Friday, November 27, 2020

MADANSA TU NDIO AMBAO HAWANA VIONGOZI WENYE DIRA NA MIPANGO ENDELEVU

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

HABARI za mwanzo wa wiki wasomaji wangu ni matumaini yangu hali ni salama kabisa kwa upande wenu. Kwangu namshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema kwa kunijaalia afya njema.

Tuko pamoja katika harakati za kuendeleza gurudumu la sanaa, mada za hapa kwa namna moja au nyingine zimekuwa msingi wa uchokozi wa mjadala mpana zaidi katika kujadili masuala ya maendeleo kwenye fani ya kudansi hapa nchini.

Leo pamoja na mambo mengine mada yangu itajikita kuzungumzia uongozi wa wasanii wa kudansi. Nianze kwa kuuliza je, wasanii wa kudansi wana viongozi wao wanaowatetea kwenye maslahi yao?  Kama wapo ni akina nani na matokeo yake baada ya kuwatetea au kuwasemea matatizo yao ya kila siku wanayokumbana nayo kwenye kazi yao ni yapi.

Vipo vyama viwili ninavyovitambua, kwanza kulikuwa na TDMA, hiki kilikuwa chama kikongwe ambacho kiliasisiwa na mtu mmoja aliyependa sana madansa, si mwingine ni Shabaan Sato. Hakuwa pekee yake kulikuwa na watu wengine nyuma yake, baadaye wakaja Malifeza, Hashimu Lundenga, Charles Maumba, mpaka chama kilipoangukia kwa mmiliki wa Ruaha Cross, John Ngogo.

Baada ya hapo chama hiki kinapata taabu kweli kuungwa mkono japo baadhi ya wanachama wa zamani bado wapo. Kwa maana halisi hiki chama kipo kama hakipo, kinasuasua. Baadaye kikaalikwa chama kingine cha kuwatetea na kuwasemea madansa, kinaitwa TDA. Hiki chama kiliasisiwa na dansa mmoja maarufu kwa kipindi cha zamani aliyeitwa Chino Loketo.

Chino alikuwa akishirikiana na baadhi ya madansa wengine, japo chama hiki kilikusudia madansa waliokuwa wakicheza kwenye bendi tu hivyo madansa wengine wanaocheza kwenye club na maeneo mengine hawakukiunga mkono baadaye madansa wengine tuliruhusiwa kujiunga na vyeo tulipewa, baada ya hapo sijui kilitokea nini chama sijakisikia tena.

Hivi vyama viwili viliwahi kusema kama ni vitetezi wa madansa na madansa waliviamini sana, lakini kuna nguvu inahitajika ambayo inaweza kivinusuru hivi vyama au kujengwa chama kingine kitakachokuwa na nguvu, mwonekano mpya na wa kisasa kwa maana vijana wa sasa wanahitaji speed na pesa, hakuna longolongo, dansa wanahitaji mikakati ya kisayansi na nguvu ya ushawishi (influence).

Madansa wamekata tamaa kwa kule kukosa sehemu ya kutoa malalamiko yao na pale anapokosa au kucheleweshewa maslahi yake, vyama vyote viwili vimeshindwa kumlinda na kumwelimisha dansa ili aweze kutumia kipaji chake vizuri kwa manufaa ya familia yake na taifa kwa ujumla.

Ukikaa na madansa ukaongea nao utagundua wanajua baadhi ya mambo kuhusu sanaa yao, lakini nani atayapeleka mbele mawazo yao? Hilo ndilo linalowakwamisha, wanahitaji mtu mwenye uthubutu wa kuwasemea kwamba kunengua pia ni kazi kama zingine itambulike kijamii na kitaaluma, tena kwa maana halisi ya kutambuliwa.

Wasanii wa kudansi wengi wao wanajiongoza wenyewe, hawana mwalimu wala mkufunzi, pia hawana mamaneja wa kuwasimamia. Na jambo lingine ni kuwa wengi wao wanatoka kwenye familia maskini sana, hivyo si rahisi kuwa na elimu kubwa na bora, tukiacha kipaji chake hana cha kujivunia.

Kuwapo na chama na uongozi imara wa madansa kutasaidia katika kusimama maslahi ya wasanii wa kundi hili ikiwa ni pamoja na kusaidia kutafuta vyanzo vya fedha ili kuinua hali ya wasanii katika nyanja mbalimbali ikiwamo mafunzo mbalimbali.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -