Monday, October 26, 2020

‘Makambo akiendelea hivi benchi litamhusu’

Must Read

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian...

                Lulu Ringo, Dar es Salaam

Kocha Mkuu wa Yanga, Mkongo Mwinyi Zahera amesema endapo mshambuliaji wake, Haritier Makambo hatoacha vitu vya hovyo, kuendelea na aina mbaya ya uchezaji alio nao kwa sasa atamuweka benchi na asipobadilika kabisa atakaa jukwaani.

Kocha huyo ameyasema hayo jana baada ya kumalizika kwa mchezo wa Yanga na KMC, uliomalizika kwa Yanga kuibuka na ushindi wa goli 1-0, goli lililofungwa  na Feisal Salum (Fei Toto) dakika ya 89 baada ya mchezaji wa KMC Ally Ally kumfanyia madhambi Makambo katika eneo la hatari.

“Kama ataendelea na mambo ya hovyo kama kutolala usiku vizuri, kula vizuri, kufanya vizuri mazoezi na akaendelea na mchezo wake mbaya atakaa benchi na kama hatabadilika atakaa jukwaani kabisa sitaweza kumtumia tena na nilishamwambia aache hivi vitu,” amesema Zahera

Katika mchezo wa jana, kipindi chote cha mchezo Yanga walionekana kuelemewa na mchezo, hasa kwa mshambuliaji Makambo kushindwa kutuliza mipira pale anapopokea pasi kutoka kwa wenzake.

Mara nyingi ambazo mchezaji huyo alikua akipokea pasi alikua akikosa stamina na kunyang’anywa mpira miguuni hali iliyosababisha benchi la ufundi la Yanga na mashabiki wake kumlalamikia kwa makosa anayoyafanya kwa kuwa yaliigharimu timu kupata ushindi wa mapema.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya kuwa na umri wa miaka...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian Mbappe na Neymar, kwenye mechi...

IBRA:Kifaa kipya Konde Gang aliyetembea kwa mguu kumwinda Harmonize

NA BRIGHITER MASAKI UKITAJA vijana wanaofanya vizuri katika mziki wa bongo fleva, huwezi kukosa kumtaja msanii chipukizi anayefahamika zaidi...

Jay-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas

-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas New York, Marekani HAKUNA shabiki wa Hip hop asiyelifahamu...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -