Tuesday, November 24, 2020

MADJ WAMESHAANZA KUKUTANA, MADANSA WATAKUTANA LINI?

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

WIKI iliyopita katika ukurasa huu nilizungumzia juu ya kuwepo kwa chama cha madansa kilicho hai chenye viongozi imara na makini, kwa jaili ya kushughulikia masuala mbalimbali ya madansa. Wito wangu ule badala ya kuitikiwa na madansa niliowakusudia, wadau wengine wa burudani kundi la wachezeshaji wa muziki, madj, wao walikuwa kwenye akili yangu kabisa.

Baada ya makala ile Ijumaa iliyopita pale  Ascape One, Madj wa zamani walikutana na wadau wakubwa kabisa wa disco wa kipindi kileee cha akina Nigga J, Kalikali, Peter Pantalakis, dj Luis, Pop Juice, Saydou, Ebony Moalim na wengine wengi siwezi kuwataja wote humu.

Niwape hongera zao kaka zangu wale kwa kukutana na kufanya utambuzi kwa wadau wote waliofika pale japo mimi mwandishi wa makala haya sikupata nafasi ya kuhudhuria. Lakini kwa kutumia mitandao yetu nimepata habari kwamba mambo yalikwenda vizuri kabisa.

Sasa hapa nataka niliangalie hili kama changamoto kwa madansa, kwamba Madj ambao tulikuwa tunashirikiana nao leo wao wanakutana, je, madj watuvute kwao au sisi tujifunze kitu kutoka kwao. Je, dunia ya leo watu watakukumbuka vipi kama hujulikani unapatikana wapi au hamjitokezi kama kikundi?

Madj wameona umuhimu wa kukutana na kukaa pamoja kupanga mikakati na pengine kuanzisha umoja wao utakaowasaidia kwenye masuala mbalimbali. Vijana wa sasa wanasema Madj wamekutana ili kuyajenga mambo yao.

Lakini hii sasa iwe chachu kwa madansa wa sasa na wa zamani kukutana na kutengeneza umoja usio rasmi, kwanza ambao utakaolazimisha kuurasimisha ili wadau wengine wautambue ili madansa wanapokwenda sehemu, kila mtu awatambue kupitia umoja huo.

Hili haliwezi kufanyika bila kubadilisha mitazamo yetu, kwa namna tunavyoyaangalia maisha na mabadiliko yake. Itakuwaje kama leo madj wanajitambulisha halafu kwa wakati huo wanawatumbulisha na mdansa wa  wakati huo wa zamani na pengine wakatoa na burudani kidogo kuwakumbusha watu  jinsi mambo yalivyokuwa kipindi hicho.

Ndipo ninapotaka madansa wa zamani waanze na wao kukutana kujenga umoja wao ili kujenga taswira mpya ya tasnia ya kudansi kuzaliwa upya. Hakuna wa kufanya haya ila wale tu waliobeba hii tasnia ya kudansi tangu miaka ya 1980, 1990 ambao mpaka sasa wapo na niliwahi kuwataja kwenye makala zangu zilizopita.

Hatujachelewa bado, viwanja vya kukutana vipo na wadau wa kusapoti wapo ni madansa tu kuamua. Nilisema hapo nyuma kwamba watu wanataka kuwaona watu wao wa burudani wa huko nyuma lakini watawaona vipi hapo ndio kwenye tatizo kwa kuwa madansa wengi wamejificha wakifikiri labda wamepitwa na wakati, si kweli kwa sababu wadau wa mambo ya zamani wapo na wanaulizia vipi wanaweza kuwaona tena madansa wa zamani kwa burudani yao.

Mfano kwa sasa zipo bendi nyingi lakini kuna watu wanataka kumsikiliza King Kikii tu, madisco yapo mengi lakini wadau wa disco la zamani wapo na wanakwenda kusikiliza vitu vya zamani kama kawaida. Shime ndugu madansa tukutane ili tujenge na wadau wataona tunachotaka kufanya. Ni muhimu sana kuanza kukutana kupanga mikakati yetu ambayo kwa namna moja au nyingine itakuwa njia ya kusonga mbele kwa fani ya dansi Tanzania.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -