Friday, December 4, 2020

ARSENAL INA NINI? KUTOKA NAFASI YA KWANZA HADI YA NNE NDANI YA SIKU TISA?

Must Read

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

LONDON, England

BAADA ya kuongoza msimamo wa Ligi Kuu England dhidi ya Chelsea kufuatia ushindi wa michezo mitatu kati ya saba iliyowasaidia kufikia kileleni, matumaini ya ubingwa kwa klabu ya Arsenal yameanza kuning’inia kwenye kuti kavu kwa sasa.

Hadi kufikia Desemba 10 mwaka huu, vijana hao wa kocha Arsene Wenger, walikuwa wanaongoza msimamo wa ligi baada ya kuzoa pointi tatu dhidi ya Stoke City, lakini wamejikuta wakishuka hadi nafasi ya nne kabla hata sikukuu ya Krismasi haijafika.

Mtandao wa Sportsmail umechambua yaliyotokea nyuma ya pazia juu ya mwenendo usioridhisha wa washika bunduki hao wa London.

Kutokuwepo kwa Cazorla ni tatizo

Ni wazi kuwa kiungo Santi Cazorla ni mtu muhimu ndani ya kikosi cha Arsenal.

Hata kocha, Arsene Wenger, anatambua kuwa bila ya Mhispania huyo Arsenal haijakamilika kwani katika michezo tisa ya ligi kuu aliyokosekana, Arsenal imeshinda minne tu.

Ni kiungo muhimu chenye uwezo wa kuiunganisha vyema safu ya ulinzi na ushambuliaji na taarifa mbaya ni kwamba atakosekana uwanjani kwa muda mrefu atakaoutumia hospitalini alikopumzishwa baada ya kufanyiwa upasuaji wa tatizo lake la muda mrefu la enka.

Granit Xhaka yupo, anaweza kutumika kwenye nafasi ya Cazorla kwa muda mrefu pia, lakini Wenger bado atamhitaji sana Cazorla mwenye umri wa miaka 32, kwa muda mrefu kadiri itakavyowezekana.

Hata hivyo, si Cazorla pekee anayeigharimu Arsenal kwa sasa bali hata kuumia kwa kitasa Shkodran Mustafi, ni tatizo lingine lililopelekea Arsenal kupoteza michezo miwili bila ya uwepo wake.

Sekeseke la mikataba

Ni wazi kuwa iwapo Arsenal itatangaza kwa pamoja kwamba Mesut Ozil, Alexis Sanchez na Arsene Wenger wameongezewa mikataba, ni picha nzuri mno itakayojengeka hapo.

Lakini shida iliyopo kwanza ni kuhakikisha hili sekeseke la mkataba linalotikisa ulimwengu wa washika bunduki na kuimeza klabu, linazimwa.

Wenger ana kazi kubwa ya kufanya msimu huu, wakati yeye pia akisaliwa na miezi 18 kabla ya mkataba wake kumalizika, Cazorla na Per Mertesacker, pia hawajaanza mazungumzo ya mkataba na dalili zinaonesha, ya msimu huu hayatakuwa na tofauti na misimu iliyopita.

 Hakuna beki wa kushoto wa maana

Kusema kwamba beki wa kushoto chaguo la kwanza, Nacho Monreal, ni uchochoro mkubwa hatutatenda haki kwake, lakini ukweli utabaki pale pale Mhispania huyo anahitaji kupatiwa changamoto kwa kusajiliwa beki mwenye uwezo wa hali ya juu kama alionao Hector Bellerin katika upande wa kulia.

Ozil hupotea kila anapohitajika

Si wote wanaotambua kuwa pindi Arsenal inapomhitaji Ozil kwenye nyakati ngumu, jamaa hupotea ghafla!

Lakini, katika kipigo cha juzi dhidi ya Manchester City, kiliwahuzunisha mashabiki na hata hasira alizozionesha kwenye mchezo dhidi ya Everton wiki iliyopita hazikuleta picha nzuri.

Nani ana shaka na kipaji murua cha Mjerumani huyu? Hakuna. Lakini nani aliyewahi kujiuliza ni wapi anapopotelea Ozil pindi timu inapohitaji uwezo wake wa kubadili mchezo mgumu kuwa mwepesi?

Klabu inaonesha kuwa tayari kumtimizia haja yake ya kulipwa pauni 200,000 kwa wiki ili asalie kikosini kwa miaka mitano, hata watu wa karibu naye wanasema jamaa anataka kubaki.

Lakini ukweli ni kwamba, Arsenal inahitaji mno kumwona kiungo wao huyo akicheza vyema hata kwenye mechi kubwa pia.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul 'Ben Pol' ameshukuru mashabiki kwa...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -