Saturday, November 28, 2020

Mambo 10 usiyoyajua kuhusu Jay-Z

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

LOS ANGELES, Marekani

Ni mmoja kati ya wanamuziki wenye mafanikio makubwa nchini Marekani. Mbali na kujishughulisha na muziki wa hip hop, pia Jay-Z ni mfanyabiashara na mwekezaji mkubwa nchini humo.

Supastaa huyo ni mume wa mlimbwende Beyonce Knowless na wawili hao wamebahatika kuzaa mtoto mmoja wa kiume aitwaye Blue Ivy Carter.

Mwaka 2006, mkali huyo alitajwa na MTV kuwa ndiye anayeshika namba moja kwenye renki za wanamuziki bora wa muda wote.

Moja kati ya albamu zake zilizojizolea umaarufu mkubwa ni ‘Reasonable Doubt’ aliyoiachia mwaka 1996, ‘The Blueprint’ ya mwaka 2001 na ‘The Black Album’ iliyofuata miaka miwili baadaye.

Mbali na hayo, yafuatayo ni mambo mengine usiyoyajua kuhusu rapa huyo ambaye hivi karibuni alitamka wazi kuwa asingempigia kura Donald Trump ambaye hata hivyo ndiye aliyeibuka kidedea kwenye kinyang’anyiro cha urais nchini Marekani.

  1. Jay-Z ni miongoni mwa watu wa mwisho kuzungumza na marehemu Notorious B.I.G kabla ya staa mwenzake huyo kupigwa risasi. Itakumbukwa kuwa B.I.G aliuawa kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana jijini Las Vegas. Tukio hilo lilitokea mwaka 1997 wakati alipokuwa akitoka katika moja ya ‘party’.
  2. Baba mzazi wa Jay-Z, Adnes Reeves, alifariki siku ambayo mwanamuziki huyo alipokuwa akisimamia shughuli za ufunguzi wa ukumbi wake wa usiku ‘night club’.

3. Tofauti na wasanii wengine, Jay-Z hana kawaida ya kuandika mistari kwenye daftari, anatunga kwa kichwa alafu anaingia zake studio kuiachia ngoma. Moja ya ngoma ambayo hakushika kalamu kuiandaa ni ile ya mkewe Beyonce iitwayo ‘Drunken Love’.

Wakiwa nyumbani, Beyonce alikuwa akiifanyia mazoezi ngoma hiyo kabla ya kwenda kuingiza ‘voko’ na hapo ndipo Jay-Z alipoanza kuingiza mistari na baadaye wakaenda zao studio.

4. Jay-Z anatajwa kuwa na utajiri wa Dola za Marekani milioni 550 na mpaka sasa ana tuzo 17 za Grammy. Mbali na muziki, nyota huyo anaingiza kiasi kikubwa cha fedha kutokana na biashara zake za mavazi na ‘dili’ za matangazo.

5. Mwaka 2005, mtoto wa dada yake aliyekuwa akifahamika kwa jina la Colleek D. Luckie, alifariki kwa ajali ya gari alilopewa na Jay-Z kama zawadi yake ya kuhitimu masomo ya chuo.

Jay-Z ni mmoja wa wamiliki wa timu ya mpira wa kikapu ya Brooklyn Nets. Ameshawahi kukiri kuwa anaipenda timu hiyo inayoshiriki NBA kuliko kitu chochote.
7. Kutokana na umaarufu na mafanikio yake, miaka kadhaa iliyopita, Chuo Kikuu cha Georgetown kilianzisha kozi maalumu inayomhusu Jay-Z. Kwa mara ya kwanza, kozi hiyo iliyopachikwa jina la ‘Sociology of Hip-Hop: Jay Z’ na ilianza na wanafunzi 40. Kozi hiyo inafundishwa na Profesa Michael Eric Dyson.

Jina alilopewa na wazazi wake ni Shawn Corey Carterm lakini alijiita Jay Z kutokana na kuvutiwa na aliyekuwa prodyuza wake, Jay-O. Imeelezwa kuwa mbali na kutengeneza midundo ‘beats’, Jay-O alikuwa mkali wa kutunga na kurap, hivyo Jay-Z alikuwa mmoja kati ya mashabiki wakubwa wa mshikaji huyo.
‘Birthday’ ya mshikaji huyo ni Desemba 4 kila mwaka, kwani alizaliwa siku hiyo ila mwaka 1969. Kila inapofika sherehe ya kuzaliwa kwake, Jay-Z huwa na kawaida ya kuangusha bonge la ‘party’ na wakati alipokuwa akisherehekea kutimiza umri wa miaka 45, alitumia Dola za Marekani milioni 3 kujiachia na washkaji akiwemo rafiki yake wa muda mrefu, Snoop Dog, ambaye hivi sasa anajiita Snoop Lion.
Tofauti na watu wengine tunaopenda umaarufu, wala Jay-Z hakutaka kuwa staa. Akilizungumzia hilo alipokuwa akihojiwa na Shirikika la Habari la Uingereza (BBC), alisema: “Sikutaka kuwa staa. Nia yangu ilikuwa ni kuelezea stori na kuzungumza ukweli.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -