Friday, December 4, 2020

Malale aitisha Yanga

Must Read

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

NA ZAINAB IDDY

KOCHA Mkuu wa timu ya Polisi Tanzania, Malale Hamsini, amezisikia sifa za kocha mpya wa Yanga, Cedric Kaze, akisema hana hofu kwa sababu anajua kuwa yeye ndiye atakayemfundisha raia huyo wa Burundi namna soka la Tanzania linavyochezwa.

Polisi Tanzania itakuwa ugenini kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam kesho kutwa kuwakabili Yanga katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Kikosi cha Malale leo kinatarajiwa kuanza safari ya kwenda Dar es Salaam kutoka Moshi, mkoani Kilimanjaro tayari kuikabili Yanga, ikiwa ndiyo timu ya kwanza kumjaribu Kaze tangu aliposaini mkataba wa kufanya kazi na Wanajangwani hao.

Akizungumza na BINGWA jana kabla ya mechi yao dhidi ya Gwambina, Malale alisema kuwa amesikia na kuona sifa zinazotolewa kwa Kaze jambo ambalo kwake linamwongezea hasira za kukifua kikosi chake ili kupata ushindi.

“Kila kona hivi sasa anazungumzwa Kaze, natamani mchezo wetu na Yanga ungeanza kabla ya Gwambina ili niweze kumfundisha jinsi gani mpira wa Tanzania unachezwa na una watu wa aina gani.

“Sio vibaya mashabiki kumsifia kocha wao, lakini sioni kama anaweza kuwa bora mbele ya kikosi changu,” alitamba Malale, akisisitiza wana kila sababu ya kuvuna pointi tatu mbele ya Yanga kutokana na ubora wa kikosi chake.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul 'Ben Pol' ameshukuru mashabiki kwa...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -