Tuesday, November 24, 2020

MAN UNITED IMEAMKA NA KASI YA ‘4G’?

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

MANCHESTER, England

MBIO za kuwania taji la Ligi Kuu England hazitabiriki. Ni ngumu kutabiri bingwa, hasa kwa kipindi hiki ambacho hata mechi za mzunguko wa pili hazijaanza.

Mpaka Leicester wanachukua ubingwa msimu uliopita wa 2015-16, hakuna aliyekuwa akitegemea hilo lingetokea. Huenda hata Leicester walianza kuamini kuwa wamefanikiwa zikiwa zimebaki siku chache.

Msimu huu hakuna anayeizungumzia Leicester kwenye mbio za ubingwa, inaaminika kuwa hawawezi kurudia maajabu hayo na hata mwenendo wao wa kusuasua kwenye ligi unathibitisha hilo.

Pep Guardiola alitua England kwa mbwembwe zote ikiwamo kuwatahadharisha wapinzani wake kuwa anakuja kuleta mapinduzi ya soka England.

Ikiwa bado hata mzunguko wa pili haujaanza, tayari ameanza kutafuta visingizio. Tofauti na kauli yake hiyo ya mwanzo, hivi karibuni ameibuka na kusema: “Hata Sir Alex Ferguson ilimchukua miaka mingi kuchukua ubingwa.”

Katika misimu kadhaa iliyopita, hasa baada ya kuondoka kwa Ferguson, Man United wamekuwa kwenye hali mbaya.

Msimu huu walianza vizuri na kuibua matumaini ya mashabiki wao lakini ghafla walipotea.

Baada ya kuyumba kwa muda mfupi, hivi sasa Man United wameonekana kusimama imara kwenye mbio za kuwania taji la Ligi Kuu England.

Kikosi hicho kinachonolewa na kocha mwenye maneno mengi, Jose Mourinho, kilikuwa na pengo la pointi tisa kuingia  ‘top four’.

 

Hata hivyo, baada ya kushinda michezo yake mitatu mfululizo dhidi ya Tottenham, Crystal Palace na West Brom, sasa wanahitaji pointi nne pekee kuwakamata Arsenal wanaoshika nafasi hiyo.

 

Hiyo imetokana na uzembe uliofanywa na Gunners kwa kukubali kichapo cha mabao 2-1 kutoka kwa Manchester City.

Kwa mujibu wa mchezaji wa zamani wa Man United, ambaye kwa sasa ni mchambuzi wa soka, Garry

Neville, kikosi hicho kimeamka.

 

“Nafikiri wameamka. Unaweza kuwaona wanavyoshangilia pamoja baada ya mechi, ni kama kuna morali fulani hivi inaanza kuwekwa.

“Ninayoiona sasa ndiyo Manchester yenyewe. Wachezaji wako vizuri, imechukua muda kidogo mambo kukaa sawa,” alisema beki huyo wa zamani.

Neville aliumwagia sifa ukuta wa Man United hasa mastaa, Marcos Rojo na Phil Jones, akidai kuwa ni mabeki visiki.

Aliongeza kuwa kiungo wa timu hiyo, Michael Carrick, naye ameonyesha kuimarika katika siku za hivi karibuni kutokana na ushirikiano wake na Paul Pogba na Zlatan Ibrahimovic.

Kwa upande wake, mchambuzi Graeme Souness, anaamini kuwa siri ya mafanikio ya hivi karibuni ya Man United ni Carrick na ‘Ibra’.

“Iko wazi, Ibrahimovic ni muhimu kama alivyo Diego Costa pale Chelsea, Ibrahimovic ni muhimu zaidi katika kikosi cha Man United,” alisema Souness.

“Nilisema tangu mwanzoni mwa ligi kuwa ili Man United iweze kuleta upinzani kwenye mbio za ubingwa, inamhitaji (Ibra) na nafikiri amethibitisha hilo.

“Mimi pia ni shabiki wa Carrick. Kwa nafasi hiyo, nafikiri ni wachezaji wachache wanaoukaribia uwezo wake,” alisema Souness.

Katika hatua nyingine, kutokana na ratiba ngumu ya kipindi hiki cha Sikukuu ya Krismasi, ametilia shaka idadi kubwa ya mastaa wazee kwenye kikosi hicho.

Amedai kuwa huenda ikawa ngumu kwa baadhi ya mastaa muhimu wakashindwa kuendana na kasi na ugumu wa ratiba kutokana na umri wao.

Nyota huyo ameongeza kuwa hakuna cha kufanya zaidi ya Mourinho kuingia kwenye soko la usajili la Januari.

“Nafikiri kuna mtihani mzito utakuja wiki chache zijazo kwa Carrick, Jones na Ibrahimovic kuwa kwenye ubora wa sasa kuelekea Krismasi,” alisema.

“Nafikiri Jose Mourinho atataka kufanya usajili mkubwa katika vipindi vijavyo vya usajili, kubadili kikosi kizima.”

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -