Wednesday, October 28, 2020

MAMBO 10 USIYOYAJUA KUHUSU WAYNE ROONEY ‘WAZZA’

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

MANCHETSRE, England

SIKU chache zilizopita, nyota wa Manchester United, Wayne Rooney, alivunja rekodi ya upachikaji mabao klabuni hapo iliyokuwa ikishikiliwa na mkongwe, Sir Bobby Charlton.

Rooney aliweka historia hiyo baada ya kufunga bao lake la 250 katika mchezo wa Jumamosi ya wiki iliyopita katika mchezo wa Ligi Kuu England ambapo Man United waliibuka na sare ya bao 1-1 dhidi ya Stoke City.

Bila shaka idadi kubwa ya mashabiki wa staa huyo wa kimataifa wa England wangetaka kujua mengi kutoka kwake.

  1. Rooney ni miongoni mwa mastaa wengi ambao walikuwa wakorofi katika enzi zao za utoto. Kuthibitisha tabia yake ya ukorofi, aliwahi kusimamishwa shule kwa siku mbili baada ya kupiga teke moja ya mashimo yaliyokuwa kwenye maabara ya shule aliyokuwa akisoma. Staa huyo alifanya hivyo kwa hasira ikiwa ni baada ya mpira wake kuharibika.
  2. Makali yake ya kupasia nyavu yalianza kuonekana akiwa kijana mdogo. Rekodi zinaonesha kuwa alianza kutema cheche akiwa na umri mdogo katika academy ya Everton. Akiwa na kituo hicho cha kukuzia vipaji, Rooney alifunga mabao 114 katika mechi 30. Kipindi hicho alikuwa na umri wa miaka 11.
  3. Alipokuwa na umri wa miaka mitano, alilazimika kulala kitanda kimoja na wazazi wake akidai kuwa alikuwa akiogopa majini aliokuwa akiwaona akiwa chumbani kwake. Rooney alisema alikuwa akiona shetani mwenye rangi ya kijani na njano.
  4. Licha ya utukutu wake alipokuwa shule, alikuwa akilipenda zaidi somo la dini. Inaelezwa kuwa katika masomo mengine, Rooney hakuwa anaelewa hata moja.

Katika mtihani wake wa mwisho wa elimu ya miaka nane, alifeli vibaya masomo mengine ikiwamo Kihispania na geografia.

  1. Rooney ni mmoja kati ya mastaa wenye vituko vingi ndani na hata nje ya uwanja. Alipokuwa Everton, aliwahi kummwagia maji ya baridi, David Moyes, ambaye alikuwa chooni. Hata hivyo, Moyes ambaye alikuwa kocha wake kwa kipindi hicho, hakujua ni mchezaji gani aliyemfanyia ‘miyeyusho’ hiyo.
  2. Alipoitwa kwa mara ya kwanza kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya England, mwaka 2003, Rooney alijikuta akipitiwa na usingizi katika moja ya vyumba vya hoteli. Mpaka kikao cha wachezaji wa kikosi cha kwanza kinaanza, mshkaji alikuwa akiuchapa usingizi.

Uongozi wa timu hiyo ulilazimika kuazima ufunguo wa akiba hotelini hapo na kufungua chumba chake ambapo walimkuta akiwa hajitambui.

  1. Rooney na mke wake wa sasa, Coleen, walikutana walipokuwa wanafunzi wa shule ya sekondari. Kipindi hicho walikuwa na umri wa miaka 16 kila mmoja. Wawili hao walifunga ndoa Juni 12, 2008. Sherehe ya ndoa yao ilikuja ikiwa ni baada ya uhusiano wao kudumu kwa kipindi cha miaka sita.
  2. Rooney ana mdogo wake aitwaye John ambaye anaichezea Chester. Dogo huyo mwenye umri wa miaka 23, aliwahi pia kukipiga Ligi Kuu Marekani katika klabu ya New York Red Bulls ambapo kikosi hicho kilikuwa na Thierry Henry.
  3. Aliposajiliwa na Man United, alikuwa ndiye mchezaji kinda anayelipwa fedha nyingi katika ulimwengu wa soka. Rooney alikuwa akiweka mfukoni kitita cha Dola za Marekani milioni 25 akiwa na Mashetani Wekundu hao.

10. Huenda wengi hawajui kuwa mbali na masumbwi, Rooney ni shabiki mkubwa wa muziki. Ni mpenzi wa chombo cha muziki aina ya gitaa. Unapowazungumzia wacharaza gitaa bora duniani mbele ya Rooney, basi hatakuelewa kama hutamtaja Paul McCartney.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -