Friday, October 30, 2020

Mabao 4 dhidi ya Celta Vigo? Kwani hawa Barcelona wana matatizo gani?

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

CATALUNYA, Hispania

INGAWA msimu uliopita Barcelona ilikutana na kichapo kikubwa zaidi ndani ya miaka tisa dhidi ya Celta Vigo kwenye dimba la Balaidos, lakini hakuna aliyefikiria kama wangekutana na kichapo dhidi ya timu ile ile msimu huu kulingana na kiwango cha vijana hao wa Catalunya.

Barca ilichapwa mabao 4-3 na Celra Vigo, ambapo waliruhusu mabao matatu ndani ya dakika 11.

Walikaribia kujiokoa na kichapo katika kipindi cha pili kabla ya mlinda mlango Marc-Andre ter Stegen kufanya masihara yaliyopelekea bao la ushindi lililomaliza mchezo huo.

Ule ubora wa Barca ndio unaondoka? Gazeti la The Sun limechambua yale yanayoonekana kuikumba timu hiyo iliyo chini ya kocha Luis Enrique.

Kikosi kipana chenye ubora mdogo

Miamba hao wa Catalunya kwa muda mrefu sasa wamekosa nguvu kwenye kikosi chao na kiukweli kwenye dirisha la usajili wa majira ya kiangazi walinyakua wachezaji wa kutosha ambao wanaifanya timu hiyo iwe na akiba nzuri ya wachezaji, bado kuna swali kama wanaosalia kwenye benchi wana ubora kama wale wanaoanza?

Samuel Umtiti angalau anaonesha uwezo kwenye nafasi ya ulinzi, lakini wachezaji kama Denis Suarez bado anapata tabu kuzoea soka la timu yake ya zamani na straika Paco Alcacer anaanza kufeli mapema.

Beki wa kushoto, Lucas Digne na kiungo Andre Gomes hawatakuwa machaguo ya kwanza labda kama kocha wao, Luis Enrique atakapoamua kuwaacha nje Andres Iniesta, Sergio Busquets na Jordi Alba.

Nguvu ya kutumia fedha kusajili imepungua

Kabla ya Paul Pogba kusaini mkataba wa kujiunga na Manchester United, ni Barca ambao walikuwa wakimhitaji wa kwanza na kama walimtaka wangeweza kufanya hivyo na hakuna ambaye angepingana na usajili huo.

Lakini walijikuta wakishindwa kutimiza haja yao kutokana na gharama ya mchezaji mwenyewe na wataendelea kushindwa zaidi.

Kiasi cha takribani pauni milioni 104 walichokitumia kwenye dirisha la usajili wa majira ya kiangazi kilikuwa ni kwa ajili ya kutanua kikosi tu.

Iko wazi kwamba baada ya kuachana na mpango wa kumsajili Pogba, rais wa klabu hiyo, Josep Maria Bartomeu ameifanya Barca ionekane wazi kuwa haitakuwa na nguvu ya kufanya usajili mkubwa kama ule wa Neymar au Suarez kwa siku za usoni.

Haitaweza kushindana na miamba kama  Man City iliyotumia pauni milioni 177, Man Utd (157) na Chelsea (108).

Sababu ya wapinzani wao Real Madrid kutumia pauni milioni 25 tu kusajili msimu huu, ni kocha mkuu Zinedine Zidane kuweka wazi kuridhika kwake na kikosi alichonacho.

Mabadiliko ya kikosi kila mara

Ile Barcelona iliyokuwa ikitesa kati ya mwaka 2008 na 2012 ilikuwa na kikosi cha kwanza ambacho ni mara chache kukiona kikiwa kimebadilishwa baina ya mechi na mechi.

Xavi alikuwa kwenye ubora wake, Messi kwenye  nyakati zake za kunyakua Ballon d’Or atakavyo.

Hivi sasa Enrique ana uwezo wa kufikiria kubadilisha wachezaji hadi saba wa kikosi cha kwanza kwenye mchezo ujao na matokeo yake ndio hayo, ushindi wa nadra au kichapo.

Alaves waliitumia vema fursa hiyo pale Camp Nou na Celta Vigo wakafanya hivyo wikiendi iliyopita, ingawa hakukuwa na mabadiliko makubwa kwenye mchezo huo wa pili.

Kama timu iko vizuri, ya nini kuibadilisha?

Ile falsafa ya Cruyff imepotea

“Kucheza soka ni rahisi sana lakini kucheza soka jepesi ni jambo gumu.”

Moja ya kauli maarufu za gwiji la Barca, Johan Cruyff na ni kauli inayoelezewa na soka linalochezwa ndani ya Barca.

Klabu hiyo imeugeuza mchezo wa soka kama sanaa. Si kitu kingine chochote.

Zile pasi zao fupi na za haraka haraka ambazo zimewafanya wang’are kwenye zama za dhahabu, zimeanza kupotea kadiri wanavyoendelea.

Huko aliko Mdachi, Cruyff, lazima atakuwa na hasira tu.

Messi…

Kwa kipindi chote ambacho Muargentina huyu amekuwa akicheza ndani ya jezi ya Barca, timu hiyo imekuwa ikimwangalia kama injini inayosaidia gari lipande milima, kuvuka mito na mabonde makubwa.

Lakini hivi sasa injini hii inaamua kushuka zaidi chini kwa ajili ya kuanzisha mashambulizi ya timu.

Ule uwezo wake unaanza kuchujwa anapocheza kama kiungo wa kati, watu wanaanza kumkaba kuanzia eneo hilo.

Anakuwa na nafasi finyu ya kuiendesha timu kwa kasi ile ile aliyokuwa nayo hapo kabla na wakati huo huo wenzake huamua kurudi chini kumfuata na kumpa msaada, hapo mashambulizi mengi huchelewa kufika mbele kwa wakati.

Hapo ndipo Barca inapoanza kuhaha, isijue nini kingine wanachoweza kufanya na wakati unazidi kuwaacha.

Je, tunaelekea kuishuhudia Barcelona ya mwisho?

 

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -