Tuesday, November 24, 2020

Makocha hawa usiwazingue kabisa

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

LONDON, England

MASHABIKI wengi wa soka wamekuwa wakifurahishwa na ukorofi wa kocha Joes Mourinho.

Mara kadhaa kocha huyo amekuwa akiviteka vichwa vya habari za michezo kutokana na tabia zake za ndani na nje ya uwanja.

Katika klabu zote alizofundisha, Mourinho ana historia ya kuacha gumzo kutokana na ukorofi wake.

Hivi karibuni, alilimwa kadi nyekundu wakati kikosi chake cha Manchester United kilipokuwa kikicheza dhidi ya Burnley.

  1. Jose Mourinho

Kama ilivyowekwa wazi hapo juu, Mourinho si mtu wa kulaza damu pale anapoona ‘amezinguliwa’.

Akiwa na Real Madrid, Mreno huyo aliwahi kumjeruhi jichoni kocha  mwenzake wa Barcelona, Tito Vilanova.

Lakini pia, ndiye aliyempachika Wenger jina la ‘profesa wa kufeli’.

  1. Sir Alex Ferguson

Ingawa si mzungumzaji sana, Ferguson alikuwa mmoja kati ya makocha wakorofi kwenye mchezo wa soka.

Kwa nyakati tofauti, Mourinho na Wenger waliwahi kukutana na vita ya Ferguson.

Mara nyingi kocha huyo raia wa Scotland, alikuwa akizozana na waamuzi pale alipohisi wachezaji wake hawakutendewa haki.

Mbali na hilo, itakumbukwa kuwa aliwahi kuingia kwenye mzozo na Shirika la Habari la Uingereza (BBC).

Kutokana na uhasama huo, mkongwe huyo alikataa kufanya mahojiano na shirika hilo.

Kwa wafuatiliaji wa Ligi Kuu England, watakumbuka kuwa Ferguson aliwahi kumtupia kiatu aliyekuwa staa wake, David Beckham.

Kiatu hicho kilitua jichoni kwa kiungo huyo wa kimataifa wa England na sekeseke hilo lilichangia kwa kiasi kikubwa kuondoka kwake na kujiunga na Real Madrid.

  1. Arsene Wenger

Kwa kipindi chote cha miaka 20 alichokaa England, Wenger hajaepuka tabia za ukorofi.

Mpaka kufikia mwaka jana, Mfaransa huyo alikuwa amelimwa kadi nyekundu 80.

Alitupiana maneno na straika, Ruud Van Nistelrooy, wakati Arsenal ilipocheza na Man United na kitendo hicho kilimfanya atozwe faini ya Dola za Marekani 30,000.

Pardew, Mourinho na Alex Ferguson ni miongoni mwa makocha waliowahi kukutana na ukorofi wa Wenger.

  1. Harry Redknapp

Ni kocha mwenye jina kubwa England. Aliwahi kuzinoa Tottenham, Bournemouth, Southampton na West Ham United.

Redknapp hapendi ‘miyeyusho’ na katika hilo aliwahi kuingia kwenye mzozo na viongozi wa klabu zake.

  1. Ruud Gullit

Alicheza kwa mafanikio akiwa na timu ya Taifa ya Uholanzi kabla ya kugeukia kazi ya ukocha.

Alijijengea umaarufu mkubwa katika vitendo vya utovu wa nidhamu alipokuwa na Newcastle United.

Alikuwa na vita ya maneno na mastaa wa klabu hiyo, Geordie na Alan Shearer.

  1. Paolo Di Canio

Aliwahi kutikisa Ligi Kuu England akiwa mchezaji kabla ya kugeukia ukocha.

Mara kadhaa aliwahi kuhusishwa na vitendo vya kibaguzi.

Muitalia huyo ni mkorofi ile mbaya na kuna kipindi aliwahi kuzichapa na mchezaji wake.

  1. Glenn Hoddle

Kocha huyo wa zamani wa Tottenham alijijengea umaarufu mkubwa akiwa mchezaji.

Mara kadhaa alikuwa akikumbwa na adhabu kutoka kwa Chama cha Soka cha England (FA) kutokana na tabia zake za kupingana na maamuzi ya waamuzi.

 

  1. Alan Pardew

Kwa kipindi chote cha maisha yake ya soka, Pardew amekuwa kivutio kikubwa kutokana na tabia zake za ukorofi.

Mara kadhaa, Pardew aliwahi kutupiana maneno na Arsene Wenger.

Lakini pia, aliwahi kutoa kauli tata alipokuwa akimzungumzia kiungo wa zamani wa Chelsea, Michael Essien.

Akizungumzia rafu aliyocheza Essien, Pardew alisema ni kama kiungo huyo ‘alimbaka’ Ched Evans wakati walipokuwa wakigombea mpira.

  1. Arrigo Sacchi

Ni mmoja kati ya makocha wakorofi na wenye nyodo ile mbaya.

Kabla ya kustaafu aliinoa kwa mafanikio AC Milan.

Aliwahi kuwafundisha mastaa, Ruud Gullit, Marco Van Basten na Frank Rijkaard.

Kocha huyo amewahi kutoa kauli ya kibaguzi alipokuwa akizungumzia ‘academy’ ya klabu yake ya Milan.

“Katika academy yetu kuna idadi kubwa sana ya wachezaji weusi,” alisema.

  1. Brian Clough

Aliiongoza Middlesbrough kufikisha mabao 200 katika mechi 213.

Pia aliwahi kuzinoa Derby County na Leeds United na alitumia muda mwingi wa kazi yake ya ukocha akiwa na Nottingham Forest.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -