Friday, December 4, 2020

Mabadiliko ya Ballon d’Or ni ‘kiama’ kwa Ronaldo, Messi?

Must Read

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

LONDON, England

BAADA ya miaka sita ya ushirikiano na Shirikiano la Soka ulimwenguni (FIFA), hatimaye Jarida la France Football la nchini Ufaransa limeamua kuichukua tuzo yake ya Ballon d’Or.

Itakumbukwa kuwa tuzo hiyo yenye heshima kubwa duniani imekuwa chini ya ufadhili wa FIFA tangu mwaka 2010, lakini sasa imerudi mikononi mwa jarida hilo.

Kabla ya ushirikiano na FIFA, jarida la French Football lilikuwa likitoa tuzo yake hiyo kwa mchezaji bora wa Ulaya.

Tarifa za French Football kutemana na FIFA zilianza kuvuma mwezi uliopita na baada ya hilo kutimia siku chache zilizopita, jarida hilo limefanya mabadiliko kwenye mfumo wa kumpata mshindi wa Ballon d’Or, tofauti na ule uliokuwa ukitumiwa na Shirikisho hilo.

Awali, katika mchakato wa kumpata mshindi wa Ballon d’Or, kura za makocha na manahodha wa timu za taifa zilikuwa zikitumika, lakini sasa hazina nafasi.

Kwa mujibu wa mabadiliko yaliyofanyika, ni kura za waandishi wa habari wa kimataifa pekee ndizo zitakazokuwa na nafasi katika mchakato wa kumsaka mwanasoka atakayetunukiwa tuzo hiyo iliyoanzishwa mwaka 1956.

Pia, jarida hilo limeweka wazi kuwa wachezaji watakaotangazwa kuingia kwenye kinyang’anyiro hicho cha kumsaka mchezaji bora wataongezeka kutoka 23 hadi 30.

Mbali na hilo, mabadiliko mengine ni yale yatakayohusisha tarehe ya kutangazwa kwa mshindi ambapo jarida hilo limedai kuwa hilo litafanyika kabla ya kufungwa kwa kalenda ya mwaka.

Lakini sasa, wachambuzi wengi wa soka wameibuka na hoja mpya wakidai kuwa huenda kitendo cha French Football kutoa nafasi kubwa kwa waandishi wa habari kikaumaliza utawala wa mastaa Cristiano Ronaldo na Lionel Messi, ambao wameonekana kuichukua mara nyingi tuzo hiyo katika miaka ya hivi karibuni.

Katika tuzo nane zilizopita, Messi, raia wa Argentina, amechukua tano, huku Ronaldo, ambaye ni nahodha wa timu ya Taifa ya Ureno akiiweka kabatini mara tatu.

Hoja ya wachambuzi ni kwamba huenda Messi asingeweza kuchukua tuzo hiyo ya Ballon d’Or mwaka 2010 kama mabadiliko haya yangekuwa yamefanyika.

Kwa mabadiliko ya sasa, wanaamini kuwa ilistahili kutua mikononi mwa Wesley Sneijder, ambaye alijikusanyia kura nyingi kutoka kwa waandishi wa habari.

Wakati Messi, anayetamba jijini Catalunyana klabu yake ya Barcelona alipotangazwa kuwa mshindi wa tuzo ya Ballon d’Or mwaka 2010, fundi huyo alishika nafasi ya nne katika orodha ya wachezaji waliopigiwa kura nyingi na waandishi wa habari.

Kwa upande wake, Sneijder, ambaye alinyakua taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya pamoja na kuifikisha Uholanzi fainali kwenye michuano ya kombe la dunia, alikuwa na alionekana kuwa na mvuto mkubwa kwa waandishi wa habari, hivyo ndiye aliyekuwa kinara wa kura zao.

Ni wazi kabisa kuwa, kama mshindi angechaguliwa kwa wingi wa kura za waandishi kama itakavyokuwa hivi sasa, basi mpachikaji mabao huyo hatari asingeweza kuibuka kidedea.

Ilikuwa hivyo pia mwaka 2013, wakati Ronaldo alipoichukua badala ya Mfaransa Frank Ribery ambaye alikuwa na kura nyingi kutoka kwenye vyombo vya habari.

Licha ya kuwa sehemu muhimu ya mafanikio ya Bayern, ikiwemo kunyakua mataji matatu na mabingwa hao wa Bundersliga, Ribery alishika nafasi ya tatu kwenye kinyang’anyiro cha kuifukuzia tuzo hiyo.

Winga huyo alikamata nafasi hiyo, licha ya kuongoza kwa kuwa na kura nyingi za waandishi, hivyo, kwa mabadiliko ya sasa, ni rahisi kusema kuwa alistahili tuzo hiyo ya Ballon d’Or kuliko Ronaldo.

Kwa takwimu hizo, ni wazi kabisa kuwa licha ya Ronaldo na Messi kuitawala tuzo hiyo yenye heshima kubwa kwenye ulimwengu wa soka, hawakuwa na sapoti kubwa kutoka kwa waandishi.

Je, nini hatima yao, ikizingatiwa kuwa sasa waandishi ndio wenye uamuzi wa mwisho juu ya nani atangazwe kuwa mshindi wa tuzo hiyo?

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul 'Ben Pol' ameshukuru mashabiki kwa...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -