Wednesday, October 21, 2020

MAKAMBO HATIHATI KUIVAA SIMBA

Must Read

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu...

NA HUSSEIN OMAR

MAUMIVU ya kumkosa mshambuliaji wake wa kimataifa wa Kongo, Heritier Makambo, huenda yakaendelea kuiumiza Yanga hadi wakati wa pambano lao dhidi ya watani wao wa jadi, Simba, Septemba 30.

Straika huyo ambaye hakuwa fiti baada ya kuumia katika mchezo wa tatu wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Coastal Union ya Tanga, jana aliukosa mchezo dhidi ya Singida United na ameonekana kuwa na tatizo kubwa ambalo litamfanya kukaa nje ya uwanja kwa wiki moja hadi mbili.

Makambo alishindwa kuendelea katika mchezo huo na kutolewa katika kipindi cha pili dakika ya 70, baada ya kupata maumivu ya nyama za paja ambayo yalimlazimu kutoka nje na nafasi yake kuchukuliwa na Amis Tambwe.

Kutokana na tatizo lake la nyama za paja, Makambo anaweza kuikosa mechi muhimu dhidi ya Simba kwa kipindi ambacho amepumzishwa kwa ajili ya kupatiwa matibabu.

Kukosekana kwa Makambo katika kikosi cha Yanga ni pigo, kwani katika siku za hivi karibuni amekuwa ndiye mshambuliaji tegemeo kwa Wanajangwani katika suala zima la upachikaji wa mabao katika kikosi hicho.

Akizungumza na BINGWA jana, Daktari wa Yanga, Edward Bavu, alisema Makambo anatarajiwa kuwa fiti kuanzia wiki moja hadi mbili na kwa sasa hivi, wanapambana kuhakikisha anakuwa fiti kwa asilimia zote na kuuwahi mchezo huo kama itawezekana.

“Ni kweli tuna majeruhi mmoja tu ambaye yupo ‘serious’, ni Makambo lakini tunapambana kuhakikisha anakuwa fiti na kuwahi mchezo dhidi ya Simba, kwani maumivu yake yanachukua wiki moja hadi mbili kuwa vizuri zaidi,’’ alisema Bavu.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya wanamuziki wa Tanzania ambao miongoni...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara  (VPL), utakaochezwa leo...

Mugalu atema cheche Simba

NA ASHA KIGUNDULA MSHAMBULIAJI wa Simba, Chris Mugalu, amesema wanakwenda mkoani Rukwa kupambana na kupata ushindi katika mchezo wao...

Malale aitisha Yanga

NA ZAINAB IDDY KOCHA Mkuu wa timu ya Polisi Tanzania, Malale Hamsini, amezisikia sifa za kocha mpya wa Yanga,...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -