Wednesday, October 28, 2020

Lwandamina kutua Dar kesho

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

NA SAADA SALIM

DILI limetiki. Hivyo ndivyo unavyoweza kusema baada ya kocha mkuu wa Zesco ya Zambia, George Lwandamina, kuamua kuachia ngazi kuinoa timu hiyo na sasa Yanga wanatakiwa kuanza kujipanga uwanja wa ndege kupokea mabegi yake.

Lwandamina, anatarajiwa kutua nchini kesho kwa ajili ya kuifundisha timu hiyo kwenye michuano ya Ligi Kuu Tanzania Bara na Ligi ya Mabingwa mwakani.

Kocha huyo alijiuzulu mara baada ya kumalizika kwa mechi yao na Nkana FC ambapo uongozi wa Zesco umekiri kupokea barua ya kuachia ngazi kwa kocha huyo, huku nafasi yake ikishikiliwa na msaidizi wake, Mpangaji Chembo.

BINGWA lilizungumza kwa nyakati tofauti na wachezaji wawili wa timu hiyo, akiwemo Misheck Chaila ambapo alisema Lwandamina ni kocha mzuri na mara nyingi anapokaa na timu huwa ni zaidi ya kocha.

“Kocha mzuri pia ni mtu mwenye mbinu nyingi sana katika mchezo wa soka, mshindani pia hapendi kufungwa,” alisema mchezaji huyo.

Naye Juma Luizio ambaye ni Mtanzania anayekipiga katika kikosi cha Zesco, alisema anasikitika sana kuondoka kwa kocha huyo kwake ni zaidi ya mzazi.

“Binafsi inaumiza kwani tumemzoea kwa jina la Kocha G, hivyo ni mwelewa sana, baada ya kutuaga rasmi kila mchezaji amebaki na huzuni, nina imani msimu ujao wachezaji wengi wataondoka,” alisema Luizio.

Kuondoka kwa Lwandamina moja kwa moja anakuja Tanzania kuanza kazi rasmi kukinoa kikosi cha Yanga, ambapo mzunguko wa pili ataonekana katika benchi la ufundi la timu hiyo akichukuwa nafasi ya Hans Pluijm.

Lwandamina aliyeiongoza Zesco ya Zambia kwenye michuano ya kimataifa ya Ligi ya Mabingwa Afrika mwaka huu na kuiwezesha kutinga nusu fainali, imeelezwa atakuja na kocha msaidizi na wa viungo.

Ujio wa Lwandamina unatokana na uongozi wa Yanga kuelezwa kukatisha mkataba wa kocha mkuu wa timu hiyo,  Hans van der Pluijm na msaidizi wake, Juma Mwambusi.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -