Wednesday, January 20, 2021

LWANDAMINA SAFI, WACHEZAJI WALIPWA YANGA

Must Read

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi...

NA CLARA ALPHONCE

BAADA ya juzi kusambaa kwa uvumi kuwa Yanga wameamua kuachana na kocha wao George Lwandamina baada ya kufungwa na mahasimu wao Simba kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii, uongozi wa klabu hiyo umeamua kumalizana na Mzambia huyo kwa kuingia naye mkataba wa mwaka mmoja.

Akizungumza na waandishi Makao Makuu ya Yanga yaliyopo Jangwani, Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa klabu hiyo, Boniface Mkwasa, alisema kuwa taarifa zilizokuwa zimezagaa juzi kuwa wameachana na kocha huyo, si za kweli ni za kutaka kuwaharibu kisaikolojia ili waweze kufanya vibaya kwenye ligi.

“Taarifa hizo si za kweli, sisi bado tupo na Lwandamina na leo (jana) saa 8:00 tunaingia naye mkataba mpya wa mwaka mmoja baada ya ule wa awali wa miezi sita kumalizika Julai 16, mwaka huu.

“Tumechelewa kuingia naye mkataba mpya kutokana na mwenyewe kuomba apewe mkataba ili aweze kumpelekea mwanasheria wake aweze kuupitia kwanza kabla ya kuusaini, jana katurudishia na sisi tumeridhika na ofa yake na tumeamua kumalizana naye kabisa,” alisema Mkwasa.

Katibu huyo aliongeza kuwa ukimya mwingi waliokuwa nao kwenye usajili umefika wakati wa watu kuona majibu yake na walianza kwenye mechi yao dhidi ya Simba, timu ilionyesha uwezo mkubwa tofauti na matarajio ya wengi.

Alisema timu yao ipo kamili kwa ajili ya kuanza ligi na hawatawadharau Lipuli kwani nia yao ni kuanza vizuri safari ya kutetea ubingwa wao kwa kupata matokeo.

Alisema wachezaji watakaokosa mchezo huo ni kipa Ben Kalolanya, Geofrey Mwashiuya na Chirwa ambao ni majeruhi.

Wakati huo huo, Mkwassa amesema kuwa bado hawajapata barua rasmi juu ya kufungiwa kwa mchezaji wao Pius Buswita ila wanasikia kwenye vyombo vya habari kuwa wamefungiwa mwaka mmoja kwa kudaiwa kusaini mkataba katika klabu mbili.

Alisema kama ni kweli watakuwa wamemfungia, basi wao kama klabu watakuwa bega kwa bega kumtetea hadi dakika ya mwisho kwa ajili ya kipaji chake.

Kuhusu mauzo ya jezi zao, alisema jana wamekutana na mawakala wote wanaouza jezi za Yanga na kupeana mikakati mbalimbali kwa ajili ya kulinda nembo ya klabu yao na kuiongezea yao mapato.

Aliongeza kuwa wamekubaliana kuwa jezi hizo zitakuwa zinapatikana katika klabu ya Yanga, pia amewataka wanachama kuwa watulivu kwa sasa na kuacha kununua jezi yoyote ya mtaani hadi watakapowapa taarifa mpya.

Pia, Mkwassa amelitaka Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kutoa mwongozo juu ya adhabu ya mshambuliaji wao, Obrey Chirwa, ambaye amesimamishwa kucheza mechi za Ligi Kuu Bara kwa madai ya kumfanyia vurugu mwamuzi katika mchezo wao dhidi ya Mbao FC msimu uliopita.

Mbali ya Chirwa, wachezaji wengine ambao wamesimamishwa na TFF kutokana na kosa hilo ni Simon Msuva na Deus Kaseke ambao kwa sasa hawapo Jangwani.

“Unajua barua hiyo ilisema wanatuhumiwa ila haikuwa na adhabu, hivyo tunaomba kamati husika kukaa na kutoa mwongozo juu ya hilo, hata kama ni adhabu, basi wapewe ili waweze kuitumikia kuliko sasa wanatumikia adhabu ambayo haipo,” alisema.

Alisema pengo la mchezaji huyo lilionekana kwenye mchezo wao dhidi ya Simba na kama angekuwapo siku hiyo, matokeo yangekuwa tofauti na waliyopata.

Katika hatua nyingine, wachezaji wa Yanga jana walilipwa mishahara yao, ikiwa ni siku moja kabla ya kuanza kwa Ligi Kuu Bara.

BINGWA liliwashuhudia baadhi ya wachezaji wa timu hiyo wakiingia kwenye ofisi za klabu hiyo kupokea chao tayari kukinukisha katika mchezo wa kesho dhidi ya Lipuli ya Iringa kwenye Uwanja wa Taifa.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na ndiyo maana timu hiyo imeshinda...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi Kuu Tanzania Bara katika kipindi...

JDart Nation wapanga kutawala Africa

CHRISTOPHER MSEKENA MWANAMUZIKI na bosi wa JDart Nation, JDart, amesema miongoni mwa mipango yake kwa mwaka 2021 ni kuhakikisha...

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki za Ligi Kuu Tanzania Bara...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -