Thursday, October 29, 2020

Maisha Manase: Mwimbaji wa Gospo anayepeta Marekani

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

MIONGONI mwa wanamuziki wa Injili wenye asili ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC)  waofanya vyema nchini Marekani ni Maisha Manase anayeishi mjini Chicago.

Safu hii imefanikiwa kufanya mahojiano ni mwimbaji huyo ambaye kwa sasa anafanya vizuri na wimbo, Nitafika.

BINGWA: Kwa asiyekufahamu Manase ni nani?

Maisha: Mimi ni mwimbaji ambaye naishi hapa Chicago, Illinois, Marekani kwa kweli namshukuru Mungu amenipa nafasi ya kumtumikia kwa sababu ni mengi sana nimeyapitia kwenye maisha yangu magumu na mazito lakini Mungu amekuwa upande wangu.

Uimbaji nilianza toka nikiwa Kongo na niliridhi kutoka kwa mama yangu mzazi na imenipa fursa ya kumtumikia Mungu na ndio ninachojivunia japo haikuwa rahisi kufika hapa nilipo ni Mungu tu ndie anayeniwezesha.

BINGWA: Changamoto zipo unazipata kwenye muziki wako hapo Marekani?

Maisha: Moja ya changamoto kubwa ninayopitia ni upande wa utayarishaji wa kazi zangu kwa sababu maprodyuza wote ninaofanya nao kazi wapo Afrika kwahiyo mpaka kazi itoke inakuwa ni changamoto kubwa kwenye maelewano ya utendaji kazi ili mawazo na hisia zangu ziwafikie mashabiki kama ninavyotaka.

Jambo lingine watu bado hawana mwitikio mkubwa sana na hasa hapa Marekani kwenye kazi za Gospo kwahiyo mara nyingi tunafanya tu kwa sababu ni huduma na sio kupata faida.

BINGWA: Kwanini uliamua kufanya Gospo na sio Bongo Fleva?

Maisha: Amani ya moyo wangu ndio iliamua na haswa nikikumbuka mambo mengi niliyopitia, najua ni Mungu alinivusha kwahiyo hakuna namna ninayoweza kukwepa kumtumikia.

BINGWA: Sasa hivi Marekani kuna maandamano ya kupinga ubaguzi wa rangi, kwako yameathiri chochote kwenye muziki wako?

Maisha: Kwa kweli hapana haijaathiri chochote, namshukuru Mungu.

BINGWA: Kwanini Kwenye video ya wimbo, Nitafika umecheza kama mtu masikini?

Maisha: Kwa sababu ni kitu nilichowahi kukipitia kwenye maisha yangu kipindi cha nyuma, nina amini kuna watu wengi wanapitia hali ngumu pengine hata zaidi kwenye hali tofauti tofauti lengo nikutia moyo na kuwakumbusha wale ambao walishawahi kupitia hayo kuwa ni Mungu aliwavusha, hatupaswi kukata tamaa, Mungu bado yuko kazini

BINGWA: Mapokezi ya video yako yapo vipi?

Maisha: Kwa kweli namshukuru Mungu, mapokezi yamekuwa makubwa sana, yanatia moyo na nina washukuru watu wote walioipokea kazi hii kwakweli wametia nguvu ya kufanya vizuri zaidi na kunipa moyo.

Pia nyimbo mpya ninazo nyingi, nasubiri kibali kutoka kwa Mungu ili nijue niachie upi tena hapo baadaye kwa sababu nimeupa nafasi kwanza wimbo wa, Nitafika.

BINGWA: Wasanii gani wa Afrika Mashariki unatamani kufanya nao kazi?

Maisha: Yeyote ambaye Bwana atanipa kibali cha kufanya naye kazi na hasa asiwe msanii tu awe mtumishi wa Mungu?

BINGWA: Tukiwa katikati ya mwaka 2020, una mipango ipo kwenye muziki wako?

Maisha: Nina malengo ya kukuza huduma yangu katika viwango vingine na kuiachia kazi bora zaidi na zitakazogusa mioyo ya watu katika kumtumikia Mungu

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -