Sunday, January 17, 2021

MAMBO 10 USIYOYAJUA KUHUSU CAVANI

Must Read

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi...

PARIS, Ufaransa

KWA sasa ndiye mfungaji bora wa PSG kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, rekodi aliyoiweka baada ya kuiongoza timu hiyo kuifunga Celtic mabao 5-0.

Katika ushindi huo mnono wa mchezo uliokuwa wa hatua ya makundi, straika huyo wa kimataifa wa Uruguay alipachika mabao 21, akimpiku Zlatan Ibrahimovic, ambaye alipasia nyavu mara 20 akiwa na PSG. Haya ni mambo 10 ambayo huenda hukuyajua kuhusu mpachikaji mabao huyo mwenye umri wa miaka 30.

  1. Nyota huyo amewahi kuziingiza vitani Juventus na AC Milan, ambazo zilimhitaji baada ya kung’ara katika michuano ya vijana ya Amerika Kusini mwaka 2007. Hata hivyo, ni Rais wa klabu ya Palermo, Maurizio Zamparini, ndiye aliyemnasa.
  2. Mwaka 2013, Cavani aliingia kwenye orodha ya wachezaji sita ghali katika historia ya PSG. Nyota huyo aliivunja rekodi ya Radamel Falcao.
  3. Cavani, ambaye husherehekea ‘birthday’ yake kila inapofika Siku ya Wapendanao (Februari 14), alizaliwa katika Jiji la Salto, ambako pia alizaliwa na kukulia straika hatari wa Barcelona, Luis Suarez.
  4. Akiwa mdogo, alivutiwa zaidi na aina ya uchezaji wa aliyekuwa straika wa timu ya Taifa ya Argentina, Gabriel Batistuta. Hiyo inatajwa kuwa sababu ya Cavani kufurahia uhamisho wake wa kucheza Palermo, iliyoko Serie A ambako hata nguli huyo alicheza akiwa na Fiorentina, Roma na Inter Milan.
  5. 5. Kwa mujibu wa ripoti iliyotoka mwaka huu katika jarida la Forbes, Cavani anashika nafasi ya 15 kwenye orodha ya wanasoka wanaoingiza mkwanja mrefu kutokana na mishahara na dili za matangazo.
  6. Mshikaji ni mume wa mrembo Soledad Cabris Yarrus na ni baba wa watoto wawili; Bautista na Lucas. Kuna kipindi kulikuwa na utata katika ndoa yao hiyo baada ya mwanamama huyo kusema Cavani alikuwa akichepuka na ‘kidenti’ cha chuo kikuu. Cavani alinaswa na kisichana hicho wakiwa kwenye mgahawa mmoja wakipata msosi wa jioni.
  7. Cavani si miongoni mwa wanasoka wanaomvutia mtukutu Mario Baloteli. “Cavani ni mchezaji mzuri na namheshimu kama mfungaji bora, lakini hapa Ufaransa kwa watu makini nawakubali zaidi Di Maria na (Ramdel) Falcao”.
  8. Mwaka 2015, Cavani alilazimika kuomba radhi kwa kauli yake kuwa wapinzani wao katika michuano ya Copa America, Jamaica, ni wepesi kama zilivyo timu za Bara la Afrika. Si tu kwa Wajamaica, kauli hiyo ilionekana kulishushia heshima soka la Afrika.
  9. Akiwa ameiwakilisha Uruguay katika mechi 90 na kufunga mabao 38, Cavani amezidiwa na Luis Suarez katika orosha ya wafungaji wa muda wote wa timu hiyo na mwaka 2011 aliiwezesha kutwaa taji la 15 la mashindano ya Copa America.
  10. Kaka yake aitwaye Walter Guglielmone alikuwa straika wa Beijing Technology ya China kabla ya kustaafu, na mdogo wake, Christian, pia anacheza soka, licha ya kuwa ana umri wa miaka 31.

Marcelo, Madrid kimeeleweka bwana

MADRID, Hispania

HAKUNA mpango wa beki wa pembeni wa Real Madrid, Marcelo, kuikacha timu hiyo kama ilivyokuwa inaripotiwa hapo awali na hiyo ni baada ya Mbrazil huyo kusaini mkataba mpya wa miaka mitano na klabu hiyo.

Kwa mujibu wa vyanzo vya habari, nyota huyo ameongeza mkataba wa kubaki Santiago Bernabeu hadi Juni 30, 2022.

Akiwa na Madrid tangu aliposajiliwa akitokea Fluminense mwaka 2007, Marcelo, mwenye umri wa miaka 29, ameshinda mataji 17, yakiwamo manne ya Ligi Kuu Hispania ‘La Liga’ na matatu ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Taarifa ya kusaini mkataba mpya imekuja ikiwa ni baada ya Chama cha Soka nchini humo kumfungia mechi mbili kutokana na adhabu yake ya kadi nyekundu katika mchezo wa La Liga dhidi ya Levante, uliochezwa mwishoni mwa wiki iliyopita.

Nyota huyo alikumbana na adhabu hiyo baada ya kumpiga teke Jefferson Lerma, hivyo ataishia jukwaani wakati Madrid watakapozivaa Real Sociedad na Real Betis.

Marcelo ni mume wa mrembo Clarice Alves na ni baba wa watoto wawili, Enzo Gattuso Alves Vieira na Liam. Marafiki wake wakubwa ni Cristiano Ronaldo na Pepe.

Madrid hawajaanza vizuri safari yao ya kulitetea taji la La Liga msimu huu, kwani licha ya kuifunga Deportivo La Coruna katika mchezo wa ufunguzi,  wamejikuta wakitoa sare katika michezo miwili iliyofuata dhidi ya Levante na Valencia.

Katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, wameanza vizuri kulisaka taji lao la 13 kwa kuisambaratisha Apoel mabao 3-0.  Wakiwa nyumbani kwenye Uwanja wa Bernabeu, Madrid walijipatia ushindi huo mnono kwa mabao ya Cristiano Ronaldo aliyefunga mawili na Sergio Ramos.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na ndiyo maana timu hiyo imeshinda...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi Kuu Tanzania Bara katika kipindi...

JDart Nation wapanga kutawala Africa

CHRISTOPHER MSEKENA MWANAMUZIKI na bosi wa JDart Nation, JDart, amesema miongoni mwa mipango yake kwa mwaka 2021 ni kuhakikisha...

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki za Ligi Kuu Tanzania Bara...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -