Sunday, November 29, 2020

MAANDALIZI YA ARS KLINIKI YAKAMILIKA

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA MWANDISHI WETU

KLINIKI ya soka ya Airtel Rising Stars inatarajia kuanza Jumatatu ijayo katika Uwanja wa Karume, huku wavulana 40 na wasichana 25 waliofanya vema kwenye michuano ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Stars 2016 wakishiriki.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Maendeleo ya Soka la Vijana wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Ayoub Nyenzi, kliniki hiyo kutakuwa na  hitimisho la michuano ya Airtel Rising Stars kwa  msimu wa sita.

Taarifa hiyo ilisema kliniki hiyo itakuwa ya siku sita na itaendeshwa na makocha wa timu ya soka ya taifa, Oscar Milambo, akisaidiwa na Kim Paulsen kwa wavulana huku wasichana wakifundishwa na kocha mkuu wa Kili Queens, Sebastian Nkoma.

Pia kliniki hiyo itatoa fursa kwa vijana kujifunza mbinu mpya za mpira na kupata mafunzo kutoka kwa makocha wazoefu ili kuongezewa vipaji vyao.

“Sisi TFF tumefanya maandalizi yote ya kliniki na tumeichukua kwa uzito wa hali ya juu kwa kuwa ndio njia sahihi ya kupata wachezaji wa timu zetu za taifa, Serengeti Boys na Taifa Queens.

Tunaamini ya kwamba kliniki haitakuwa na mafanikio kwa wachezaji tu bali na timu zetu kupata wachezaji walio bora. Tumekuwa tukishuhudia wachezaji wazuri wenye vipaji kwenye kila msimu wa Airtel Rising Stars.

Nachukua nafasi hii kuzishauri klabu zetu za mpira wa miguu kujitokeza kuangalia wachezaji wakati wa siku sita za kliniki hii ya Airtel Rising Stars,” ilisema.

Kwa upande wake, kocha mkuu wa timu ya Taifa ya vijana chini wa umri wa miaka 17, Milambo, alisema: ‘Wachezaji watafundishwa nidhamu ya mpira ndani na nje ya uwanja, jinsi ya kumiliki mpira mbele ya mchezaji wa timu pinzani, kutoa pasi za uhakika pamoja na mafunzo ya nadharia.”

Sambamba na hayo, wachezaji pia watakuwa na fursa ya kukutana na wenzao na hii itakuwa na hamasa kwao kwani wengi wao itakuwa mara ya kwanza kupata mafunzo kutoka kwa makocha.

Akizungumzia juu ya kliniki hiyo, Ofisa Uhusiano Airtel Tanzania, Jane Matinde, alisema michuano ya Airtel Rising Stars 2016 imekuwa na mafanikio makubwa.

Matinde alisema Airtel inajivunia kuwa sehemu ya mradi huu wa kukuza vipaji vya soka, kwani imesaidia kubadilisha soka la Tanzania.

Wachezaji zaidi ya 1000 wavulana na wasichana walishiriki kwenye michuano ya Airtel Rising Stars 2016 kutoka mikoa ya Mwanza, Morogoro, Mbeya, Arusha, Kinondoni, Ilala, Temeke, Lindi na Zanzibar.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -