Saturday, November 28, 2020

MAJEMBE 11 YA LWANDAMINA YANGA

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA HUSSEIN OMAR

MAMBO sasa yameiva katika kikosi cha Yanga, kwani hadi sasa inaonekana Kocha Mkuu wa timu hiyo, George Lwandamina, amepata majembe 11 ya kikosi cha kwanza ‘first eleven’ atakachokitumia katika mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Ikiwa ni wiki ya pili tangu kocha huyo kuanza kuinoa timu hiyo, sasa ameonekana kujenga kikosi chake kwani kwenye mazoezi yanayofanyika kwenye viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam, Lwandamina ameonekana kupata majembe yake ya kuanza nayo.

Katika mazoezi hayo, Lwandamina amekuwa akiwaanzisha pamoja Ally Mustapha ‘Barthez’, Juma Abdul, Haji Mwinyi, Vincent Andrew, Kelvin Yondani, Justin Zulu, Simon Msuva, Thaban Kamusoko, Donald Ngoma, Amissi Tambwe na Deus Kaseke.

Kikosi hicho kinaweza kuwa ndicho cha kwanza hasa kutokana na jinsi ambavyo amekuwa akiipanga timu yake, kukazania mazoezi na kuwaelekeza mambo wachezaji walioko kwenye kikosi hicho.

Wakati ikiwa hivyo na ikielezwa kwamba hayo ndiyo majembe yake muhimu yaliyomgusa vilivyo hadi hivi sasa kocha huyo anaonekana kuwaacha kwenye kikosi cha kwanza nyota kadhaa akiwemo kipenzi cha mashabiki, Haruna Niyonzima.

“Huenda Niyonzima akaingia kikosi cha kwanza baadaye, lakini kwa sasa hayumo maana amechelewa kujiunga na wenzake hivyo hajafanya nao mazoezi ya kutosha,” anasema shabiki mmoja wa timu hiyo aliyekuwa kwenye mazoezi ya timu hiyo.

BINGWA lilishuhudia kocha huyo akiwapanga kwenye kikosi cha pili kipa Deogratius Munishi “Dida’, Hassan Ramadhani ‘Kessy’, Oscar Joshua, Mbuyu Twite, Vincent Bossou, Pato Ngonyani, Juma Said ‘Makapu’, Haruna Niyonzima, Obrey Chirwa, Malimi Busungu na Godfrey Mwashiuya.

Katika mazoezi ya jana yaliyoanza saa nane mchana, Ngoma alifunga bonge la bao kwa kichwa baada ya kumalizia pasi ya mwisho ya Abdul aliyepanda mbele kusaidia mashambulizi.

Ngoma alionyeshana kazi vilivyo na Bossou hali iliyomfanya kuomba penalti kila mara kwa kudai amechezewa faulo na beki huyo raia wa Togo.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -