Wednesday, October 28, 2020

MAKAMBO ACHAGUA PACHA YANGA

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

NA HUSSEIN OMAR


STRAIKA wa kigeni wa Yanga, Heritier Makambo, amesema ana uwezo wa kucheza pamoja na Ibrahimu Ajib kama ilivyo kwa Anthony Matheo kwa mafanikio makubwa kwani tayari ameshawasoma vilivyo wenzake hao.

Akizungumza na BINGWA jana, Makambo, alisema mabao waliyoyapata katika mchezo mmoja wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Mtibwa Sugar, ulitokana na uelewano wa muda mfupi na wawili hao, akiamini wanaweza kufanya makubwa zaidi baada ya kujifua nao kwa muda mrefu sasa.

“Mimi sina tatizo, kufunga ni sehemu ya kipaji changu katika mpira, hivyo yeyote nitakayecheza naye, nipo vizuri kwa sababu wote ni wachezaji wa Yanga,” alisema Makambo.

Alisema akicheza na Ajib anafurahi mno kama ilivyo anapopangwa na Matheo au Amissi Tambwe, kwani kila siku katika mazoezi, wamekuwa wakipewa nafasi ya kucheza pamoja kwa nyakati tofauti ili kutengeneza kombinesheni.

Katika mazoezi yaliyofanyika wiki iliyopita kwenye Uwanja wa Chuo cha Polisi Kurasini, Dar es Salaam, benchi la ufundi la Yanga chini ya Kocha Msaidizi, Noel Mwandila, wamekuwa na kazi moja tu, kuunganisha vipaji walivyonavyo kikosini hasa baada ya ujio wa Makambo, Mrisho Ngassa, Feisal Salum ‘Fei Toto’, Deus Kaseke  na Pappy Tshishimbi, ili kuunda jeshi la maangamizi.

Kwa kuwa wachezaji wote hao wapya ni mafundi, kazi pekee inayowakabili Zahera, Mwandila na kocha wa makipa, Juma Pondamali, ni kuwaelekeza mifumo na mbinu za timu yao hiyo, ikiwamo kuwajengea kombinesheni itakayowawezesha kuelewana na wenzao waliokuwapo ndani ya kikosi hicho.

Wakati huu Yanga inapojiandaa kuivaa Stand United katika mchezo wao wa pili wa Ligi Kuu Tanzania Bara, benchi la ufundi la timu hiyo linafahamu kuwa maandalizi yao hayo pia ndiyo yanayoweza kuwarahisishia kampeni yao ya kutwaa ubingwa msimu huu baada ya mwaka jana kuporwa na Simba.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -