Thursday, October 22, 2020

MAGULI:SIMBA,YANGA,AZAM ZINASAJILI KUONGEZA IDADI

Must Read

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu...

NA ZAINAB IDDY
ELIASI Maguli ni moja ya washambuliaji waliopitia changamoto nyingi katika soka la Tanzania, lakini kwa sasa angalau ameweza kupiga hatua nyingine mbele  baada ya kupata nafasi ya kukipiga soka la  kulipwa nchini Oman.

Maguli kwa sasa anaichezea klabu ya Dhofar SC inayoshiriki Ligi Kuu ya Oman aliyojiunga nayo  kama mchezaji huru baada ya kumaliza kandarasi yake ya mwaka mmoja katika klabu ya hapa nyumbani ya  Stand United  ya mkoani Shinyanga.

Kabla ya kwenda Oman, Maguli alikabiliana na vikwazo vingi katika soka la Tanzania ambalo limetawaliwa na kila aina ya figisu figisu.

Kwa mfano wa  vikwazo hivyo au changamoto hizo ni pale aliposhuhudia klabu zote mbili alizopata kuzitumikia Simba na Stand zikiandamwa na migogoro ikihusisha ama  viongozi na wachezaji au viongozi kwa viongozi.
Mazingira hayo  yalikuwa mtihani kwa  mchezaji mchezaji huyu katika  kutimiza malengo yake ingawa sasa usemi wa ‘Mungu hamtupi mja wake’ unaonekana una maana kwake baada ya kutua Omani.
Jambo zuri zaidi kwa Maguli ni kwamba kwenye  kikosi chake cha  Dhofar SC ameweza kulishawishi benchi la ufundi  kumpa nafasi ya kuanza katika kikosi cha kwa kwanza na kuwa moja ya wachezaji tegemewa.
Katika mechi tatu alizoichezea timu hiyo Maguli amefanikiwa kufunga mabao mawili,Dhofar SC ikiwa imecheza mechi nne za Ligi Kuu nchini humo kabla ya mchezo wa jana Ijumaa dhidi ya Al-Nasr.
BINGWA  limefanya mahojiano na Maguli akiwa nchini Oman   ambaye anazungumzia maisha yake ya kisoka nchini humo na matarajio yake kwa siku za usoni.

Safari ya Oman ilivyokuwa
Maguli anasema  kabla ya kwenda Oman alipokea  ofa nyingi za ndani na nje ya nchi,ndani ya Bara la Afrika na nchi ya Afrika.

“Wakati naendelea na ligi Tanzania nilikua na hizo ofa nyingi na nzuri sana kwangu, ofa hizo zilikuwa na hapo nyumbani na nje ya Tanzania,baadhi zilinitaka wakati wa dirisha dogo na hata baada ya kumalizika kwa msimu, lakini nilivuta subira .Hata hivyo zile za nyumbani nilizikataa.

“Kuna wakati Klabu ya Super Sport ya Afrika Kusini ilinitaka kwaajili ya majaribio,ingawa pia w alikuwa wameziona video zangu. Lakini hawa jamaa wa  Omana walikua tayari washanifutilia nilipokua timu ya taifa, kwa hiyo wao hawakuhitaji  majaribio zaidi ya  kuchukua vipimo vya afya tu na  kumalizana nao kwenye suala ya mkataba.

“Hapa ndipo nilipoona hakuna haja ya mimi  kwenda kwenye majaribio, bora nikafanyiwe vipimo kisha  nijiunge nao hawa jamaa wa huku  na ndicho kilichofanyika, lakini hayo yote yalifanywa kwa usiri kwani nilihofia watu kunizunguka kasha  kuliua hili suala ukizingatia sio mara ya kwanza kupata ofa kama hizi lakini mwisho zinahishia kwenye vyombo vya habari tu,”anasema Maguli.

Kwanini alizipiga chini Simba, Yanga, Azam

Simba,Yanga na Azam FC zilikuwa na mipango na kumsajili Maguli kabla ya uamuzi wake wa kutimkia Omani,hapa anazungumzia sababu iliyomfanya azikache.

“Ni kweli Simba,Yanga na Azam zilikuwa zinanihitaji,lakini niliamua kuzipiga chini ofa zao kutokana na ukweli kwamba jamaa huwa wanasajili kwaajili ya kuongeza idadi ya wachezaji lakini si kuwatumia,ukiangalia katika klabu hizo kuna wachezaji  wachezaji wengi ninaocheza nao namba moja lakini  hawapati nafasi.

“Lakini nilihitaji pia kutimiza lengo la kupata changamoto za kucheza soka la kulipwa , hivyo nisingekuwa tayari kusaini timu za nyumbania mbazo mara nyingi zinalemaza wachezaji,”anasema.

Hataki kusikia soka la Tanzania.

“Nina takribani miaka mitano nacheza soka la Tanzania ukianzia Ligi Daraja la Kwanza hadi Ligi Kuu, kutokana na  changamoto zake kiukweli sitamani kurudi kucheza mpira wa ndani.

Anasema hata kama atashindwa kufanya vizuri nchini Omani hatakuwa tayari kwenda mahali pengine lakini sio kurudi nyumbani kuzichezea  timu kubwa inatokana na ubabaishaji uliopo.

“Malengo yangu ni kusonga mbele sio kurudi nyuma, ndio maana hivi sasa najituma ili nitimize ninachokitaka pasipo kuangalia timu gani nacheza, kikubwa nitoke nilipo sasa na kusogea mbele,”anasema.

Tofauti ya soka Oman,Tanzania

“Tofauti ipo kubwa sana kwa mchezaji mmoja mmoja, hawa jamaa wametuzidi kiukweli ,kwani licha ya ushindani wa namba kutokana na kujituma kwa wachezaji lakini pia hata uendeshaji wao wa ligi ni bora zaidi yetu.

“Katika suala la uendeshaji wa ligi, timu yenye uwezo ndiyo inayostahili kushinda bila kuangalia kama ni kubwa ama ndogo,waamuzi nao wako makini kuhakikisha haki inatendeka.

“Ni vigumu kumkuta refa akifanya kazi kinyume na sheria ya soka , kwani hakuna kubebana wala kufichiana uovu ,shirikisho lenyewe la soka lipo makini tofauti na hapo nyumbani ubabaishaji mwingi kuanzia katika klabu hadi shirikisho,”anasema

Mechi yake ya kwanza Oman

“Aisee hii sitoisahau kabisa kwani ni mechi ambayo nilikuwa na hofu nyingi, lakini pia nikajikuta naumia kifundo cha mguu na kutolewa dakika ya 20  na kukaa nje  kwa wiki moja kitu ambacho kilinifanya nishindwe kucheza mchezo unaofuata ,”.anasema

Ushindani wa namba

“Ushindani wa namba ni mkubwa sana tofauti na Ligi ya  Tanzania na hakuna kujihakikishia namba ya kudumu, kwani ukicheza chini ya kiwango kwenye mechi moja ndio umejipa tiketi ya kukaa benchi.

“Kwa mfano katika klabu yetu tuko mastraika wanne na wote tunahitaji kuanza kikosi cha kwanza hivyo lazima ujitume ili kupata nafasi,”anasema

Anaifuatilia Ligi ya Tanzania hatua kwa hatua

Licha ya kutotamani tena kucheza soka katika lIgi Kuu ya Tanzanai Bara , lakini Maguli anasema kuwa anaifuatilia ligi hiyo hatua kwa hatua .

“Tanzania ni nyumbani hivyo kila kinachoendelea lazima nikijue kwa kwani kila asubuhi na jioni lazima nipitie kwenye mitandao kujua kipi kimejili na ndio maana inakuwa rahisi kujua ligi imefikia hatua gani na nini kinaendelea,”.anasema.

Anasema kulingana na ligi ilipofikia sasa ni vigumua kusema timu gani inastahili kutwaa ubingwa kwani mara nyingi kumekuwa na kawaida ya kubadilika kutokana na waamuzi kuingia na matokeo mfukoni.

Wito wa wanandinga wa kibongo
“Kikubwa ni kujituma tu kwani huwezi jua ni wapi unaweza kuonekana, binafsi sikujua kama siku moja nitaangukia hapa lakini imekuwa hivyo kwani waliniona kwenye mechi ya Algeria wakaanza kunifuatilia.

“Juhudi na malengo ndio jambo kubwa na la muhimu katika maisha yoyote yale na wasiache kumshirikisha  Mungu kwani ndio kimbilio la kila mmoja wetu, lakini pia nawashukuru kwa sapoti yao kwangu na wasichoke waendelee kuniunga mkono wachezaji na Watanzania kwa ujumla kwani hakuna fanani bila ya hadhira,”anasema.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya wanamuziki wa Tanzania ambao miongoni...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara  (VPL), utakaochezwa leo...

Mugalu atema cheche Simba

NA ASHA KIGUNDULA MSHAMBULIAJI wa Simba, Chris Mugalu, amesema wanakwenda mkoani Rukwa kupambana na kupata ushindi katika mchezo wao...

Malale aitisha Yanga

NA ZAINAB IDDY KOCHA Mkuu wa timu ya Polisi Tanzania, Malale Hamsini, amezisikia sifa za kocha mpya wa Yanga,...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -