Monday, November 30, 2020

MAMBO MATANO KUHUSU AHMAD

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

ADDIS ABABA, Ethiopia

UKURASA mpya kwenye Shirikisho la Soka Afrika (CAF) umefunguliwa, sasa Ahmad Ahmad ndiye Rais wa shirikisho hilo, akimwangusha Issa Hayatou wiki iliyopita.

Kuna mambo matano kuhusu kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 57 aliyepata kura 34 dhidi ya 20 za mpinzani wake.

Ameongoza FA Madagascar awamu tatu

Chama cha Soka cha Madagascar kilimchagua Ahmad kama rais kwa awamu ya tatu mwanzoni mwa mwaka huu.

Alinyakua kiti hicho bila kupingwa, akipata kura 21 kati ya 22, akishinda kwa zaidi ya asilimia 50 inayotakiwa.

Uchaguzi huo ulisimamiwa na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji wa CAF, Constant Omari, ambaye ni Rais wa Shirikisho la Soka la DR Congo (FECOFA).

Aliwahi kuwa waziri mara mbili

Ahmad aliwahi kuwa waziri wa michezo mara mbili nchini kwao Madagascar. Baadhi ya watu wanaomkosoa wanasema hakufanya vizuri kwenye nafasi hiyo na kudai kuwa hataweza kufanya lolote CAF.

Vice Senate President

Pia Ahmad ni mwanasiasa, ambapo kwa sasa ni Makamu wa Rais wa Maseneta wa Madagascar na ni miongoni mwa wenye ushawishi mkubwa nchini mwao.

Aliendelea kutembea Nigeria kuomba kura

Machi 2 mwaka huu, Ahmad alitembelea Nigeria, akiwaambia Rais wa Maseneta wa Nigeria, Bukola Saraki, Waziri wa Michezo Solomon Dalung na viongozi wa Shirikisho la Soka la Nigeria (NFF) kwamba, soka la Afrika haliwezi kuendelea kuendeshwa kizamani wakati mashirikisho mbalimbali duniani yanaongozwa na vijana, wenye nguvu na ubunifu.

Ampa upinzani mkubwa Hayatou

Kabla ya Hayatou kung’olewa CAF na Ahmad kwa mara ya kwanza baada ya kutawala awamu nane, alikuwa akiwashinda wapinzani wake wote aliowahi kukutana nao.

Kwa hoja yake ya mabadiliko, Ahmad aliweza kuwateka watu pamoja na kuonekana kama mwokozi wa shirikisho hilo kuliko kuendelea na mkongwe.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -