Thursday, October 29, 2020

LWANDAMINA ATAKA MECHI MBILI KUIUA SIMBA

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

NA ZAINAB IDDY

KOCHA mkuu mpya wa Yanga, George Lwandamina, amesema anahitaji mechi mbili tu kuwasoma wapinzani wake Simba na kumaliza mchezo.

Lwandamina ambaye ameingia kandarasi ya miaka miwili ya kuinoa Yanga, amewatoa wasiwasi mabosi wa klabu hiyo kwamba wasiwe na hofu kwani amekuja kuendeleza pale ambako mtangulizi wake Hans van der Pluijm amekomea.

Kocha huyo wa zamani wa Zesco United ya Zambia, anakabiliwa na mtihani mgumu baada ya mabosi wake wapya kumpa masharti ambayo ni kuhakikisha Yanga inatetea ubingwa wake, kuendeleza ubabe dhidi ya Simba na kufanya vizuri zaidi katika michuano ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF), ambapo katika michuano iliyopita ya  Kombe la Shirikisho iliishia hatua ya makundi.

Lakini kocha huyo Mzambia hajatikiswa na masharti hayo badala yake amewataka mabosi kutulia tuli akisema watafaidi matunda mazuri ya ujio wake.

Taarifa ambazo BINGWA limezinasa kutoka kwa mmoja wa mabosi wa Yanga ambaye hakutaka kutajwa jina, amesema  Lwandamina amewahakikishia anafahamu umuhimu wa kushinda mechi dhidi ya wapinzani wao Simba, hivyo atahakikisha anaendeleza rekodi za Pluijm.

“Unaweza kudhani ni masihara lakini huo ndio ukweli, Lwandamina ameomba kuiangalia Simba michezo miwili tu iwe kwa CD au live ‘moja kwa moja uwanjani’, kama itapatikana fursa baada ya hapo achwe afanye kazi yake.

“Hakupendekeza ni mechi gani atakayoiangalia pindi inapocheza na Simba, ila ametaja ni mbili tu kwani anaamini anaweza kuifunga Simba bila kutumia nguvu nyingi kwakua aliwashawahi kufanya hivyo alipokuwa na kikosi cha Zesco kwenye mechi ya kirafiki,” alisema kigogo huyo wa Yanga.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -