Monday, August 10, 2020

MALINZI AKWAMA MAHAKAMANI

Must Read

Klabu zamiminika kuomba kutumia U/Nelson Mandela

NA ASHA KIGUNDULA UONGOZI wa Chama cha Soka Mkoa wa Rukwa (RUREFA), umesema umeanza...

Kipa mpya Azam atamba kumsaulisha Abarola

NA ZAINAB IDDY KIPA mpya wa Azam, David Kissu, ameuahidi uongozi na mashabiki wa...

Yanga: Hatuna mpango na wasugua benchi Msimbazi

NA ZAINAB IDDY UONGOZI wa Yanga, umesema hauna mpango wa kusajili wachezaji wanasugua benchi...

NA KULWA MZEE

KESI ya kutakatisha Dola za Marekani 173,335 inayomkabili aliyekuwa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamali Malinzi na wenzake wanne,  imekwama kuendelea na kuahirishwa hadi Juni 11 mwaka huu kwa sababu hakimu anayesikiliza kesi hiyo amepata udhuru wa kikazi.

Kesi hiyo ilipangwa kusikilizwa ushahidi huo jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri.

Mashauri hakuwepo hivyo kesi ilitajwa mbele ya Hakimu Mkazi, Martha Mpanze. Katika kesi hiyo upande wa Jamhuri umewaleta mashahidi wawili.

Katika kesi hiyo, mbali na Malinzi, washtakiwa wengine ni Selestine Mwesigwa, Nsienda Mwanga, Meneja wa Ofisi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Miriam Zayumba na Karani wa TFF, Flora Rauya.

Malinzi anakabiliwa na mashtaka 28 ya kula njama, kughushi, kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na utakatishaji wa fedha wa Dola za Marekani 173,335 (sawa na Sh 43,100,000).

Mwesigwa anakabiliwa na mashtaka sita  ya kula njama, kughushi, kuwasilisha nyaraka za kughushi na utakatishaji wa fedha.

Kwa upande wa mshtakiwa Mwanga anakabiliwa na mashtaka mawili ya utakatishaji wa fedha, mshtakiwa  Zayumba yeye anakabiliwa na mashtaka  tisa ya kughushi na Flora anakabiliwa na shtaka moja la kughushi.

Washtakiwa walikana mashtaka yanayowakabili, Malinzi, Mwesigwa na Nsiande wapo rumande kwa kuwa wanakabiliwa na mashtaka ya utakatishaji fedha huku wenzao Zayumba na Flora wapo nje kwa dhamana.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Klabu zamiminika kuomba kutumia U/Nelson Mandela

NA ASHA KIGUNDULA UONGOZI wa Chama cha Soka Mkoa wa Rukwa (RUREFA), umesema umeanza...

Kipa mpya Azam atamba kumsaulisha Abarola

NA ZAINAB IDDY KIPA mpya wa Azam, David Kissu, ameuahidi uongozi na mashabiki wa timu hiyo kuwa atajituma na...

Yanga: Hatuna mpango na wasugua benchi Msimbazi

NA ZAINAB IDDY UONGOZI wa Yanga, umesema hauna mpango wa kusajili wachezaji wanasugua benchi katika klabu ya Simba kwa...

TSHISHIMBI KUMFUATA MORRISON SIMBA

NA ZAINAB IDDY KIUNGO wa Yanga, raia wa DR Congo, Papy Tshishimbi, anatarajiwa kumfuata winga wa kikosi hicho, Bernard...

TSHISHIMBI KUMFUATA MORRISON SIMBA

NA ZAINAB IDDY KIUNGO wa Yanga, raia wa DR Congo, Papy Tshishimbi, anatarajiwa kumfuata winga wa kikosi hicho, Bernard...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -