Thursday, November 26, 2020

MAJERAHA YA CAZORLA YANAVYOIMALIZA ARSENAL

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

London, England

TAARIFA zilizotoka juzi ni kwamba nyota wa Arsenal, Santi Cazorla, hataweza kurejea uwanjani mpaka kumalizika kwa msimu  huu.

Kwa maana hiyo, mashabiki wa Gunners watarajie kumwona staa wao huyo msimu ujao.

Hata hivyo, wachambuzi wa soka wanaamini kuwa kukosekana kwa fundi huyo ni pengo kubwa kwa Arsenal hasa kwa  Mesut Ozil.

Cazorla amekuwa akifanya kazi nzuri ambayo kwa kiasi kikubwa imekuwa ikimbeba Ozil na Arsenal kwa ujumla.

Wakati Mhispania Cazorla alipokuwa uwanjani, Arsenal walikuwa wakilingana pointi na Manchester City waliokuwa kileleni.

Kipindi cha miaka na miezi minne ambacho Cazorla amekuwa benchi, Arsenal imeyumba.

Staa huyo mwenye umri wa miaka 32, amekuwa sehemu muhimu ya safu ya kiungo ya Arsenal.

Katika mechi 85 alizoanza kikosini misimu minne iliyopita, Arsenal walikuwa na wastani wa pointi 2.15.

Mpaka sasa nyota huyo amekosa mechi 54 tu lakini tayari Gunners wameshuka na kuwa na wastani wa pointi 1.70.

Alipokuwa uwanjani, aliiwezesha Arsenal kushinda mechi sita za Ligi Kuu England.

Madhara makubwa ya kukosekana kwa Cazorla yapo kwa Ozil. Katika mechi tisa ambazo wawili hao wameanza kikosini, mechi pekee ambayo Arsenal walipoteza ni ile waliyocheza dhidi ya Paris Saint-Germain ambapo timu hizo zilitoka sare ya bao 1-1.

Tatizo kubwa la sasa katika safu ya kiungo baada ya Cazorla kuumia ni pasi za uhakika zenye macho.

Francis Coquelin hana sifa alizonazo mchezaji huyo katika kufanya kazi hiyo.

Ni Cazorla pekee aliyekuwa akiweza kumlisha mipira Ozil na kumfanya Mjerumani huyo kung’ara uwanjani.

Ni mechi tatu pekee ambazo wawili hao wamefanikiwa kumaliza dakika 90 za ligi wakiwa pamoja uwanjani, lakini wamefanikiwa kutengeneza ‘kombinesheni’ kali.

Katika mchezo dhidi ya Huill ambapo Arsenal walishinda mabao 4-1, pasi za Cazorla kwa Ozil zilikuwa 26, akifanya hivyo kwa dakika 67 pekee.

Kwa sasa Ozil amekuwa akitupiwa lawama na mashabiki wa Arsenal kwa kutocheza katika kiwango bora, lakini huenda ni kutokana na kukosa huduma bora ya Cazorla.

Ozil amefunga mabao mengi katika dakika 490 alizocheza akiwa na ‘babu’ Cazorla. Ni tofauti na idadi aliyofunga akiwa bila nyota huyo wa zamani wa Malaga.

Lakini pia, takwimu zinasema Ozil amegusa mpira mara nyingi kwa kipindi ambacho Cazorla alikuwa uwanjani.

Cazorla amekuwa akimpatia Ozil hasa kwa pasi zake za kupenyeza kama aliyotoa katika mchezo ambao Arsenal waliicharaza Chelsea mabao 3-0.

“Ni kweli lazima ‘utammis’ Cazorla,” alisema kocha wa Arsenal, Arsene Wenger, baada ya timu yake kukosa ushindi katika mchezo wa Oktoba mwaka jana dhidi ya  Middlesbrough.

Huo ulikuwa ni mchezo wa kwanza kwa Arsenal kuingia uwanjani bila huduma ya Cazorla.

“Kutoka katika eneo la kiungo hadi eneo la hatari la wapinzani, ni mwepesi wa kutoa pasi zake na ni za uhakika,” alisema Wenger.

Kukosekana kwa Cazorla kumesababisha safu ya kiungo ya Arsenal kukosa pasi za haraka kuelekea katika lango la timu pinzani huku Mohamed Elneny na Granit Xhaka wakionekana wazi kushindwa kuziba pengo la staa huyo.

Kuna taarifa zisizo rasmi kuwa huenda Cazorla akatimka Emiratse wakati wa majira ya kiangazi. Kama Cazorla ataamua kuondoka, basi Arsenal watakuwa na wakati mgumu kuhakikisha wanasajili mchezaji wa aina yake.

Licha ya taarifa kuwa Ozil na Wenger nao wanaweza kuondoka, lazima Arsenal ifikirie mara mbili juu ya uamuzi wake wa kumruhusu Cazorla kuondoka.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -