Friday, November 27, 2020

MAMBO SABA YANGA WANAYOTAKIWA KUYAFANYIA KAZI ALGERIA

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA HUSSEIN OMAR


JUZI, mashabiki wa soka walishuhudia mchezo mkali wa Kombe la Shirikisho barani Afrika uliozikutanisha Yanga na MC Alger, kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Pamoja na kipindi kigumu ambacho Yanga wamepitia, ikiwamo mwenyekiti wao kupata misukosuko na ikiripotiwa kuwa mara kadhaa wachezaji wamekuwa wakicheleweshewa mishahara yao, hilo halikuwazuia kuibuka na ushindi wa bao 1-0.

Matokeo hayo yameipa Yanga nafasi finyu ya kusonga mbele, huku ikiwa ni faida kubwa kwa MC Alger, pindi timu hizo zitakaporudiana Machi 14 mjini Algies, Algeria.

Makala haya yanakuletea mambo saba ambayo mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu Vodacom Tanzania Bara wanapaswa kuyafanyia kazi ili waweze kusonga mbele baada ya filimbi ya mwisho ya mchezo huo wa marudiano utakaopigwa wiki ijayo.

Stamina

Wachezaji wa Yanga wanatakiwa kuongeza stamina kidogo ili iwe rahisi kwao kumudu kucheza soka la kasi wakiwa ugenini.

Hilo linatokana na ukweli kwamba nchi za Ukanda wa Kaskazini zinasifika kuwa na hali ya hewa ya baridi.

Kuwa na stamina ya kutosha kutawasaidia kuhimili kasi ya Waarabu hao ambao kwa vyovyote watacheza soka ya kasi na kushambulia.

Ni vema sasa Yanga wakaingia kambini mapema na kulifanyia kazi suala hilo, vinginevyo itakuwa ngumu kupata ushindi wakiwa ugenini.

Safu ya ulinzi

Katika mchezo wa juzi, pamoja na safu ya ulinzi kucheza kwa uelewano mkubwa, bado upande wa kushoto wa Yanga anaocheza Haji Mwinyi umeonekana kushindwa kwenda na kasi ya mchezo.

Licha ya kuweza kupanda mbele kusaidia mashambulizi, Mwinyi alionekana kushindwa kurudi mapema katika eneo lake na kumfanya beki Hassan Kessy kulazimika kuacha jukumu lake kusogea upande wa kushoto.

Kiungo bado tatizo Yanga

Bado sehemu ya kiungo imeonekana kuwa ni tatizo kwani viungo Said Juma Makapu, Thaban Kamusoko na Haruna Niyonzima walishindwa kuelewana na kuiunganisha timu.

Makapu alifeli kwa asilimia 50 katika suala zima la kukaba mtu kwa mtu na kuna wakati alionekana kujificha na kushindwa kufungua akiogopa kupewa pasi.

Hali hiyo ilimfanya Niyonzima na Kamusoko kulazimika kushuka chini eneo la robo tatu ya uwanja kuchukua mipira kupandisha mbele.

Kutokana na juhudi za wawili hao, timu iliweza kutulia katika kipindi cha pili na kucheza, ambapo Niyonzima na Kamusoko waliweza kusambaza vizuri mipira na kupata bao baada ya kuingia kwa Donald Ngoma.

Kwa kiasi kikubwa, Zamiseleni na kiungo wake wa ulinzi, Taonga Mbwembya, walionekana kuificha safu ya kiungo ya Yanga.

Ingawa Kamusoko alionyesha uhai kwa kiasi fulani kwa kuongeza nguvu eneo la kiungo, bado hakukuwa na umuhimu wa Makapu kumaliza dakika 90 katika eneo la kiungo wa ulinzi hasa katika mechi ngumu na muhimu kama ile.

Huenda mambo yangekuwa mazuri kama Kamusoko angecheza nafasi ya kiungo wa ulinzi, huku Haruna Niyonzima akicheza kiungo mshambuliaji kurudi kucheza kiungo wa kati.

Safu ya Ushambuliaji

Bado Yanga ina kazi kubwa katika mchezo wa marudiano mbele ya Waarabu kwani wanatakiwa kutumia siku chache zilizobaki kulifanyia kazi eneo la ushambuliaji.

Katika mchezo wa juzi, Kocha George Lwandamina alimwanzisha Obrey Chirwa kucheza kama straika wa mwisho wakati kiuhalisia Mzambia huyo ni winga.

Licha ya Chirwa kuonekana kuwasumbua mabeki wa MCA, alikosa umakini katika kumalizia pasi za mwisho kwani alipoteza zaidi ya nafasi tatu za kufunga.

Kocha Lwandamina anatakiwa kulifanyia kazi eneo hilo kwani linaweza kumsaidia kupata bao la mapema wakiwa ugenini na kutuliza presha ya mchezo kwa wachezaji wake.

Mabadiliko

Kutoka kwa Niyonzima na kuingia Emanuel Martin, ilikuwa ni kamari iliyochezwa na Kocha Lwandamina katika mchezo huo.

Hakukuwa na sababu ya kumtoa Niyonzima ambaye muda wote aliwafanya MCA hao kupoteana uwanjani kutokana na uwezo wake wa kukaa na mipira.

Katika mechi muhimu kama ile ambayo timu ilihitaji matokeo, Lwandamina hakupaswa kufanya mabadiliko yale, hasa baada ya kuingia kwa Donald Ngoma ambaye alishirikiana vema na Chirwa na kuifanya safu ya ushambuliaji ya Yanga kutulia.

Kuelekea mchezo huo wa marudiano, ni vema benchi la ufundi la Yanga likawa makini na mabadiliko wanayoyafanya ili kuepuka kurudia makosa.

Fitina

Viongozi wa Kamati ya Mashindano ya Yanga wakiongozwa na Paulo Malume wana kazi kubwa ya kuhakikisha wanatuma watu wao mapema Algeria, ili kuweka mazingira mazuri ya mahali timu itakapofikia na kufanyia mazoezi.

Waarabu ni wazuri sana katika fitina za ndani na nje ya uwanja lakini ni mafundi wa kuwatoa wapinzani mchezoni.

Wamekuwa wasumbufu katika suala zima la usafiri wa ndani, hoteli na uwanja wa mazoezi.

Hivyo, Yanga lazima watambue kuwa   wanakwenda vitani na si mchezoni. Wanatakiwa kujipanga kifedha katika suala zima la kukabiliana na fitina hizo za Waarabu, vinginnevyo hadithi inaweza kuwa ile ile ya siku zote.

Hamasa

Mbali na makosa kadhaa ya kiufundi kujitokeza katika mchezo huo, lakini kitu kingine viongozi wa Yanga wanachotakiwa ni kuongeza hamasa kwa wachezaji wao.

Ikumbukwe baada ya mchezo wa juzi kumalizika, wachezaji wa timu hiyo hawakuondoka pamoja uwanjani baada ya kuambulia ahadi hewa kutoka kwa viongozi wa timu hiyo juu ya malipo ya mishahara yao.

Lakini pia, kukosekana kwa mshabiki uwanjani ni hamasa nyingine waliyoikosa wachezaji wa Yanga katika mchezo huo wa juzi.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -