Sunday, January 17, 2021

MAMBO 10 USIYOYAJUA KUHUSU ROONEY

Must Read

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi...

MANCHESTER, England

STAA Wayne Rooney amewathibitishia wakosoaji wake kwamba hajakwisha licha ya umri wa miaka 31.

Mwanzoni mwa wiki hii, mkali huyo alipasia nyavu za Manchester City na kuiwezesha timu yake ya Everton kuambulia sare ya bao 1-1 katika mchezo uliozikutanisha timu hizo kwenye Uwanja wa Etihad na lilikuwa la 200 kwake tangu alipoanza kucheza Ligi Kuu.

Je, uliyajua mambo haya yanayomhusu mshambuliaji huyo wa kimataifa wa England ambaye alikuwa Manchester United msimu uliopita?

  1. Alitumia kitita cha pauni milioni moja katika sherehe ya harusi yake na bibiye Coleen. Wawili hao walikuwa wapenzi tangu shule kabla ya kuoana mwaka 2008 nchini Italia.
  2. Mshikaji ni muumini wa Dini ya Kikiristo, mfuasi wa dhehebu la Roman Katoliki. Mara nyingi amekuwa akinaswa akiwa na ‘rozali’ shingoni mwake na aliwahi kulisema hilo katika fainali za dunia za mwaka 2010.
  3. Nje ya soka, Rooney ni shabiki mkubwa wa mchezo wa masumbwi. Enzi hizo, mjomba wake alikuwa akimiliki ‘gym’ na mara kadhaa alikuwa akipanda ulingoni kuzitwanga na binamu zake katika mapambano ya kirafiki tu. Kipindi hicho, alikuwa akivutiwa zaidi na bondia Mike ‘Iron’ Tyson.
  4. Mwaka 2002, akiwa na umri wa miaka 16, Rooney alizomewa katika mechi yake ya kwanza Ligi Kuu England. Timu yake ya Everton ilikuwa inakipiga na Tottenham. Mashabiki wa Spurs walimzomea kila alipogusa mpira wakiuliza ‘wewe nani’.
  5. Rooney ni shabiki mzuri wa muziki wa hip hop na mara nyingi amekuwa akisikiliza kazi za wasanii 50 Cent na Eminem. Lakini pia, ni msomaji wa vitabu akivutiwa zaidi na vile vya mwandishi Harry Potter. Mwigizaji bora kwake ni John Travolta.
  6. Akiwa na umri wa miaka 17, nyota huyo alisaini mkataba wake wa kwanza wa kuichezea Everton na alikuwa akiingiza kitita cha pauni 8,000 kwa wiki. Kabla ya hapo, walikuwa wanampa pauni 75 kwa wiki.
  7. Ni mmoja kati ya mastaa wanaopenda ‘michepuko’. Wakati mkewe Coleen akiwa mjamzito wa mtoto wao wa pili, Rooney alitajwa kumlipa changudoa mmoja ili atoke naye kimapenzi. Baadaye ilivuja kuwa msichana huyo alikuwa ni Jennifer Thompson aliyekuwa na umri wa miaka 21. Pia, mwaka 2004, mtandao wa Sunday Mirror ulizinasa taarifa zake nyingine za kutoka nje ya ndoa yake.
  8. 8. Mwaka 2004, Newcastle ambao kwa kipindi hicho walikuwa moto wa kuotea mbali, walitaka kumng’oa Rooney pale Everton kwa pauni milioni 20. Newcastle walimtaka mchezaji huyo wakiamini angekuwa mrithi wa Alan Shearer. Hata hivyo, Everton walikataa na kuikubali ofa ya pauni milioni 27 kutoka Manchester United.
  9. Kama viongozi wa Chama cha Soka cha England (FA) wangezubaa, basi Rooney angeichezea timu ya Taifa ya Jamhuri ya Ireland. Huenda angekwenda kuungana na Robbie Keane kwenye safu ya ushambuliaji. Nyota huyo ana asili ya Ireland kwa kuwa mababu zake ni wazawa wa nchini humo.
  10. Aliposaini mkataba mpya na Man United baada ya mvutano wa muda mrefu, alikubaliwa ombi lake la kulipwa pauni 300,000 kwa wiki. Kwa kipindi hicho, alizidiwa na Samuel Eto’o, Lionel Messi na Cristiano Ronaldo pekee.
- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na ndiyo maana timu hiyo imeshinda...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi Kuu Tanzania Bara katika kipindi...

JDart Nation wapanga kutawala Africa

CHRISTOPHER MSEKENA MWANAMUZIKI na bosi wa JDart Nation, JDart, amesema miongoni mwa mipango yake kwa mwaka 2021 ni kuhakikisha...

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki za Ligi Kuu Tanzania Bara...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -