Tuesday, October 20, 2020

Malale alia ukame wa mabao JKT Ruvu

Must Read

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu...

NA ESTHER GEORGE

KOCHA Mkuu wa JKT Ruvu, Malale Hamsini, amelia na ukame wa mabao kutokana na washambuliaji wake kupoteza nafasi za kufunga Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.

JKT Ruvu waliibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Mbeya City katika mechi iliyochezwa juzi kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya, lakini Malale amesema walikosa mabao mengi.

Malale alisema amegundua upungufu katika safu ya ushambuliaji kwani inakosa utulivu uwanjani.

Alisema wangeweza kupata mabao mengi zaidi lakini washambuliaji wake walionekana ni tatizo katika umaliziaji.

Malale alisema mechi hiyo imewapa changamoto kwani atahakikisha anafanyia kazi upungufu uliojitokeza ili kuweza kufanya vizuri katika mechi inayofuata dhidi ya Mbao FC.

“Mechi ilikuwa na upinzani mkali kwa sababu kila timu ilihitaji pointi tatu, nimegundua upande wa ushambuliaji bado kuna tatizo,” alisema Malale.

Malale alisema ataendelea kuwapa mazoezi makali wachezaji wake ili kuweza kuwajengea ufiti na kuweza kukabiliana na wapinzani wao.

Alisema malengo yake ni kuona wanafanya vizuri ili waweze kushika nafasi za juu katika msimamo wa ligi hiyo.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya wanamuziki wa Tanzania ambao miongoni...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara  (VPL), utakaochezwa leo...

Mugalu atema cheche Simba

NA ASHA KIGUNDULA MSHAMBULIAJI wa Simba, Chris Mugalu, amesema wanakwenda mkoani Rukwa kupambana na kupata ushindi katika mchezo wao...

Malale aitisha Yanga

NA ZAINAB IDDY KOCHA Mkuu wa timu ya Polisi Tanzania, Malale Hamsini, amezisikia sifa za kocha mpya wa Yanga,...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -