Wednesday, October 28, 2020

MAISHA, MAPITO YA MSANII MASHAKA HADI KIFO CHAKE

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

NA JEREMIA ERNEST

*Aliigiza kama mlemavu akapata kweli ulemavu

*Ameacha lawama kubwa kwa wasanii wenzake

MSANII mkongwe wa sanaa za maigizo nchini, Ramadhani Mrisho Ditopile ‘Mashaka’, amezikwa juzi Jumapili katika makaburi ya Kinyerezi, jijini Dar es Salaam baada ya kufariki mwishoni mwa wiki.

Mashaka alifariki kwa ugonjwa wa shinikizo la damu juzi Jumamosi katika Hospitali ya Amana iliyopo Ilala, jijini Dar es Salaam, alikokuwa amepelekwa kwa ajili ya kupatiwa matibabu siku moja kabla ya kifo chake.

Pamoja na shinikizo hilo la damu, pia marehemu alikuwa akisumbuliwa na kisukari ambapo siku moja kabla ya kifo chake alizidiwa ghafla usiku na kukimbizwa Hospitali ya Amana na madaktari walifanikiwa kumpa huduma ya kwanza na matibabu ikiwa ni pamoja na kumwekea mashine ya kupumulia.

Asubuhi yake hali ilizidi kuwa mbaya na madaktari Amana walitoa rufaa ya kumpelekea katika Hospitali ya Muhimbili (Mloganzila), wakati wakiandaa gari la wagonjwa, Mashaka akakata roho.

Marehemu Mashaka ni kati ya wasanii waliotikisa mno katika tasnia hiyo ya maigizo miaka ya 1990, akiwa katika Kundi la Kaole Sanaa Group na kuibua vipaji vingi.

Miezi saba kabla ya kifo chake, gazeti la BINGWA lilifanya mazungumzo na msanii huyo nyumbani kwao Ilala Bungoni na kuzungumzia maisha yake kabla na baada ya kuingia katika sanaa pamoja na mafanikio na yale yaliyomkwamisha.

Marehemu ambaye kabila lake ni Mndengereko, alizaliwa mwaka 1961, jijini Dar es Salaam na kupata elimu ya msingi Shule ya Amana iliyopo Ilala, baadaye alijiunga na Chuo cha DMI kwa ajili ya kozi fupi ya ubaharia.

LINI ALIANZA SANAA?

Katika mahojiano hayo marehemu alisema aliyegundua kipaji chake ni mwigizaji mkongwe, Rajab Kibwana Hatia ‘Mzee Pwagu’ (marehemu), ambaye alikuwa akienda kukaa kijiweni Ilala karibu na duka lao alilokuwa akiuza Mashaka.

“Mara nyingi nilikuwa nikimuiga sauti yake lakini baadaye nilihama kwenye duka lile la Ilala na kumwacha dada yangu, mimi nikaenda Ubungo. Siku moja dada yangu akanipigia simu nikitoka chuo niende dakani kuna ujumbe wangu kutoka kwa Mzee Pwagu,” alisema Mashaka.

Alisema alipoenda akakutana na Mzee Pwagu ambaye alimwambia kuna igizo wanafanya na ameona yeye anafaa na kumpeleka Kaole Sanaa Group wakati huo ndio kundi hilo linaanzishwa na marehemu Mzee Kipara, marehemu mama Ambiliki, Bi Kidude na Bi Hindu, baada ya kucheza igizo hilo lilipelekwa ITV kisha wakapewa mkataba na kituo hicho.

MAFANIKIO NA CHANGAMOTO

“Baada ya kujulikana kwa kipindi kile nilipata matangazo, hivyo nikawa na kipato kupitia matangazo niliyokuwa nafanya,” alisema Mashaka.

Alisema aliweza kuendesha familia yake kwa kazi ya sanaa na alipata mtaji na kuanza kulima, pia kujulikana na watu tofauti kulimfanya aweze kwenda sehemu mbalimbali kwa sababu ya kujulikana.

Msanii huyo ambaye alitamba kwenye mchezo wa Kabla Hujafa Hujaumbika, ambao aliigiza kama mlemavu na kurushwa kwenye kituo cha runinga cha ITV, alisema pamoja na mafanikio lakini alikutana na changamoto nyingi na kuamini kwamba ni kweli hujafa hujaumbika, kutokana na yale yaliyomtokea kwenye maisha yake.

“Kweli nimeamini hujafa hujaumbika, kwa kuwa hili nimelishuhudia kwenye maisha yangu, nilipata ajali mwaka 2006 wakati natokea shambani kwangu Tanga katika Kijiji cha Kilindi, mguu ukavunjika mara tatu,” alisema Mashaka.

“Nililazwa kwa muda mrefu na baadaye kupona na kuanza kazi zangu, lakini miaka saba baadaye nilipooza na baada ya uchunguzi ikagundulika kuwa na mafuta mengi mwilini.”

Pamoja na kupona na kuendelea vizuri, lakini mguu wake haukurudi kwenye hali yake ya kawaida kwani alikuwa akiuburuza wakati anatembea na kuwa na ulemavu ambao aliugiza kwenye tamthilia ya Hujafa Hujaumbika.

Lakini pamoja na hali hiyo, aliweza kufanya kazi zake kama kawaida, lakini nilishangazwa na kitendo cha kutelekezwa na wasanii wenzake ambao wengine aliwaibua mwenyewe.

Alisema kwenye sanaa amepitia mambo mengi sana na anakumbuka aliwahi kupigwa Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere, kwa sababu aliigiza na msanii mwenzake aitwaye Zawadi kama baba anayetesa watoto.

“Kuna baba alinivamia na kunitia kabali na kuniuliza kwanini nawatesa watoto, lakini baada ya kumwelewesha aliweza kunilipa,” alisema Mashaka.

“Pia sanaa iliwahi kunifanya nilale mzungu wa nne na mke wangu, baada ya kurejea nyumbani nikiwa na rangi ya mdomo kwenye shati, nilijaribu kumwelewesha kuwa aliyenipaka ile rangi ni Zawadi ila hakutaka kunielewa akidhani nilikwenda kwa mchepuko. Lakini alipokuja kuona lile igizo ndipo akaamini.”

Mashaka alikanusha usemi wa wengi kwamba marehemu Steven Kanumba amekufa pamoja na filamu za Bongo na kusema kwamba tatizo hawana nyota, lakini wanaweza kuigiza vizuri na tasnia hiyo haijafa.

Pia alimsifia Ben ‘Serengo’ akisema kuwa hajapata mtu wa kumsimamia na nyota, ila ni msanii mzuri zaidi ya Kanumba kwani unaweza kumpa sehemu yoyote akacheza.

MAMBO ALIYOKUWA AKIFANYA KABLA YA KIFO CHAKE

Marehemu alikuwa akiishi Rombo, Ubungo na familia yake huku akifanya shughuli za kilimo mkoani Tanga na biashara ndogo ndogo, pia alikuwa akitunga nyimbo za muziki wa taarabu kwa bendi mbalimbali na msanii yeyote kulingana na walivyokuwa wakikubaliana. Kabla ya kifo chake alikuwa akitafuta mfadhili wa kumwezesha kutoa filamu yake ambayo hakuitaja jina, ingawa mwenyewe alisema ni filamu ambayo haikuwahi kutokea.

 

 

 

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -