Monday, November 23, 2020

MAMBO 10 USIYOYAJUA KUHUSU ANGEL DI MARIA

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

PARIS, Ufaransa

ANGEL di Maria ndiye aliyekuwa chanzo cha kifo cha Barcelona katika mchezo wa Jumanne ya wiki hii uliochezwa jijini Paris, Ufaransa.

Akiwa na uzi wa PSG, Di Maria alipasia nyavu mara mbili na kuifanya timu yake hiyo kuibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Barca katika mchezo huo wa kwanza wa hatua ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Mabao mengine ya PSG yalifungwa na mastaa, Julian Draxler na Edinson Cavani.

Haya ni mambo 10 usiyoyajua kuhusu nyota Di Maria ambaye kabla ya kutua PSG aliwahi kuzichezea Real Madrid na Manchester United.

  1. Di Maria alizaliwa Siku ya Wapendanao ‘Valentines’ Day’ na hiyo ilikuwa mwaka 1988. Jina lake kamili ni Angel Fabian Di Maria Hernandez.
  2. Majeruhi sugu ya goti yalimfanya baba mzazi wa nyota huyo, Miguel, kuachana na soka kabla ya kutimiza ndoto yake ya kuichezea klabu aliyokuwa akiitamani ya River Plate.
  3. Di Maria alikaribia kutua Arsenal akiwa na umri wa miaka 20. Kipindi hicho alikuwa akiichezea Rosario ya Argentina. Kilichokwamisha uhamisho huo ni sheria za England ambazo zilibana kutoa kibali cha kufanya kazi.
  4. Klabu iliyompeleka Ulaya ni Benfica na hiyo ilikuwa mwaka 2009. Kwa miezi kadhaa aliyokaa klabuni hapo, jina lake lilianza kuvuma na ndipo mkongwe Diego Maradona alipomtabiria kuwa nyota wa Argentina katika siku za usoni.
  5. Katika kukumbuka maisha ya tabu aliyoishi na wazazi wake hapo mwanzoni, baada ya kusajiliwa na Benfica, alimwambia baba yake asifanye kazi yoyote na badala yake atamnunulia nyumba na kumlipa mshahara.
  6. Katika Fainali za Kombe la Dunia za mwaka 2014, Di Maria alitengeneza nafasi nyingi za mabao kuliko Lionel Messi aliyekuwa akicheza naye kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Argentina. Baadaye Di Maria alitangazwa kuwa mchezaji bora wa fainali hizo zilizofanyika nchini Brazil.
  7. Alipotua Manchester United kwa ada ya pauni milioni 59.7, alikabidhiwa jezi namba 7 ambayo ilivaliwa na mastaa wakubwa klabuni hapo; George Best, Bryan Robson, Eric Cantona, David Beckham na Cristiano Ronaldo.
  8. Mkewe, Jorgelina, ni Muargentina mwenzake na wamebahatika kupata mtoto mmoja wa kike. Hata hivyo, binti huyo aitwaye Mia alizaliwa akiwa njiti wa miezi sita na aliweza kuishi kutokana na msaada mkubwa wa jopo la madaktari wa jijini Madrid.
  9. Msimu uliopita, Di Maria alitajwa kuwa kinara wa pasi za mabao Ligi Kuu Ufaransa ‘Ligue 1’. Nyota huyo alitoa ‘asisti’ 18 na kumfunika aliyekuwa mchezaji mwenzake katika kikosi hicho cha PSG, Zlatan Ibrahimovich, aliyefanya hivyo mara 13.

10. Di Maria ni mmoja kati ya wachezaji wachache wanaomvutia staa Cristiano Ronaldo. Mreno huyo alipinga vikali uamuzi wa Real Madrid kumpiga bei Di Maria akiamini bado alikuwa akihitajika kwenye kikosi hicho

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -