Monday, October 26, 2020

MABEKI WA KULIA WALIOVUMA NCHINI (4)

Must Read

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian...

NA HENRY PAUL

Wiki iliyopita BINGWA Jumatatu lilikukumbusha baadhi ya mabeki mahiri wa kulia waliokuwa na uwezo mkubwa wa kucheza safu hiyo, ambao walitamba hapa nchini wakicheza Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara (sasa Ligi Kuu), pamoja na wengine hata kuchezea timu ya taifa, Taifa Stars.

Ufuatao ni mwendelezo wa baadhi ya wachezaji hao ambao wanakumbukwa hadi leo hii na wapenzi wa soka nchini kwa kuwa na uwezo mkubwa wa kucheza safu hiyo na kuwafanya mawinga wa kushoto waliokuwa wanakabiliana nao kupata wakati mgumu kuwapita.

7.DAUDI SALUM ‘BRUCE LEE

Unapozungumzia mabeki waliokuwa na uwezo mkubwa wa kumudu kucheza vyema safu ya beki wa kulia, kamwe huwezi kuacha kulitaja jina la mlinzi shupavu, Daudi Salum maarufu ‘Bruce Lee’, kwani nyota huyu alikuwa mahiri mno katika nafasi hii hususan alipokuwa akichezea timu ya Simba inayojulikana kwa jina la ‘Wekundu wa Msimbazi’.

Nyota huyu pamoja na kuwa makini mno katika kuwadhibiti mawinga wasumbufu wa kushoto, pia alikuwa mahiri mno katika kupanda mbele kuongeza mashambulizi, huku akipiga krosi muruwa kwa washambuliaji wa kati.

Pia mkongwe huyu alisifika kwa aina ya uchezaji wake, kwani alikuwa anawadhibiti mawinga wa kushoto kwa kuwakata mapanga ‘nyombo’, huku akiruka juu mithili ya mwigizaji wa sinema za Kichina, hali iliyowafanya wapenzi wa soka hususan wa klabu ya Simba kumbatiza jina na marehemu Bruce Lee ambaye alikuwa anacheza na kuigiza sinema za ‘kung fu’ za Kichina.

Salum alijiunga na klabu ya Simba msimu wa 1978/1979 na kuwa mmoja wa wachezaji wa kutumainiwa wa timu hiyo, akichukua nafasi ya beki mahiri Shabani Baraza ambaye alikuwa akicheza nafasi ya beki wa kulia aliyekuwa ameanza kuchoka.

Mkongwe huyo baada ya kujiunga na Simba baadhi ya wachezaji aliowakuta na kuwa nao, ni kipa Athumani Mambosasa (marehemu), Omari Mahadhi ‘Bin Jabir’ (marehemu), Abdallah ‘King’ Kibadeni, Omari Gumbo, Ezekiel Greyson ‘Jujuman’ (marehemu), Amri Ibrahim na Mohamed Bakari ‘Tall’.

Wengine ni Nico Njohole, Jumanne Masmenti (marehemu), Adam Sabu (marehemu), Martin Kikwa, Thuwen Ally, Abbas Dilunga, Willy Mwaijibe, Abbas Kuka, George Kulagwa na Rahim Lumelezi.

Mkongwe huyo kutokana na umahiri mkubwa aliokuwa akiuonesha akiwa na timu ya Simba msimu wa 1979/1980, alichaguliwa kuchezea kikosi cha timu ya taifa, Taifa Stars na alikuwa ni mmoja wa wachezaji waliokuwa katika kikosi hicho kilichoshiriki fainali za Mataifa Afrika zilizofanyika mjini Lagos, Nigeria mwaka 1980.

Miongoni mwa wachezaji aliokuwa nao katika kikosi hicho ni Juma Pondamali ‘Mensah’, Athumani Mambosasa (marehemu), Mohamed Kajole ‘Machela’ (marehemu), Shaban Ramadhani, Salim Amir, Juma Mkambi ‘General’ (marehemu), Omari Hussein ‘Keegan’, Hussein Ngulungu na Peter Tino.

Wengine ni Mohamed Salim, Thuwen Ally, Ahmed Amasha ‘Mathematicians’, Leodger Tenga, Jella Mtagwa, Mohamed Rishard ‘Adolph’, Rashid Iddi ‘Chama’, Mtemi Ramadhani, Charles Alberto na Willy Kiango (marehemu).

8.JUMA SHABAAN ‘UNCLE J

Shabaan ni miongoni mwa wachezaji waliokuwa na uwezo mkubwa wa kucheza safu ya beki wa kulia, kwani mchezaji huyu mbali na kuwa kikwazo kwa mawinga wasumbufu, pia alikuwa na uwezo mkubwa wa kupanda mbele na kupiga krosi.

Mkongwe huyu ambaye ana umbo la kawaida, alianza kujulikana katika ulimwengu wa soka msimu wa 1974/1975 alipojiunga na klabu ya Yanga akitokea Mkoa wa Morogoro. Baada ya kujiunga na timu hiyo akawa ni mmoja wa wachezaji wa kutumainiwa chini ya kocha mkuu, Tambwe Leya ambaye hivi sasa ni marehemu.

Nyota huyo baada ya kujiunga na Yanga, alikuwa ni mmoja wa wachezaji walioiwezesha timu hiyo kutwaa taji la Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, baada ya kuifunga Simba mabao 2-0, yaliyofungwa na Gibson Sembuli na Sunday Manara.

Mwaka 1976 baada ya kutokea mgogoro mkubwa ulioikumba klabu ya Yanga, Juma Shabaan alikuwa ni miongoni mwa wachezaji waandamizi waliojiengua katika timu hiyo na kwenda kujiunga Nyota Afrika ya Morogoro.

Nyota huyo miongoni mwa wachezaji aliokuwa nao katika timu hiyo ya Nyota Afrika ni Patrick Nyaga, Kitwana Manara, Sunday Manara, Omari Kapera ‘Mwamba’ (marehemu), Gibson Sembuli (marehemu), Juma Matokeo (marehemu), Leodger Tenga, Jella Mtagwa, Muhaji Mukki (marehemu), Boi Wickens (marehemu) na Ali Yusuf.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya kuwa na umri wa miaka...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian Mbappe na Neymar, kwenye mechi...

IBRA:Kifaa kipya Konde Gang aliyetembea kwa mguu kumwinda Harmonize

NA BRIGHITER MASAKI UKITAJA vijana wanaofanya vizuri katika mziki wa bongo fleva, huwezi kukosa kumtaja msanii chipukizi anayefahamika zaidi...

Jay-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas

-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas New York, Marekani HAKUNA shabiki wa Hip hop asiyelifahamu...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -