Wednesday, October 28, 2020

Man City, Tottenham na Leicester zitatingaje 16 bora?

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

LONDON, England

KWA sasa Manchester City wako kwenye nafasi nzuri ya kuweza kutinga hatua ya 16 bora baada ya kuichapa Barcelona juzi Jumanne.

Kwa upande wa kikosi cha Arsene Wenger, Arsenal kiko kileleni mwa msimamo wa Kundi A wakifungana na Paris Saint Germain kwa pointi 10 baada ya michezo yao minne.

Baada ya kupambana kutoka nyuma kwa mabao 2-0 dhidi ya Ludogorets na kushinda mabao 3-2, Arsenal wamekwisha kutinga hatua ya 16 bora. Lakini kwa sasa Gunners wana changamoto ya kumaliza nafasi ya juu ya Kundi A na kukwepa kupangiwa na mojawapo ya timu kubwa kama akimaliza nafasi ya pili.

Kama Gunners watawafunga PSG mechi yao ijayo basi nafasi ya kwanza itakuwa ya kwao, lakini kama watapoteza watapaswa kushinda mechi dhidi ya Basel na PSG wapoteze mechi ya mwisho. Tofauti ya mabao itakuwa na umuhimu ili timu kuweza kusonga mbele, Arsenal wanahitaji kujihakikishia kuwa juu ya PSG ambao ndio wapinzani wao pekee.

 

Man City watafuzu vipi?

Baada ya kushinda mechi yao ya mwisho dhidi ya Barcelona juzi Jumanne usiku, Manchester City wamejiwekea mazingira mazuri ya kuweza kusonga mbele.

City wanaweza kujihakikishia nafasi ya kufuzu hatua hiyo ya 16 bora katika mchezo wao dhidi ya Borussia Monchengladbach, kama wakiweza kuibuka na ushindi dhidi ya klabu hiyo ya Ujerumani.

Kama wakipoteza mchezo wao dhidi ya klabu hiyo ya Ujerumani, City na Monchengladbach watafunga kwa pointi saba na kusubiria uhakika wa kufuzu kwenye mechi zao za mwisho za Kundi C, Desemba mwaka huu.

 

Leicester watatingaje?

Kwa kutoka sare na FC Copenhagen juzi Jumatano usiku, Leicester wamepoteza nafasi ya kufuzu hatua ya 16 bora, lakini wako kwenye nafasi nzuri kusonga mbele.

Wanahitaji ushindi mmoja katika mechi mbili zilizobakia na kuweza kukaa kileleni mwa msimamo wa kundi lao. Hata kama klabu hiyo ya Foxes itapoteza mechi yao inayofuata dhidi ya Club Brugge, lakini kikosi hicho cha Claudio Ranieri, bado kitakuwa na nafasi ya kufuzu kwenye mechi yao ya mwisho dhidi ya FC Porto mwezi ujao kama matokeo yatakuwa mazuri upande wao.

 

Itakuwaje kwa Tottenham?

Tottenham watakuwa na kazi ngumu kufuzu kwenye Kundi E baada ya kuchapwa bao 1-0 dhidi ya Bayer Leverkusen. Monaco wanaongoza msimamo wa kundi hilo wakiwa na pointi nane, huku Leverkusen wakishika nafasi ya pili wakiwa na pointi sita, Spurs wanashika nafasi ya tatu wakijikusanyia pointi nne, huku CSKA Moscow wako mkiani na pointi zao mbili.

Kutokana na matokeo hayo ya kuchapwa na Bayer Leverkusen, lakini ushindi wa mechi mbili zilizobaki utaivusha Spurs, lakini kama watapoteza dhidi ya CSKA kwenye mechi inayofuata watakosa nafasi hiyo ya kufuzu.

Hayo ndiyo makadirio ya klabu zote kwenye kundi hilo na Spurs wanaweza kumaliza kwenye nafasi yoyote kwenye timu hizo nne baada ya mechi mbili zilizobaki.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -