Monday, November 30, 2020

Man City wana bahati kinoma

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

MANCHESTER, England

MSIMU huu Manchester City wameanza vizuri mbio za kuwania taji la Ligi Kuu England ikiwa ni baada ya kushinda michezo yao yote sita.

Kwa upande mwingine, wengi wanahusisha mafanikio ya kikosi hicho na ujio wa Mhispania, Pep Guardiola.

Guardiola hajapoteza mchezo hata mmoja tangu alipokabidhiwa mikoba ya kuinoa Etihad.

Hata hivyo, wachambuzi wa soka wamehusisha mafanikio ya Guardiola na maamuzi ya waamuzi na wengine wamedai kuwa kikosi hicho kimetawaliwa na bahati msimu huu.

Katika mchezo wa ligi dhidi ya Sunderland, Man City walipata ushindi wa mabao 2-1.

Huku matokeo yakiwa sare ya bao 1-1, staa wa Sunderland, Paddy McNair, alijifunga na kuisaidia Man City kujizolea pointi zote tatu.

Kama si bao hilo lililofungwa zikiwa zimebaki dakika tatu kabla ya kumalizika kwa mchezo, mtanange huo ungemalizika kwa sare.

Katika mchezo wa ‘Manchester derby’ dhidi ya mahasimu wao Man United, mlinda mlango, Claudio Bravo, alistahili kadi nyekundu lakini mwamuzi ‘alipeta’.

Bravo ambaye uzembe wake ulichangia kupatikana kwa bao la Zlatan Ibrahimovic, alimchezea rafu straika na nahodha wa Man United, Wayne Rooney.

Rooney alikuwa wa kwanza kumiliki mpira lakini kipa huyo raia wa Chile alifika na kumwangusha.

Mchezo huo ulimalizika kwa Man City kuibuka na ushindi wa mabao 2-1, lakini huenda matokeo yangekuwa tofauti kama Bravo angelimwa kadi nyekundu.

Adhabu hiyo ingemfanya Bravo kukosa michezo mingine mitatu na hilo lingeiweka katika wakati mgumu safu ya ulinzi ya vijana hao wa Etihad.

Mchezo mwingine ambao Man City walibahatika na maamuzi ya refa ni ule uliowakutanisha na Swansea.

Vijana hao wa Etihad walizawadiwa penalti baada ya Kevin De Bruyne kujiangusha baada ya kuguswa kidogo na Mike van der Hoorn.

Penalti hiyo ilifungwa na straika Muargentina, Sergio Aguero na baada ya hapo mambo yakawa mazuri kwa Manchester City ambapo walishinda mabao 3-1.

 

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -