Saturday, November 28, 2020

MAGUFULI AMTOA LUPANGO NEY WA MITEGO

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA RAMADHAN HASSAN, DODOMA

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli, ameagiza msanii wa muziki wa kizazi kipya, Elibariki Emmanuel ‘Ney wa Mitego’, kuachiwa mara moja huku akiruhusu wimbo wake wa Wapo upigwe mahali popote.

Juzi msanii huyo alikamatwa maeneo ya Turiani, mkoani Morogoro akitokea Mpwapwa, Dodoma kupitia Kongwa ambapo sababu za kukamtwa kwake ni kuhisiwa kuwapo kwa maneno ya kuudhi na kukashifu katika wimbo wake wa Wapo.

Akizungumza na waandishi wa habari jana mjini hapa, Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe, alisema alizungumza na Rais Magufuli na kuagizwa msanii huyo aachiwe kwani ametoa wimbo mzuri.

“Niliweza kubahatika na kuongea na Mheshimiwa Rais hata suala la huyu mwanamuziki likajitokeza, maana naye ni mpenda muziki sana, akaniuliza hivi kuna nini, ni haya ninayoona katika magazeti? Nikasema na mimi nimekuja kuthibitisha sababu ni huo wimbo wake unaoitwa Wapo.

“Mheshimiwa Rais akaniuliza: ‘Umeusikia huo wimbo?’ Nikamwambia bado, akaniambia ‘hebu utafute au mimi nikutumie?’ Bahati nzuri anao na anausikiliza kila siku, juzi, jana na leo, akaniambia kwamba anaupenda na mimi nikausikiliza vizuri sana.”

“Si kwamba Basata (Baraza la Sanaa la Taifa) wamevunja sheria, wamefuata sheria iliyoanzisha hicho chombo na wao kwa imani kabisa huo wimbo umekiuka maudhui, hiyo sheria iliyoanzishwa na Basata pamoja na kanuni zake, kwahiyo wakatumia hiyo sheria kumkamata na kumpeleka jijini Dar es Salaam.

“Lakini huku mimi wameniandikia ujumbe kuwa hili suala la Waziri unalionaje, ikabidi na mimi niwasiliane na viongozi wakuu wa Wizara na Naibu Katibu Mkuu na kuwaeleza kwamba hata Rais naye ameshangaa,” alisema.

Alisema Rais alimuomba aangalie suala hilo akidhani kuwa msanii huyo alichofanya ni kuelezea hisia zake, hivyo kiongozi huyo wa nchi kuagizwa Ney wa Mitego kulindwa kwani hajavuka mipaka.

Waziri huyo alisema: “Pia Rais Magufuli ameshauri wimbo huo uboreshwe ili uwe mzuri zaidi na kwamba, asiondoe kitu chochote ila aongeze kwa sababu unazungumzia changamoto zilizopo katika jamii, halafu watu wanaitikia wapo… Watu wenye tabia hizi wapo…Rais ameagiza aongeze wakwepaji kodi, aongezee watu kama hao wapo; wabwia unga na mihadarati, wapo… Watanzania kwenye vijiwe hawafanyi kazi, waitikie wapo.”

Alisema kuwa Rais Magufuli amewashauri Basata kumpeleka Ney wa Mitego Dodoma akidai atafurahi mno kumwona ili amwelekeze vizuri hata mambo ya kuongeza katika wimbo wake huo akiamini utakuwa mzuri zaidi.

Kuhusiana na wimbo kupigwa au kutopigwa, Waziri Mwakyembe alisema: “Hata mkuu wa nchi ana mawazo kama hayo, hata mimi nitakuwa naupiga sana, kuna watu wana vitabia vya ajabu, hivyo tunatakiwa tuitikie kwa pamoja, ‘wapo’.”

Wakati huo huo, Jeshi la Polisi Kituo cha Kati, Dar es Salaam, jana lilimwachia msanii huyo ikiwa ni saa chache baada ya agizo la Rais Magufuli.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -