Tuesday, October 20, 2020

MAMBO NI MOTO STARS

Must Read

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu...

MWAMVITA MTANDA NA GLORY MLAY

*Amunike amwita Erasto Nyoni, jamaa atua kambini fasta 

*Ajib naye njiani, Cape Verde kazi wanayo kesho

KOCHA Mkuu wa timu ya Taifa, Taifa Stars, Emmanuel Amunike, amemwita Erasto Nyoni katika kikosi chake hicho kinachojiandaa kuivaa Cape Verde kesho katika mchezo wa kuwania kufuzu fainali za Kombe la Mataifa Afrika (Afcon 2019).

Mchezo huo utapigwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, ikiwa ni siku chache baada ya Stars kupokea kipigo cha mabao 3-0 kutoka kwa wapinzani wao hao kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Cape Verde.

Mara baada ya kupewa taarifa za kutakiwa Stars, Nyoni hakutaka kuremba, alifungasha virago vyake fasta na kuungana na nyota wenzake kambini kuimarisha safu ya ulinzi iliyoonekana kupwaya mno Cape Verde.

Akizungumza na BINGWA Dar es Salaam jana, Amunike alisema  amelazimika kuongeza nguvu katika safu yake ya ulinzi baada ya mabeki wake kumwangusha katika mchezo wao uliopita.

“Mechi ya Cape Verde ilikuwa ngumu sana kwa kuwa safu yangu ya ulinzi haikuwa imara, nimeona bora nimuongeze Nyoni kutokana na kiwango chake, najua anaweza kuisaidia timu katika mechi ijayo,” alisema Amunike.

Amunike alisema bado kuna matumaini makubwa ya kupata ushindi katika mechi hiyo ya kesho, kwani wachezaji wake wana uzoefu wa kuutumia vema uwanja wa nyumbani.

“Jambo ambalo linanipa matumaini ni kwamba huu ni uwanja wa nyumbani, nina imani (wachezaji) wanaweza kuutumia vizuri. Kuna mabeki ambao hawakucheza mechi ya awali, akiwamo Nyoni ambaye ameongezeka, nina imani watasaidia timu kufanya vizuri,” alisema Amunike.

Mbali na Nyoni, wachezaji wengine ambao hawapo Stars waliokuwa katika mipango ya Amunike, ni nyota wa Yanga, Ibrahim Ajib ambaye kocha huyo raia wa Nigeria, aliahidi kumpa nafasi baada ya kumwona akiifungia timu yake bonge la bao katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Mbao FC kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam wiki iliyopita.

Amunike aliliambia BINGWA kuwa atampa nafasi Ajib katika mchezo dhidi ya Lesotho:

“Nimegundua (Ajib) ni mchezaji mzuri, ana kiwango cha kimataifa, ninamuhitaji sana katika kikosi changu, lakini katika mechi ijayo (dhidi ya Cape Verde Ijumaa iliyopita), amechelewa, nitampa nafasi mechi dhidi ya Lesotho,” alisema.

Akithibitisha kuitwa kwa Nyoni, Meneja wa Taifa Stars, Dany Msangi, alisema ‘kiraka’ huyo ameongezwa kuziba pengo la Hassan Kessy atakayekosekana katika mchezo huo kutokana na kutumikia adhabu ya kadi mbili za njano.

Alisema Nyoni alijiunga na wenzake jana tayari kwa maandalizi ya mwisho kabla ya kushuka dimbani kesho kuwakabili Cape Verde kwenye Uwanja wa Taifa.

“Ni kweli mwalimu ameongeza nguvu kwenye kikosi chake kwa kumwita beki Erasto Nyoni, kocha amelazimika kufanya hivyo kutokana na kumkosa Kessy ambaye anatumikia adhabu ya kadi mbili za njano alizopata katika michezo dhidi ya Uganda na Cape Verde.

“Mbali na Kessy, mshambuliaji Thomasi Ulimwengu pia atakosekana katika mchezo huo kutokana na kuwa na kadi mbili za njano, licha ya kuwakosa wachezaji hao, bado tuna matumaini ya kufanya vizuri na kuibuka na ushindi,” alisema.

Msangi alisema kikosi hicho kinaendelea vizuri na mazoezi kuhakikisha kinaibuka na ushindi katika mchezo huo wa kesho, hivyo kujiweka vizuri katika mbio za kuwania kufuzu fainali hizo zitakazopigwa mwakani nchini Cameroon.

“Baada ya kuwasili, mwalimu jana (juzi) alikuwa na kikao na wachezaji kwa ajili ya kuangalia makosa yaliyojitokeza katika mchezo wa awali na kwamba kikosi hicho kilitarajiwa kuendelea na mazoezi jana jioni na leo asubuhi,” alisema Msangi.

 

 

.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya wanamuziki wa Tanzania ambao miongoni...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara  (VPL), utakaochezwa leo...

Mugalu atema cheche Simba

NA ASHA KIGUNDULA MSHAMBULIAJI wa Simba, Chris Mugalu, amesema wanakwenda mkoani Rukwa kupambana na kupata ushindi katika mchezo wao...

Malale aitisha Yanga

NA ZAINAB IDDY KOCHA Mkuu wa timu ya Polisi Tanzania, Malale Hamsini, amezisikia sifa za kocha mpya wa Yanga,...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -