Saturday, October 31, 2020

MAMBO YA KUTARAJIA USAJILI WA JANUARI

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

LONDON, England

DIRISHA dogo la usajili linakaribia, ambalo litakuwa ni Januari mwakani na tayari baadhi ya klabu zimeshajua wachezaji watakaowasajili.

Manchester United watapeleka ofa kwa wachezaji kama 10 kwa ajili ya kikosi cha kwanza, ingawa nao watamuuza Bastian Schweinsteiger.

Wakati United wakionekana kuwa tayari kwa ajili ya kununua na kuuza Januari mwakani, je, dirisha hilo la usajili litafunguliwa na kufungwa lini na mambo gani tuyatarajie?

Dirisha hilo la usajili la Januari mwakani, litafunguliwa Jumapili, Januari 1, saa 6:01 usiku. Hivyo dili nyingi tutaanza kuzisikia Jumatatu, ingawa wapo ambao watawatangaza wachezaji siku ya kwanza kabisa.

Nyota kama Gabriel Jesus, alisajiliwa na Manchester City wakati wa kiangazi, lakini atatangazwa mwakani.

Baada ya kufunguliwa Januri 1 mwakani, litafungwa Januari 31 saa 5:00 usiku England na usiku mkubwa kwa nchi za Ulaya, ingawa pia tunaweza kuona dili nyingine zikikamilika baada ya dirisha hilo kufungwa.

Ikiwa kama masuala yote ya usajili yamekamilika kabla ya kufungwa kwa dirisha hilo la usajili, basi taratibu nyingine zinaweza kukamilika baada ya dirisha kufungwa.

Klabu za Ligi Kuu England zilitumia kiasi cha pauni milioni 165.4 kwa ajili ya dirisha dogo la usajili la Januari, mwaka huu.

Newcastle walitumia pauni milioni 26.3, Watford pauni milioni 26 na Norwich milioni 23, lakini Norwich na Newcastle zilishuka daraja.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -