Friday, September 25, 2020

Mabosi Arsenal wapoteza imani kwa Ljungberg

Must Read

Azam FC yakiri Mbeya City kiboko

NA WINFRIDA MTOI LICHA ya kuchukua alama tatu kwa Mbeya City, uongozi wa Azam...

Niyonzima ala kiapo mechi za ugenini

NA ZAINAB IDDY NAHODHA msaidizi wa Yanga, Haruna Niyonzima, amesema kuwa mipango ya timu...

Yanga achana nao

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga umekuja na mkakati maalum wa kuhakikisha wanakusanya pointi...

LONDON, England

MAMBO yameendelea kuwa magumu ndani ya klabu ya Arsenal na safari hii bodi ya klabu hiyo wameitisha kikao kwa ajili ya kujadili hatima ya kocha wa muda, Freddie Ljungberg, aliyechukua nafasi ya Unai Emery.

Kamati nzima ya klabu hiyo ilijadili endapo mkongwe huyo ataendelea kubaki au kumtema baada ya kuiongoza Arsenal michezo mwili ya Ligi Kuu England pasipo kupata ushindi.

Katika mchezo wa kwanza dhidi ya Norwich iliyochezwa Carrow Road, Arsenal ililazimishwa sare ya mabao 2-2 kabla ya kupoteza kwa Brighton mabao 2-1 wakiwa nyumbani.

Ni wazi mabosi hao wamekosa imani naye na wataangalia uwezekano wa kutafuta njia mbadala, ikiwamo kuingia sokoni na kutafuta kocha wa kudumu atakayeinoa Arsenal.

Hadi sasa makocha kadhaa wametajwa ambao wamependekezwa na bodi hiyo akiwamo Mikel Arteta, Rafa Benitez, Maxi Allegri, Patrick Vieira, Mauricio Pochettino na Brendan Rodgers licha ya wiki iliyopita kuongeza mkataba wa miaka mitano kuinoa Leicester City.

Baada ya Arsenal kufungwa na Brighton, Ljungberg alisema kwasasa wachezaji wake wamejawa na hofu ya kutojiamini na watachukua muda kurudi mchezoni.

Wakati mabodi wa Arsenal wakiwaza hatima ya Ljungberg, Arsenal itashuka leo dimbani kumenyana na West Ham kwenye mechi ya Ligi Kuu England.

Arsenal ambao haijapata ushindi wowote katika mechi nne mfululizo walizocheza za ligi, wanashika nafasi ya 11 kwenye msimamo wa ligi wakiwa na pointi 19 kabla ya mechi za jana.

West Ham licha ya kufungwa na Wolves mabao 2-0 mchezo uliopita, watawavaa Arsenal wakiwa na kumbukumbu nzuri ya kuwafunga Chelsea bao 1-0.

Katika mchezo wa Ligi Kuu England uliochezwa jana, Leicester City walijiimarisha nafasi ya pili kwenye msimamo baada ya kuwafunga Aston Villa mabao 4-1.

Leicester City walianza walianza kupata bao dakika ya 20 lililofungwa na Jamie Vardy kufuatia pasi ya Kelechi Iheanacho na Iheanacho akatupia bao la pili dakika ya 41 akimalizia pasi ya James Maddison.

Aston Villa wakicheza nyumbani walipata bao dakika za mwisho kipindi cha kwanza kupitia kwa nyota wao Jack Grealish lakini Johny Evans akaipa Leicester City bao la tatu dakika ya 49 kufuatia kazi nzuri ya Maddison kabla ya Vardy dakika ya 75 kuhitimisha ushindi mnono wa Leicester City.

Nayo Newcastle walitoka nyuma licha ya Danny Ings kuwapa Southampton bao la kuongoza na kuibuka na ushindi wa 2-1 kupitia mabao ya Jonjo Shelvey na Federico Fernandez.

Kwenye Uwanja wa Carrow Road, Norwich City walitangulia kupata bao dakika ya 27 kupitia kwa Alexander Tettey lakini mabao ya Enda Stevens dakika ya 49 na George Baldock dakika ya 52 yalitosha kuipa Sheffield United ushindi.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Azam FC yakiri Mbeya City kiboko

NA WINFRIDA MTOI LICHA ya kuchukua alama tatu kwa Mbeya City, uongozi wa Azam...

Niyonzima ala kiapo mechi za ugenini

NA ZAINAB IDDY NAHODHA msaidizi wa Yanga, Haruna Niyonzima, amesema kuwa mipango ya timu yao ni kuwa na mwendelezo...

Yanga achana nao

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga umekuja na mkakati maalum wa kuhakikisha wanakusanya pointi tatu kila mchezo, wakianzia mechi...

CHAMA GUMZO KILA KONA

NA WINFRIDA MTOI KIWANGO kilichoonyeshwa na kiungo wa Simba, Clatous Chama katika mchezo wa juzi wa Ligi Kuu Tanzania...

United ‘kimeo’ yamtoa povu Evra

MANCHESTER, EnglandBEKI wa zamani wa Manchester United, Patrice Evra, amekerwa na namna mambo yanayoendelea katika klabu hiyo, hasa ishu za usajili.
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -