Tuesday, November 24, 2020

MADRID NDANI YA MTIHANI MZITO WA COPA DEL REY

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

MADRID, Hispania


KAMA kuzungumzia historia kwenye soka ni jambo zuri, basi kwa Real Madrid ni kama nuksi kwani kichapo cha mabao 2-1 walichokipata usiku wa kuamkia jana kwenye nusu fainali ya kwanza ya Copa del Rey dhidi ya Celta Vigo kwenye dimba lao la Santiago Bernabeu, kimeibua historia ya kukatisha tamaa dhidi yao.

Mabingwa hao wa Ulaya na duniani, ambao walikuwa wakitamba hivi karibuni kwa kushinda mechi mfululizo hadi kufikia mechi 40 bila kupoteza, walijikuta wakichapwa mchezo wa pili mfululizo.

Celta walianza kuziona nyavu za Madrid kipindi cha pili kupitia kwa Iago Aspas lakini dakika chache baadaye, Marcelo alisawazisha bao hilo kabla ya Jonny Castro kupachika bao la ushindi kwa upande wa Celta.

Kichapo hicho kiliibuka historia kuwa ‘Los Blancos’ hao waliwahi kuondolewa mashindanoni dhidi ya timu mbili ambazo ziliwafunga mabao 2-1 kwenye mechi ya kwanza wakiwa Bernabeu.

Mara ya kwanza ilikuwa ni 1995 dhidi ya Valencia, mchezo wa marudiano Madrid walishindwa kusawazisha na kujikuta wakiondolewa kwa jumla ya mabao 2-4.

Hivi karibuni pia, wakiwa chini ya utawala wa kocha Jose Mourinho, Madrid walijikuta wakilazimishwa sare ya mabao 2-2 ugenini dhidi ya Barcelona, baada ya kubugizwa mabao 2-1 Bernabeu. Je, watauvunja huu mwiko wa kushindwa kugeuza matokeo baada ya kufungwa nyumbani dhidi ya Celta kwenye mchezo wa marudiano ugenini? Tusubiri tuone.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -