Saturday, November 28, 2020

YALIYOMKUTA MOURINHO SASA YAMEGEUKIA KWA GUARDIOLA

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

MANCHESTER, England


HIVI karibuni kocha wa Manchester United, Jose Mourinho, amenukuliwa akisema kwamba anaipenda mno klabu hiyo kwa sasa, maneno hayo yanaakisi pia wakati mgumu alionao mpinzani wake jijini Manchester, Pep Guardiola.

Zaidi ya miezi miwili iliyopita, Mourinho alikuwa binadamu mwenye bahati mbaya katika dunia ya soka, hakufurahishwa na chochote kile ulichodhani anakifurahia!

Ukweli ni kwamba, alisumbuliwa mno na presha ya kuinoa United na alidai kwamba maisha ndani ya hoteli ya Lowry iliyopo jijini Manchester yalikuwa na ‘nuksi’ kwake.

Alipata shida mno ya kuhakikisha timu yake inafanya vyema uwanjani, hasa katika kurudisha imani iliyopotezwa na makocha wa zamani, Louis van Gaal na David Moyes.

Siku chache baada ya kutangazwa kuwa kocha mkuu wa United, Mourinho alianza kuonja joto ya jiwe; akaanza kwa kutimuliwa kutoka kwenye benchi lake la ufundi katika mchezo wao wa Ligi Kuu England dhidi ya Burnley uliomalizika kwa suluhu baada ya kuonesha utovu wa nidhamu kwenye eneo lake.

Mwezi mmoja baadaye alioneshwa kadi nyekundu tena na muda huu ni kwa kuipiga teke chupa ya maji wakati kikosi chake kikibanwa na West Ham na kulazimishwa sare ya bao 1-1.

United ilihangaika kutoka katikati mwa msimamo wa ligi licha ya kufanya usajili wa bei mbaya; Paul Pogba mchezaji ghali zaidi duniani kwa pauni milioni 89, Eric Bailly (pauni mil 30), Henrikh Mkhitaryan (pauni mil 30) na Zlatan Ibrahimovic kwa uhamisho wa bure. Mourinho alihaha mno kutafuta utambulisho wa United, kikosi kilikuwa kinacheza soka lisiloeleweka.

Wakati huo huo, Guardiola alitulia na wala hakuwa na presha.

Wiki moja baada ya Mourinho ‘kutoa povu’ kwenye mahojiano yake na waandishi wa habari juu ya mwenendo wa kikosi chake, City ilikuwa inafanya vizuri mno ambapo iliichapa Barcelona mabao 3-1 kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Ndio, kwa kitendo cha Guardiola kuifunga timu iliyompa jina alilonalo sasa, kiliwapa watu imani kwamba jamaa amekuja kutawala soka la England.

Kila mmoja alijua sasa amekuja kocha atakayebadilisha upepo mzima wa ligi hiyo. Alifanya vizuri kiasi cha kushinda mechi sita mfululizo za ligi ndani ya mechi kumi alizoshinda katika michuano yote.

Upande wa pili, Mourinho alikuwa kwenye wakati mgumu mno, timu yake ikikamata nafasi ya saba huku City ikiongoza kwenye msimamo.

Lakini sasa hivi upepo umegeuka, ile furaha aliyokuwa nayo Guardiola hapo mwanzo imetoweka na anadai kwamba huu ni msimu wake wa mwisho kufundisha soka huku Mourinho yeye mambo yake yanamnyookea.

“Kitu kilichonifanya niifurahie klabu hii na watu wake, kufanya kazi kwa ajili ya watu ni watu wenyewe. Watu hao ni mashabiki wa Manchester United ambao wana kumbukumbu ya nyakati tulizopitia na sasa ni mashuhuda wa nyakati nzuri tulizonazo.

“Ni watu ambao walisimama kwenye matamanio ya baadaye lakini walielewa ugumu wa kuyafikia na kila siku waliipa timu ushirikiano.

“Kwangu mimi hicho ni kitu cha muhimu, kinakufanya uzame kwenye mapenzi mazito na klabu.

“Nawapenda sana wachezaji wangu na umoja wao kama walivyo mashabiki.

“Ni vijana wazuri na ninaopenda kufanya nao kazi, nina furaha sana,” anasema Mourinho.

Kwa upande wa Guardiola mwenye umri wa miaka 45, yeye anadai kwamba mara baada ya miaka mitatu ya kuinoa City itakapomalizika, hataendelea tena. Na hata akiondoka kwenye klabu hiyo hataendelea kufundisha soka tena.

Maneno hayo ya kukata tamaa yalijumuisha hisia kwamba Guardiola yupo kwenye hatari ya kufukuzwa iwapo hataleta mafanikio ndani ya klabu hiyo.

Yeye yuko tofauti na Mourinho hivi sasa, hajazungumzia hata suala la kuwapenda wachezaji wake.

“Najitahidi kuwashawishi kwa sababu nahisi hiyo ndiyo njia nzuri ya kupata ushindi.

“Wanajiuliza kwanini tufanye hivi, lakini wakicheza zaidi wataamini zaidi.

“Inahitajika miaka kadhaa ili hilo litimie,” anasema.

Lakini kwa hali halisi ilivyo, Guardiola ataendelea kuwepo Man City kwa miaka hiyo kadhaa anayosema?

Mshahara wake wa mwaka ni pauni milioni 15, ni mshahara mnono kwa sababu waliomleta City walihitaji ndoto za klabu zitimie.

Watu wa karibu na klabu wanadai kwamba sababu kubwa inayomfanya Guardiola kuwa kwenye hali hii ni migogoro ya chini chini na uongozi wa klabu ambao ulimpatia kiasi kikubwa cha fedha kufanya usajili.

Alitumia pauni milioni 135.1 kufanya usajili katika majira ya kiangazi na sasa kinda la Brazil, Gabriel Jesus, naye ametua kwa dau la pauni milioni 28.6.

Na licha ya kukanusha kumhitaji beki wa kati wa Southampton, Virgil van Dijk, ukweli ni kwamba wamelenga kumnyakua kitasa huyo kwa ada ya pauni milioni 50.

Pesa yaweza kuwa si kila kitu kwenye soka lakini maswali yanaendelea kuulizwa lengo la Guardiola lilikuwa ni nini kutumia fedha yote ile kama hapati furaha aliyoitaka?

Na upande wa pili, Mourinho amezama kwenye penzi zito na Manchester United yake, maisha ni mzunguko.

 

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -