Tuesday, October 27, 2020

MAANDALIZI YA KWENDA CAMEROON YAANZE

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

FAINALI zijazo za Kombe la Afrika (Afcon) zimepangwa kufanyika  mwaka 2019 nchini Cameroon, huku Tanzania ikiwa kwenye Kundi L pamoja na Uganda, Lesotho na Cape Verde.

Katika fainali zinazoendelea nchini Gabon, Tanzania ilishindwa kufuzu baada ya kufanya vibaya kwenye kundi lao G lililoundwa na Misri, Nigeria na Chad ambao baadaye walijitoa.

Tanzania ilianza vibaya kuwania kufuzu fainali zinazofanyika Gabon, baada ya kuchapwa mabao 3-0 katika mchezo wa kwanza na Misri waliofuzu kwenye kundi hilo.

Lakini waliendelea kufanya vibaya kwenye michuano ya Afrika ya Chan inayoshirikisha wachezaji wanaocheza Ligi ya Ndani ya nchi zao kwa kufungwa  mabao 3-0 na Uganda na baadaye kutolewa na Waganda hao kwa jumla ya mabao 4-1 kufuatia sare ya bao 1-1 waliyoipata ugenini.

Baadaye Tanzania ilishindwa kupata ushindi muhimu nyumbani katika mchezo wa Afcon, baada ya kutoka sare tasa na Nigeria na kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Chad.

Lakini Chad walishindwa kurudiana na Tanzania baada ya taifa hilo kujitoa, ambapo Watanzania walipoteza mchezo wa mwisho wa kundi lao kwa kufungwa na Nigeria.

Matumaini ya Tanzania kutofuzu katika fainali hizo za Gabon yalianza kuonekana mapema, baada ya kufanya vibaya kwenye michuano ya kimataifa ya Cosafa iliyokuwa moja ya sehemu ya  maandalizi ya Taifa Stars  kuelekea kwenye fainali za mwaka huu.

Katika michuano hiyo ambapo Tanzania ilishiriki kama mgeni mwalikwa iliyofanyika Mei mwaka juzi, Taifa Stars ilifungwa michezo yote kwenye kundi lao.

Tanzania ilianza kupoteza mwelekeo baada ya michuano ya Cosafa chini ya Kocha Mkuu Mart Nooij, lakini baadaye Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), lilikuja kujichanganya baada ya kutimua benchi nzima la timu hiyo.

Hilo lilikuwa ni kosa la kwanza lililofanywa na TFF la kutimua benchi la ufundi, huku michuano ya Afcon ikiwa imeanza, lakini maandalizi duni kwa Taifa Stars ilikuwa sababu kubwa.

Timu yetu iliingia kwenye michuano ya Afcon ikiwa haina maandalizi ya kutosha, haikucheza mechi nyingi za kimataifa kwa lengo la kuwajengea wachezaji wetu uzoefu zaidi ya ile michuano ya mwaliko ya Cosafa.

Sasa tunapolianza kundi jepesi la Tanzania kuelekea Afcon ya 2019 nchini Cameroon, tunaweza kuliangalia hivyo kwa macho, lakini bila kuwapo kwa maandalizi, hakika itakuwa ni vigumu kufuzu fainali hizo.

Kutokana na kiwango kilichoonyeshwa na timu ya Tanzania katika michuano ya kufuzu Afcon ya mwaka huu, bado kipo chini ya Uganda ambao kwa sasa wako Gabon kushiriki fainali hizo.

Cape Verde na Lesotho pamoja ni nchi ndogo zenyewe zimetengeneza mpira wao vizuri, hivyo Tanzania  ianze maandalizi mapema kama tunataka kwenda Cameroon.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -