bao 2-2 ugenini.

Timu ya taifa

Lwandamina, aliyepata mafunzo ya ukocha nchini Ujerumani na Uholanzi, alianza kukinoa kikosi cha vijana wa Zambia U-20 mwaka 2003 hadi 2008 na kufanikiwa kutwaa Kombe la Cosafa.

Mwaka 2007, aliiongoza timu hiyo kucheza nusu fainali ya Kombe la Afrika kwa vijana na kupata tiketi ya kushiriki fainali za Kombe la Dunia la vijana yaliyofanyika Canada, ambapo Zambia waliishia hatua ya 16 bora.

Mwaka 2005 aliteuliwa kuwa kocha msaidizi wa timu ya taifa ya Zambia chini ya Kalusha Bwalya, akichukua nafasi ya kocha wa zamani wa Simba, Patrick Phiri.

Lwandamina aliendelea na kazi hiyo chini ya Herve Renard aliyechukua nafasi ya Kalusha.

Mwaka 2010 baada ya Renard kubwaga manyanga, Lwandamina alipewa kwa muda kuiongoza Zambia kwenye michezo miwili ambayo alipoteza yote na kunyimwa kibarua hicho.

Lakini hii haikuwa mwisho wa safari yake na timu ya taifa ya Zambia ambapo Mei 2015, siku tano kabla ya pambano la kufuzu fainali za Afrika dhidi ya Guinea-Bissau, Lwandamina alipewa jukumu la ukocha mkuu wa taifa hilo.

Akiwa kocha mkuu, Lwandamina aliiongoza Zambia kufuzu fainali za Afrika 2016 ambapo walitolewa kwenye hatua ya mtoano na Guinea kwa changamoto ya mikwaju ya penalti.

Ikumbukwe Wanajangwani hao walimtimua kocha Ernest Brandts na benchi zima la ufundi baada ya kipigo cha mabao 3-1 dhidi ya Simba katika mchezo maalumu wa kirafiki maarufu Nani Mtani Jembe iliyochezwa Uwanja  wa Taifa Desemba mwaka 2013.

Yanga ilifanya hivyo tena kwa mwaka uliofuata kwa Mbrazil, Marcio Maximo, baada ya kufungwa 2-0 na Simba katika mechi ya Mtani Jembe iliyochezwa Desemba 13, 2014 na mikoba yake kuchukuliwa na Pluijm.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya kuwa na umri wa miaka...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian Mbappe na Neymar, kwenye mechi...

IBRA:Kifaa kipya Konde Gang aliyetembea kwa mguu kumwinda Harmonize

NA BRIGHITER MASAKI UKITAJA vijana wanaofanya vizuri katika mziki wa bongo fleva, huwezi kukosa kumtaja msanii chipukizi anayefahamika zaidi...

Jay-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas

-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas New York, Marekani HAKUNA shabiki wa Hip hop asiyelifahamu...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -