Monday, January 18, 2021

Majaliwa aongoza kumuaga Tahir

Must Read

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi...

NA RAMADHAN HASSAN, DODOMA

WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa, ameongoza wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuuaga mwili wa mwamuzi wa kimataifa wa Tanzania,  marehemu Hafidh Ally Tahir katika Uwanja wa Ndege wa Dodoma.

Tahir alikuwa ni Mbunge wa Jimbo la Dimani kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Marehemu Tahir alifariki jana majira ya saa 9 alfajiri katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma kutokana na shinikizo la damu.

Kifo hicho kilithibitishwa na mganga mkuu wa hospitali hiyo, Dk. James Kiologwe, ambaye alisema Tahir alifika muda huo akiwa na gari yake huku akilalamika sehemu za kifuani kubana.

Mwili huo ulisafirishwa jana saa 11:45 asubuhi kwa ndege kwenda Zanzibar huku wabunge wa Bunge hilo wakimlilia kutokana na kuwa ni mmoja ya watu waliosaidia michezo bungeni na Tanzania kwa ujumla.

Mbali na Majaliwa, pia alikuwepo Spika wa Bunge hilo, Job Ndugai na kiongozi wa kambi ya upinzani Bungeni, Freeman Mbowe.

Akizungumza na BINGWA jana katika uwanja huo, kocha wa timu ya Bunge Sports Club, Venance Mwamoto, alisema marehemu alikuwa ni mtu muhimu kutokana na kuwa kiunganishi katika timu ya Bunge na michezo kwa ujumla.

Akimzungumzia marehemu alisema amefahamiana naye wakati akiichezea timu ya Majimaji kutokana na kuchezesha michezo mingi ya Ligi Daraja la Kwanza wakati huo.

“Nimehuzunika sana kumpoteza mtu wa michezo, alikuwa mwamuzi ambaye  alisimamia haki na pia tulisoma naye mafunzo ya juu ya ukocha Zanzibar kabla ya mimi kwenda Ujerumani, hapa katika timu ya Bunge mimi kocha mkuu yeye ni msaidizi wangu,” alisema.

Mwenyekiti wa timu ya Bunge Sport Club, William Ngeleja, alisema hadi saa tatu usiku wa jana walikuwa na marehemu wakipanga mipango ya kushiriki katika mashindano ya Mabunge ya Afrika Mashariki wakijadili ushiriki wa timu hiyo.

Alisema wakati wakiwa katika vikao hivyo hakuonesha dalili za kudhoofika kiafya na walikuwa wakicheka  pamoja na kujadiliana jinsi ya kuhakikisha timu hiyo inachukua ubingwa katika mashindano hayo.

‘’Kifo ni siri ya Mwenyezi Mungu, ila mimi nimepokea kwa masikitiko zaidi sisi familia ya michezo tutammisi sana kwa mambo matatu, alikuwa ni kocha hivyo tutakosa ujuzi wake, pili alikuwa ni mwamuzi hivyo alikuwa anatusaidia kutuelekeza sheria na tatu  alikuwa ni mchezaji wetu,’’ alisema.

Marehemu Tahir amezaliwa Oktoba 30 mwaka 1953, Dimani Zanzibar na elimu ya msingi aliipata Shule ya Kombeni mwaka 1957-1966  na sekondari akisoma katika shule hiyo hiyo.

Mara baada ya kumaliza masomo yake hapa Tanzania alienda Yugoslavia kwa masomo ya juu na baadaye Misri.

Tahir amefanya kazi kwa muda mrefu katika redio ya Zanzibar (ZBC).

Pia katika uhai wake amechezesha fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) mara 9 pamoja na mashindano ya dunia kwa vijana chini ya miaka 17.

Vilevile ni mwamuzi ambaye alikuwa akichezesha michezo mikubwa Tanzania na barani Afrika mfano wa mechi hizo ni Zamaleck na Al Ahly za Misri.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na ndiyo maana timu hiyo imeshinda...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi Kuu Tanzania Bara katika kipindi...

JDart Nation wapanga kutawala Africa

CHRISTOPHER MSEKENA MWANAMUZIKI na bosi wa JDart Nation, JDart, amesema miongoni mwa mipango yake kwa mwaka 2021 ni kuhakikisha...

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki za Ligi Kuu Tanzania Bara...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -