Monday, October 26, 2020

MAMBO 10 USIYOYAJUA KUHUSU MAHREZ

Must Read

Boni Mwaitege amkalisha Mgogo

NA VALERY KIYUNGU KUPITIA shindano la Nani Zaidi linaloendeshwa na redio Passion Fm ya...

Mzuka warudi tena kwa s2kizzy

NA CHRISTOPHER MSEKENA SIKU chache baada ya kuvamiwa na kufanyiwa uharibifu wa studio zake...

The Yeamen waipiga ‘Shoti’

NA JEREMIA ERNEST MSANII kutoka kundi la The Yeamen, Suma Toto, amewaomba mashabiki wa...

LONDON, England

RIYARD Mahrez ni mmoja kati ya wachezaji tegemeo katika kikosi cha mabingwa watetezi wa Ligi Kuu England, Leicester City.

Siku chache zilizopita, nyota huyo wa kimataifa wa Algeria alinyakua tuzo ya Mchezaji Bora wa Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC).

Mahrez aliwabwaga wapinzani wake Sadio Mane, Yaya Toure na Piere-Emerick Aubameyang.

Hata hivyo, huenda mambo yafuatayo yanayomhusu mwanasoka huyo ni mageni miongoni mwa mashabiki wake na wale wa soka la Ulaya kwa ujumla.

  1. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 25 ni swahiba mkubwa wa kaka yake Paul Pogba, Mathias. Wawili hao walianza kujuana walipokuwa wakiicheza klabu ya Quimper ya Ufaransa.
  2. Mahrez ni mchezaji wa kwanza raia wa Algeria kupachika mabao (hat trick) Ligi Kuu England. Alifanya hivyo katika mchezo dhidi ya Swansea City, ambapo Leicester iliibuka na ushindi wa mabao 3-0.
  3. Staa huyo ni muumini wa Dini ya Kiislamu na mkewe, Rita Mahrez, ni raia wa Uingereza.
  4. Ingawa alikuwa na uwezo wa kuiwakilisha timu ya Taifa ya Ufaransa kwa kuwa ndiko alikozaliwa, aliamua kuichezea Algeria, nchi ambayo wazazi wake walizaliwa.
  5. Mshara wake wa sasa katika kikosi cha Leicester ni kitita cha pauni 55,000, kiasi ambacho ni zaidi ya Sh milioni 100 za Kitanzania.
  6. Mahrez ndiye aliyemshawishi staa Islam Sliman kujiunga na Leicester wakati wa majira kiangazi. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 28, alitua klabuni hapo akitokea Sporting Lisbon.
  7. Inadaiwa kuwa rafiki mkubwa wa Mahrez pale Leicester ni mpachikaji mabao hatari wa kikosi hicho, Jamie Vardy.
  8. Hakujua klabu ya Leicester inakopatikana kabla ya kujiunga nayo. Alieleza kuwa watu wengi nchini Ufaransa waliijua Leicester kuwa ni timu ya mchezo wa rugby na si soka.
  9. Mshikaji aliwahi kupitia maisha magumu kinoma. Siku moja aliiba baiskeli na hiyo ni baada ya kuiazima kwa kisingizio kuwa anakwenda kuchukua vifaa vyake vya michezo.

10. Aliwahi kuambiwa na mmoja wa makocha wake kuwa hawezi kutoboa kupitia soka. Kauli ya kocha huyo ilitokana na umbo lake dogo.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Boni Mwaitege amkalisha Mgogo

NA VALERY KIYUNGU KUPITIA shindano la Nani Zaidi linaloendeshwa na redio Passion Fm ya...

Mzuka warudi tena kwa s2kizzy

NA CHRISTOPHER MSEKENA SIKU chache baada ya kuvamiwa na kufanyiwa uharibifu wa studio zake za Pluto Republic, prodyuza nyota...

The Yeamen waipiga ‘Shoti’

NA JEREMIA ERNEST MSANII kutoka kundi la The Yeamen, Suma Toto, amewaomba mashabiki wa Bongo Fleva kuendelea kulipa sapoti...

JB Maeba atimiza ndoto zake na Cannibal

NA CHRISTOPHER MSEKENA MSANII wa Afro Pop na Bongo Fleva anayeishi Kenya, James Tesha a.k.a JB Maeba, amesema anafurahi...

‘Certified Lover Boy’ ya Drake yaiva

TORONTO, CANADA RAPA nyota ulimwenguni, Aubrey Graham maarufu kama Drake, ametangaza habari njema ya ujio wa albamu yake ya...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -