Friday, November 27, 2020

MADRID, BARCA HAKIJAELEWEKA UBINGWA LA LIGA

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

CATALUNYA, Hispania


BADO ni ngumu kutabiri litakapoelekea taji la La Liga msimu huu hasa baada ya matokeo ya mechi za wikiendi hii.

Matumaini ya Barcelona kuchukua ubingwa huo yaliingia mdudu kwa kichapo cha mabao 2-0 walichopokea juzi kutoka kwa Malaga.

Kama wangeshinda mechi hiyo, basi wangekuwa wamewafikia mahasimu wao Real Madrid ambao wamejichimbia kileleni wakiwa na pointi 72.

“Tulitawala na makosa yetu ndiyo yaliyotugharimu, tulitengeneza nafasi, lakini hatukuwa na bahati. Tungeweza kushinda kwa juhudi za Luis Suarez katika kipindi cha kwanza lakini hatukupewa penalti ya Sergi Roberto,” alisema kocha Luis Enrique.

Kwa upande wao, Madrid walishindwa kuwakimbia zaidi wapinzani wao hao wanashika nafasi ya pili kwa pointi 69,  baada ya kuambulia sare ya bao 1-1 dhidi ya Atletico Madrid.

Kwa maana hiyo basi, sasa Madrid wamebaki kileleni mwa ligi hiyo kwa tofauti ya pointi tatu pekee, matokeo yaliyoibua matumaini kwa Barca kuwa wanaweza kupambana na kuwang’oa kileleni.

Katika mchezo huo ambao Barca walikuwa ugenini kwenye Uwanja wa La Rosaleda wenye uwezo wa kupokea mashabiki 30,044, mabao ya Malaga yaliwekwa kimiani na mastaa wake, Sandro na Jony.

Matokeo hayo yamewawezesha Malaga kuchomoka kwenye hatari ya kushuka daraja na ulikuwa ni ushindi wake wa pili mfululizo baada ya ule walioupata kutoka kwa Sporting Gijon.

Barca walilazimika kucheza wakiwa pungufu kwa dakika 30 za mwisho wa mtanange huo baada ya nyota wao, Neymar, kulimwa kadi nyekundu.

Hiyo ilikuwa ni kadi ya kwanza kwa Mbrazil huyo katika michezo 181 ambayo ameshaicheza tangu alipotua Barca.

Kipigo hicho kimewapunguza kasi Barca kwani sasa watabaki kwenye nafasi yao ya pili wakiwa na pointi 69, huku wakitambua wazi kuwa wapinzani wao hao wana ‘kiporo’ cha mchezo mmoja.

Hata hivyo, Barca hawakuonekana kuwa kwenye ubora wao walipokuwa wakivaana na Malaga. Tangu kuanza kwa msimu huu, kile ndicho kilichokuwa kiwango kibovu zaidi.

Kocha Luis Enrique aliingia na mfumo wa 4-3-3, lakini hakuwa na kikosi cha kwanza kilichozoeleka na ambacho kimekuwa kikimpa matokeo mazuri.

Alilazimika kuwatumia Mathieu, Andre Gomes na Denis Suarez ili kuchukua nafasi za Gerard Pique na Ivan Rakitic. Lakini pia, alimpumzisha Andres Iniesta.

Alimtumia Javier Mascherano kama beki wa kulia kutokana na kukosekana kwa Sergi Roberto ambaye amekuwa akifanya vizuri katika eneo hilo.

Pongezi kwa kocha wa Malaga, Diego Michel ambaye mbinu yake ya kutumia mabeki watano ilionekana kuyamaliza kabisa makali ya washambuliaji wa Barca.

Lakini pia, mpango wake wa kuwatumia viungo watatu ulionekana kuzaa matunda.

Aprili 15, mwaka huu, Barca watakuwa na mtihani wa kurejesha matumaini yao ya ubingwa kwa kuvaana na Real Sociedad na wataingia uwanjani bila huduma ya staa Neymar.

Pia, baada ya kuvaana na Sociedad, Barca watakuwa na kibarua kigumu cha kutafuta pointi tatu katika mchezo wa Aprili 28, dhidi ya Madrid utakaopigwa Santiago Bernabeu.

Juzi Madrid wakiwa mbele ya mashabiki wao 81,044 kwenye Uwanja wa Bernabeu, walitoa sare ya bao 1-1 na mahasimu wao wakubwa Atletico.

Bao la kichwa la kipindi cha pili lililofungwa na beki kisiki, Pepe, lilionekana kuwapa ushindi vijana hao wa kocha Zinedine Zidane lakini

Antoine Griezmann alipasia nyavu na kuamua mchezo huo umalizike kwa timu hizo kugawana pointi.

Kocha Zinedine Zidane alisema hakufurahishwa na matokeo hayo na hakusita kuwatupia lawama wachezaji wake akisema hawakuwa na utulivu.

“Nililiona bao (tulilofungwa, hatukuzuia vizuri. Ulikuwa ni mpira uliotoka nyuma  na hatukuwa tumejipanga vizuri. Ni sare lakini tumekosa pointi mbili,” alisema Zizou na kuongeza kuwa kikosi chake kilicheza vizuri na kilistahili ushindi.

Hiyo ilikuwa ni mara ya kwanza kwa Madrid kushindwa kuibuka na ushindi dhidi ya Atletico katika michezo minne iliyochezwa Bernabeu na mtanange huo ulikuwa wa 22 kuzikutanisha timu hizo tangu mwaka 2012.

Madrid watakuwa na nafasi nyingine ya kuzifukuzia ndoto zao za kuchukua ubingwa msimu huu watakapokuwa ugenini Aprili 15 kukipiga na Gijon.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -