Thursday, October 29, 2020

Wengi wajitokeza kumzika Mashali

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

NA ZAITUNI KIBWANA

MAMIA ya mashabiki wa masumbwi  jana walijitokeza kumzika bondia Thomas Mashali, kwenye Makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Mashali alifariki alfajiri Jumatatu wiki hii, baada ya kupigwa na watu wasiojulikana waliodhani ni mwizi huko Kimara Bonyokwa katika wilaya mpya ya Ubungo.

Shughuli za maziko zilianza saa tano asubuhi katika viwanja vya Leaders Club na kuhudhuriwa na wadau wengi wa ngumi, akiwamo Francis Cheka, Abdallah Pazi ‘Dulla’, Katibu wa Shirikisho la Ngumi nchini (PST), Antony Rutta na Seleman Kidunda.

Wengine ni promota wa ngumi za kulipwa, Siraju Kaike, Cosmas Cheka, Ibrahim Class, Francis Miyeyusho, Mfaume Mfaume, Rashid Matumla, Yasin Abdallah ‘Ustadh’ na Kaimu Mkurugenzi wa zamani wa Idara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na michezo, Juliana Yasoda.

Akisoma wasifu kaka wa marehemu, Zunda Ndalanga, alisema mdogo wake atakumbukwa kwa mengi kutokana na mchango wake mkubwa kwenye familia yao.

“Yapo mengi ila nina imani kila mtu anayajua mazuri ya Mashali, hivyo tunawashukuru wote ambao wamejitokeza kumpumzisha kwenye nyumba yake ya milele,” alisema.

Mwenyekiti wa kamati ya mazishi, Modest Rashid, aliwaasa vijana waliojitokeza kumzika marehemu kutofanya vitendo vyovyote vya uvunjwaji wa amani.

“Tunawaomba jamani kila aliyekuja hapa aondoke kwa amani, kuna watu wa aina mbalimbali tusije tukasikia vitendo vya uvunjifu wa amani.

“Wengi wanasema ngumi ni uhuni,  wizi, leo tunaomba kila aliyekuja hapa afike nyumbani kwake kwa usalama, siku hii iwe nzuri kwa Mashali na si ya kumpa sifa mbaya,” alisema Rashid.

Kwa upande wake bondia Dulla Mbabe, alisema wamepata pengo kubwa kuondokewa na mwana masumbwi mwenzao.

Kabla ya mauti kumfika, Mashali alikuwa amepigana mapambano 26 akishinda 19, kupigwa matano na kutoka sare moja.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -