Wednesday, October 28, 2020

Mabao la dakika za majeruhi

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

LONDON, England

HAKUNA kitu cha kufurahisha kama kufunga bao muhimu dakika za majeruhi kwenye mechi. Kocha, mchezaji na shabiki kutamfanya awe na imani kwamba mechi haijaisha mpaka kipyenga cha mwisho.

Mwishoni mwa wiki iliyopita katika mechi kati ya Burnley na Arsenal, tuliona nahodha wa Gunners, Laurent Koscielny, akifunga bao ambalo lilikuwa na utata baada ya mpira kumpiga mkononi dakika za majeruhi za mchezo huo na kushinda 1-0 na Burnley kurejea nyumbani bila pointi.

Bahati hiyo ya Arsenal, imeufanya mtandao wa HITC kuangalia mabao matano ya ushindi ya Ligi Kuu England, ambao yamefungwa dakika za majeruhi.

  1. Liverpool – 28

Kama kuna timu ya kuogopa wakati mchezo unaelekea kumalizika ni Liverpool. Kikosi hicho cha Jurgen Klopp kinaongoza kwenye orodha hiyo, ambapo kimefunga mabao 28 ya ushindi dakika za majeruhi katika mechi zao.

  1. Arsenal – 24

Halikuwa jambo la kushangaza kuona wiki iliyopita Arsenal kufunga bao la ushindi dakika za majeruhi. Gunners wako nyuma ya Liverpool kwa mabao manne. Moja ya mabao ambayo yatabaki kwenye kumbukumbu ya mashabiki wa soka ni lile la Danny Welbeck, ambaye alifunga bao dakika ya 95 dhidi ya mabingwa wa Ligi Kuu England, Leicester, Februari mwaka huu.

  1. Chelsea – 20

Timu nyingine tishio za kuangalia ni Chelsea. Kikosi hicho cha Antonio Conte kimefunga jumla ya mabao 20 katika historia ya klabu hiyo katika mechi za Ligi Kuu England.

  1. Everton – 19

Mahasimu wa Liverpool kutoka Merseyside, Everton wanashika nafasi ya nne wakiwa na jumla ya mabao 19 waliyofunga dakika za majeruhi. Everton ndiyo timu ambayo inaweza kukuharibia sherehe dakika za majeruhi.

  1. Man United – 18

Manchester United wanashika nafasi ya tano wakiwa na mabao 18 ya ushindi waliyofunga dakika za majeruhi. Kwa msimu huu moja ya mabao ya dakika za majeruhi alifunga chipukizi wa klabu hiyo ya Old Trafford, Marcus Rashford, dhidi ya Hull City.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -