Wednesday, October 28, 2020

MAJEMBE HAYA YANA UMRI MKUBWA LAKINI WANATISHA EPL

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

LONDON, England


WASWAHILI wanasema ‘ng’ombe hazeeki maini’. Ndiyo, pale Ligi Kuu England (EPL) kuna orodha ndefu ya mastaa wenye umri mkubwa lakini wameendelea kuwa kiwango cha juu.

Wanapokuwa uwanjani, suala la umri wao mkubwa huwa halina nafasi kabisa na badala yake unaweza hata kuwafananisha na makinda.

Ni mastaa gani hao na wanakipiga katika klabu gani ambazo zimeeendelea kuwang’ang’ania licha ya uzee wao?

Gareth Barry (Everton)

Kwa taarifa yako, mpaka sasa Barry ameshacheza zaidi ya mechi 600 na bado ni tegemeo kwenye kikosi chas Everton kilichopo chini ya Mholanzi Ronald Koeman. Mshikaji ana umri wa miaka 35 na ameendelea kuwa kwenye ubora wake.

Mwishoni mwa msimu uliopita, alishindwa kuwika kwenye kikosi cha Roberto Martinez na kulikuwa na shaka kuwa asingeweza kubaki na kocha mpya, Koeman.

Hata hivyo, imekuwa tofauti, kwani Koeman mwenyewe amekiri kuwa Barry ni miongoni mwa wanasoka wenye akili nyingi aliowahi kuwafundisha na amemtabiria kufikisha michezo 1,000.

Jose Fonte (Southampton)

Mkali huyo ana umri wa miaka 32 kwa sasa, lakini ni kama kinda aliyezaliwa miaka 20 tu iliyopita.

Amekuwa na namba ya kudumu kwenye kikosi chake cha Southampton na ni kipenzi cha mashabiki wa klabu hiyo.

Umri wake haumzuii kuwa nguzo imara ya safu ya ulinzi ya Southampton na amekuwa akitajwa kuwa ni mmoja kati ya mabeki bora wa kati.

Wakati wa dirisha la usajili la majira ya kiangazi, kocha Jose Mourinho alitaka kumpeleka Old Trafford, lakini mpango huo ulikwama.

Ni wazi Mourinho alimuona Fonte kuwa ni bora mbele ya Marcos Rojo na Phil Jones.

Ashley Williams (Everton)

Everton inatajwa kuwa miongoni mwa timu zenye wachezaji wengi wenye umri mkubwa.

Wachezaji wanne wa kikosi cha kwanza wana zaidi ya umri wa miaka 30. Nahodha huyo wa timu ya Taifa ya Wales ana umri wa miaka 32.

Licha ya ugeni wake pale Everton ambayo amejiunga nayo akitokea Swansea, Williams amekuwa tegemeo kwenye kikosi cha kocha Koeman.

Santi Cazorla (Arsenal)

Ukitazama kile anachokifanya dimbani, huenda ukakataa kuwa Mhispania huyo ana umri wa miaka 31.

Amekuwa kwenye kiwango cha juu tangu alipotua England mwaka 2012.  Katika msimu wake wa kwanza Arsenal, alifunga mabao 12 na kutoa asisti 12, huku akitajwa kuwa mchezaji bora wa mwaka klabuni hapo.

Kuanzia hapo amekuwa sehemu muhimu ya safu ya kiungo pale Emirates na hata anapokuwa nje kuuguza majeraha, pengo lake limekuwa likionekana.

Fernandinho (Manchester City)

Ni kiraka pale Etihad, unaweza kumpanga nafasi uitakayo na hayo yote anayafanya akiwa na umri wa miaka 31.

Kwa sasa ni nguzo kwenye safu ya kiungo na mara kadhaa amekuwa akitumika katika ulinzi.

Kutokana na uwepo wa mafundi David Silva na Ilkay Gundogan, Mbrazil huyo amekuwa aking’ara vilivyo.

Ndiye mchezaji pekee wa Man City ambaye amecheza dakika nyingi na hilo limemfanya kuwa mfano mzuri kwa wachezaji makinda kwenye ‘academy’ ya Etihad.

Zlatan Ibrahimovic (Man United)

Ni ngumu kutabiri kuwa huu utakuwa msimu wa mwisho kwa Msweden huyo, licha ya umri wa miaka 34 alionao hivi sasa.

Akiwa na umri huo, bado Ibrahimovic haonekani kuchoka na ameendelea kuwasumbua mabeki wa timu pinzani kwa kadri anavyotaka.

Kuna kipindi ilionekana kama straika huyo ameanza kupotea, lakini katika mechi za hivi karibuni amerudi upya.

Laurent Koscielny (Arsenal)

Kama ungeulizwa beki huyo kisiki wa Arsenal ana umri gani, basi ungeweza kutaja miaka 25 hadi 29. Ni kutokana na shughuli yake pevu uwanjani.

Mlinzi huyo wa kati ana umri wa  miaka 31 na hata  Rio Ferdinand aliwahi kusema kuwa Mfaransa huyo ndiye beki bora wa kati pale England, lakini bado ni muhimu kwenye kikosi cha Arsene Wenger.

Wayne Rooney (Manchester United)

Ingawa amekuwa akitajwa kushuka kiwango, lakini bado Rooney anabaki kuwa mmoja kati ya washambuliaji hatari duniani.

Ana umri wa miaka 30, lakini hakuna mchezaji mwenye umri huo ambaye amemzidi Rooney kwa kutoa pasi za mabao ‘asisti’.

Siku chache zilizopita, aliweka rekodi ya kuwa mchezaji aliyeifungia Man United mabao mengi kwenye michuano ya Ulaya. Unaanzaje kumbeza Mwingereza huyo?

James Milner (Liverpool)

Kama ilivyo kwa Rooney, Milner naye ana umri wa miaka 30, lakini shughuli yake uwanjani ni balaa tupu.

Ni chaguo la kwanza kwenye safu ya ulinzi ya kikosi cha Liver chini ya Jurgen Klopp.

Amekuwa akiingia uwanjani mara kwa mara, isipokuwa pale tu anapokuwa majeruhi ambapo pengo lake huzibwa na ‘kimeo’ Alberto Moreno.

David Silva (Manchester City)

Nani kakwambia umri wake wa miaka 30 ni tatizo anapokuwa kwenye kazi zake?

Hana umbo kubwa kama Marouane Fellaini au Paul Pogba, lakini kama unahitaji burudani ya soka utakiri kuwa amewazidi kwa kila kitu mastaa hao wa Old Trafford.

Ameshinda mataji mawili ya Ligi Kuu England akiwa Etihad na bado anaonekana kuwa silaha ya ushindi ya kocha Pep Guardiola.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -