Wednesday, October 21, 2020

MAKOCHA HAWA WA KIZUNGU WATAWABEBA WAARABU AFCON 2017?

Must Read

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu...

LIBREVILLE, Gabon

HABARI ya mjini kwa sasa ni mtifuano wa fainali za Mataifa ya Afrika za mwaka huu (Afcon 2017), utakaoanza kesho nchini Gabon. Kwa mara ya kwanza, Gabon watajaribu kuchukua taji hilo la Afcon 2017 wakiwa kwenye ardhi ya nyumbani. Itawezekana?

Hata hivyo, mataifa ya Afrika Kaskazini yaani Waarabu wanapewa nafasi kubwa ya kuleta upinzani wa kutosha kwenye michuano hiyo. Mashabiki wengi wa soka wanajua kuwa Waarabu wamekuwa na maendeleo mazuri kwenye mchezo wa soka.

Katika michuano ya mwaka huu itakayoanza kesho Jumamosi na kufikia tamati Februari 5, Waarabu watakuwa wakiwakilishwa na Misri, Algeria, Tunisia na Morocco.

Timu zote hizo zina makocha wa Kizungu na wenye majina makubwa katika soka la Afrika. Lakini je, Wazungu hao wataziwezesha nchi za Kiarabu Afcon 2017?

Hector Cuper (Misri)

Kocha huyo raia wa Argentina ana umri wa miaka 61 na itakumbukwa kuwa alitua Misri kuchukua kibarua cha Mmarekani, Bob Bradley, ambaye alitimuliwa.

Miongoni mwa klabu kubwa alizowahi kuzinoa barani Ulaya ni Mallorca, Valencia na Inter Milan ambayo katika msimu wa 2000-03 aliiwezesha kumaliza ligi ikiwa nafasi ya pili. Kwa sasa kikosi chake cha Misri kinategemea zaidi mashambulizi ya kushtukiza ‘counter-attack’ huku kasi ya staa wake, Mohamed Salah, ikifanikisha hilo.

Ingawa Mafarao ni hatari kwa mashambulizi ya kushtukiza, ni wazembe mno katika kuzuia hatari za mipira ya adhabu.

Misri ndiyo timu inayoongoza kwa kuchukua mara nyingi ubingwa wa Afcon. Imetwaa taji hilo mara saba. Hata hivyo, Mafarao hao hawajashiriki Afcon kwa kipindi cha miaka saba iliyopita.

Moja kati ya sababu zinazotajwa kusababisha hilo ni hali mbaya ya kiuchumi inayosababishwa na machafuko ya kisiasa nchini humo.

Georges Leekens (Algeria)

Mbelgiji Georges Leekens, kwa sasa ana umri wa miaka 63 na wakati anakabidhiwa mikoba ya kuinoa Algeria kwa mara ya kwanza ilikuwa mwaka 2003. Wengi walitegemea angefeli hasa kutokana na mfumo mbovu uliokuwapo kwenye soka la nchi hiyo.

“Nilijua utakuwa mtihani mzito na ndiyo maana ilinichukua miezi miwili kufikiria. Lakini sikutaka kufikiria kuwa itakuwa ngumu kivile,” alisema Leekens alipokuwa akihojiwa na jarida la Voetbal.

Mafanikio ya kwanza ya Leekens yalikuwa ni kuiwezesha Algeria kufuzu Afcon 2004. Leekens alitangaza kuikacha timu hiyo  ambapo mashabiki wengi hawakufurahishwa na uamuzi wake huo lakini alirejea kwao Ubelgiji na kujiunga na klabu ya Excelsior Mouscron.

Hii ni mara yake ya pili kuinoa Algeria na sasa kila kitu kiko sawa ikiwamo uwezeshwaji mkubwa wa Serikali. Kikosi cha sasa cha Leekens kinatajwa kufanana na kile cha miaka ya 1980 kilichokuwa na mastaa kama Rabah Madjer na Lakhdar Belloumi. Kwa sasa, Algeria ina Yacine Brahimi, Riyad Mahrez na Islam Slimani.

Henryk Kasperczak (Tunisia)

Kama ilivyo kwa kocha Leekens, Kasperczak mwenye umri wa miaka 70 ni miongoni mwa makocha maarufu kule Kaskazini mwa Afrika. Ni nyota wa zamani wa timu ya Taifa ya Poland na alikuwa  sehemu ya kikosi cha Taifa hilo kilichofuzu fainali za Kombe la Dunia za mwaka 1998.

Kasperczak amepoteza mechi moja pekee katika michezo yake 10 iliyopita.  Aliiongoza Tunisia kutinga Afcon 2017  na pia timu yake inaongoza Kundi A katika mechi za kuwania kufuzu fainali za Kombe la Dunia za mwaka 2018.

Kocha huyo anafahamika vyema kwa mfumo wake wa kujilinda na mara nyingi hutumia mabeki watano. Hata hivyo, wapo wanaodai kuwa kikosi chake hakijakutana na timu vigogo barani Afrika. Silaha kubwa ya kocha huyo ni safu yake ya ulinzi kama timu hiyo ilivyofanya katika fainali za mwaka 2015. Nguzo yao ya safu ya ulinzi ni Wahbi Khazri wa Sunderland.

Herve Renald (Morocco)

Kocha Renald ana umri wa miaka 48 na ni mmoja kati ya makocha wenye majina makubwa hapa Afrika. Kabla ya kutua Morocco, aliwahi kuzinoa Zambia na Ivory Coast, ambazo zote alizipa ubingwa wa fainali za mataifa Afrika.

Baada ya kuwa kocha pekee aliyeweza kubeba taji la Afcon akiwa na timu mbili tofauti, Renard aliamua kurejea kwao Ufaransa ambako alipata dili la kuinoa Lille ya Ligi Kuu nchini humo ‘League 1’.

Hata hivyo, haikuchukua zaidi ya miezi sita kabla ya kibarua chake kuota nyasi na ndipo alipoamua kurejea Afrika na kukubali ofa ya kuifundisha Morocco. Huenda sasa anataka kuifukuzia rekodi ya kuwa kocha aliyenyakua taji la Afcon akiwa na timu tatu tofauti.

Safu ya ushambuliaji inaweza kumpa jeuri ya kufikia mafanikio hayo. Hakim Ziyech wa Ajax, Oussama Tannane (Saint-Etienne), na Younes Belhanda (Nice), ni miongoni mwa mastraika wanaoweza kumpa jeuri katika mashindano ya Afcon 2017.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya wanamuziki wa Tanzania ambao miongoni...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara  (VPL), utakaochezwa leo...

Mugalu atema cheche Simba

NA ASHA KIGUNDULA MSHAMBULIAJI wa Simba, Chris Mugalu, amesema wanakwenda mkoani Rukwa kupambana na kupata ushindi katika mchezo wao...

Malale aitisha Yanga

NA ZAINAB IDDY KOCHA Mkuu wa timu ya Polisi Tanzania, Malale Hamsini, amezisikia sifa za kocha mpya wa Yanga,...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -