Wednesday, November 25, 2020

MAMBO 10 USIYOYAJUA KUHUSU N’GOLO KANTE

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

LONDON, England

JINA lake lilianza kuvuma msimu uliopita na hiyo ni kutokana na kiwango kikubwa alichokionesha akiwa na Leicester City.

Kama ambavyo mashabiki wa soka hawakutarajia kuiona timu hiyo ikinyakua taji la Ligi Kuu England, hakuna aliyewaza kuwa huenda NG’olo Kante angekuwa bonge la staa.
Mwanzoni mwa ligi, ilikuwa rahisi mno kumpotezea na kutoa nafasi kubwa kwa viungo, Cesc Fabregas, Yaya Toure, Granit Xhaka na wengineo.

Kante akawa zaidi ya hao na wengine ambao hawako kwenye orodha hiyo na hilo likawafanya Chelsea kumsajili na huenda mpaka leo mabosi wa Stamford Bridge wanajipongeza kwa dili hilo.

Makala haya yanakuletea mambo 10 usiyoyajua kuhusu kiungo huyo mwenye asili ya Afika, lakini anayeiwakilisha Ufaransa katika michuano ya kimataifa.

1. Mshikaji aliwahi kuitosa timu ya Taifa ya Mali na kuamua kuichezea Ufaransa. Viongozi wa Shirikisho la Soka la Mali walijaribu mara mbili kumshawishi Kante kuichezea timu yao lakini alikataa. Ingawa alizaliwa Ufaransa, wazazi wake ni raia wa Mali.

2. Kwa sasa Kante ni mmoja kati ya mastaa wanaolipwa vizuri England akiwa anakinga pauni 110,000 pale Chelsea. Mshahara huo ni mkubwa kuliko ule wa pauni 55, 000 aliokuwa akipewa na Leicester.

3. Kante si aina ya wachezaji wenye vituko vingi nje ya uwanja. Marafiki zake wamekuwa wakimtaja kuwa ni mpole. “Nje ya uwanja, alikuwa mpole sana lakini ndani ya uwanja ni kama shetani,” alisema rafiki yake, Left-back Fabien, mwenye umri wa miaka 34.

4. Umbo dogo lilikaribia kumnyima ulaji pale Leicester. Kocha msaidizi wa Leicester, Steve Walsh, alipompeleka Kante Leicester, haikuonekana kama angesajiliwa. Kocha mkuu, Claudio Ranieri, alitilia shaka umbo la Kante na mikikimikiki ya Ligi Kuu England.

5. Bao lake la kwanza kuifungia Ufaransa lilikuwa ni lile alilopachika katika mchezo dhidi ya Russia ambapo aliiwezesha timu yake hiyo kuibuka na ushindi wa mabao 4-2 kwenye Uwanja wa nyumbani wa Stade de France.

6. Kante aliipiga teke ofa ya kocha Jose Mourinho. Wakati wa dirisha la usajili la majira ya kiangazi, Manchester United ilikuwa ni miongoni mwa timu zilizokuwa zikiiwania saini ya nyota huyo lakini alikataa na kuamua kujiunga na Blues.

7.Kutokana na sura yake ya kitoto alipofika kwenye uwanja wa mazoezi wa Leicester kwa mara ya kwanza, mabosi wa timu hiyo walimuuliza: “Umekuja kumtafuta nani hapa?”

8. Katika msimu wake wa kwanza Ligue 1, hakuna mchezaji aliyepokonya mipira mara nyingi zaidi yake kwenye Bara la Ulaya.

9. Japokuwa hajawahi kuhudhuria onyesha lake hata moja, Kante anamuelewa sana kimwana Rihanna ambaye hivi karibuni alikuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na rapa Drake.

10. Wakati dunia nzima ikimtambua Kante ni nani, kocha mpya wa Chelsea, Antonio Conte, alidai kuwa jina hilo lilikuwa geni kwake kabla ya nyota huyo kutua Stamford Bridge kwa ada ya pauni milioni 30.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -