Wednesday, October 21, 2020

MABENCHI YA MIAMBA HAWA YANA NGUVU KIASI GANI?

Must Read

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu...

LONDON, England

LIGI Kuu England inaelekea kwenye kipindi cha sikukuu na kama kawaida suala la uchovu na majeruhi kwa wachezaji huanza kuziadhibu zile timu ambazo zina vikosi dhaifu vya kupambana kwenye ligi hiyo.

Mtandao wa SkySport umechambua uzito wa aina ya wachezaji wanaokaa benchi katika timu zilizo kwenye mbio za kuwania ubingwa kati ya Chelsea, Arsenal, Liverpool, Man City, Tottenham na Man United; ni ipi yenye wachezaji wa nguvu na ipi itapata shida ya kuhimili presha kwa kukosa nguvu ya kutosha kwenye benchi lake la ufundi?

Walichofanya ni kuondoa wachezaji wenye nafasi kubwa kwenye vikosi vya kwanza na kuhesabu idadi ya mechi walizocheza kwenye Ligi kuu England, mechi za kimataifa na gharama za usajili zilizotumika kuwasajili wachezaji hao wanaoachwa benchi ambapo walipata wastani wa wachezaji wenye uwezo wa kutumika kama wachezaji wa ‘sub’.

Ni habari mbaya kwa Tottenham, kwani kwa mujibu wa uchambuzi wa SkySport, timu hiyo ina benchi dhaifu lenye wastani wa wachezaji waliocheza mechi 37 tu za ligi, mechi saba za kimataifa, huku wakiwa na thamani ya jumla ya pauni milioni 5.4.

Kati ya wachezaji hao saba, wapo makinda kutoka akademi yao, Harry Winks, Josh Onomah na Cameron Carter-Vickers na walikuwepo kwenye benchi dhidi ya Swansea.

Chelsea wao wana benchi lenye nguvu kuliko timu zote hizo zilizo kwenye mbio za ubingwa ambapo wachezaji wanaotokea benchi ndani ya klabu hiyo wamecheza jumla ya mechi 109 za ligi kuu, 29 za kimataifa na thamani yao ni pauni milioni 12.2.

Straika Michy Batshuayi ameigharimu timu hiyo kiasi cha pauni milioni 33.2, lakini amejumuishwa kwenye benchi katika mechi zote msimu huu, huku Oscar na Cesc Fabregas wakitokea benchi mara nane, Branislav Ivanovic (sita), John Terry (tano) na Willian (nne).

United wao wanakamata nafasi ya pili kwa kuwa na benchi lenye wachezaji imara kwa mujibu wa utafiti wa SkySport, ambapo wastani wa wachezaji wao walio benchi wamecheza jumla ya mechi 92 za ligi kuu, 26 za kimataifa, huku wakiwa na thamani ya pauni milioni 10.8.

Kati ya timu nyingine nne zilizobakia, Arsenal wana wachezaji waliocheza jumla ya mechi 23 za kimataifa, City wana wachezaji wenye idadi kubwa ya mechi za ligi (92) na thamani ya pauni milioni 7.9, lakini mechi za kimataifa walizocheza ni chache, mechi 16 tu.

Wakati huo huo, wastani wa wachezaji walio kwenye benchi la Liverpool wamecheza mechi 69 za ligi, 20 za kimataifa wakiwa na jumla ya thamani ya pauni milioni 6.2.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya wanamuziki wa Tanzania ambao miongoni...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara  (VPL), utakaochezwa leo...

Mugalu atema cheche Simba

NA ASHA KIGUNDULA MSHAMBULIAJI wa Simba, Chris Mugalu, amesema wanakwenda mkoani Rukwa kupambana na kupata ushindi katika mchezo wao...

Malale aitisha Yanga

NA ZAINAB IDDY KOCHA Mkuu wa timu ya Polisi Tanzania, Malale Hamsini, amezisikia sifa za kocha mpya wa Yanga,...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -