Monday, October 26, 2020

MAJAJI MSIMWANGUSHE BASILA MISS TANZANIA 2018

Must Read

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian...

WAREMBO 20 wanaoshiriki fainali za shindano la Miss Tanzania, wameanza kambi mwishoni mwa wiki iliyopita, wakijichimbia katika Hoteli ya Serena, iliyopo Mbezi Beach, Dar es Salaam.

Walimbwende hao watajifua vikali ndani ya wiki mbili tayari kuchuana kuwania taji litakalomwezesha mshindi kukata tiketi ya kushiriki mashindano ya dunia, yaani Miss World.

Kwa wakati wote watakaokuwapo kambini, warembo hao watakuwa wakinolewa katika miondoko ya kiuanamitindo (catwalk) au minato, nidhamu, kujitambua, kufahamu na kuvielezea vivutio vya utalii wa Tanzania, ushirikiano, upondo, mambo ya kijamii, afya na mengineyo.

Kabla ya fainali za shindano hilo, kutakuwa na mashindano madogo madogo yanayotoa tiketi ya kutinga nusu fainali kwa watakaofanya vizuri.

Mashindano hayo ambayo yapo hata Miss World, ni michezo (Sports), mwanamitindo bora (Top Model), mvuto wa sura katika picha (Photogenic), Urembo kwa Malengo (Beauty with Purpose), mrembo wa mashabiki (World Multimedia) na mrembo mwenye kipaji (Talent).

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam mwanzoni mwa wiki, Mkurugenzi wa Kampuni ya The Look, waandaaji wa shindano hilo, Basila Mwanukuzi, alisema kuwa fainali za shindano hilo zitafanyika Septemba 8, mwaka huu, kwenye Ukumbi wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, jijini.

Alipoulizwa juu ya suala zima la majaji wa fainali za mwaka huu, Basila aliwataka mashabiki wa urembo kutokuwa na wasiwasi, kwani wamejipanga kuhakikisha haki inatendeka kwa kila mshiriki.

“Majaji majina yao yameshapelekwa Basata (Baraza la Sanaa la Taifa), wao ndio wanapitia CV (wasifu) zao, baada ya hapo watachagua majina na kuyarudisha katika Kamati ya Miss Tanzania,” alisema.

BINGWA tukiwa kama miongoni mwa wadau wa mashindano hayo ya urembo nchini, tungependa kuwatakia kila la heri warembo wote waliopo kambini kulisaka taji la Miss Tanzania 2018.

Lakini pia tutoe wito kwa Kamati ya Miss Tanzania kuwa makini katika suala zima la majaji ili kuepuka udanganyifu wowote ule unaotokana na ushawishi kutoka kwa jamaa za washiriki.

Uzoefu unaonyesha kuwa mara nyingi majaji wamekuwa chanzo cha kuvuruga shindano hilo kwa kuwapa ushindi warembo wasio na sifa na mwisho wa siku, lawama kuwaangukia waandaaji.

Kwa kuwa Basila hili ndilo shindano lake la kwanza akiwa kama mratibu, ahakikishe anawasimamia vilivyo majaji ili wasijemwangusha kama ilivyokuwa huko nyuma.

Basila ni vema akafahamu kuwa iwapo majaji wataboronga, lawama zote zitaelekezwa kwake na si Basata au jaji yeyote yule.

Tumalizie kuwa kumpongeza Basila kwa kuingia kwa kishindo katika mashindano hayo, kwnani japo ni mwaka wake wa kwanza, amefanikiwa kuvuna warembo wenye ubora wa hali ya juu ambao ni wazi watawapa wakati mgumu mno majaji kumpata mshindi.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya kuwa na umri wa miaka...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian Mbappe na Neymar, kwenye mechi...

IBRA:Kifaa kipya Konde Gang aliyetembea kwa mguu kumwinda Harmonize

NA BRIGHITER MASAKI UKITAJA vijana wanaofanya vizuri katika mziki wa bongo fleva, huwezi kukosa kumtaja msanii chipukizi anayefahamika zaidi...

Jay-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas

-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas New York, Marekani HAKUNA shabiki wa Hip hop asiyelifahamu...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -